Kwanini wahanga wa mabomu Mbagala hawajalipwa fedha zao mpaka leo?

shaliza

Member
May 27, 2011
17
0
Ulipukaji wa mabomu katika kambi ya mbagala mwaka 2009 mwezi wa tano ulileta maafa hususani kwa wakaazi wa eneo hilo na viunga vyake,nyumba za wananchi zilibomoka kwa kupigwa na mabomu,zingine zilipata nyufa kubwa ambapo ni hatari kwa maisha ya wakazi hao,lakini cha kushangaza wale ambao hawajapata maafa makubwa wamelipwa hela nyingi za kuweza hata kununua kiwanja kingine na hata kujenga nyunba ingine nzuri kabisa ya kifahari,hapa kuna aina ya kaufisadi fulani kanakotembea kama kizungumkuti fulani.

nilijaribu kumhoji bwana fulani(jina lake tunaweka kapuni)alisema fedha alisema nyumba yake ni kubwa na ina hitilafu kubwa sana lakini kalipwa fedha kidogo sana kiasi hatakuweka mabati mapya ni tatizo,hata kubomoa nyuimba ili ajenge ipya pia hawezi kwa sababu hela aliyolipwani kama milioni moja hivi na elfu hamsini na sita wakati nyumba yake ilitakiwa alipwe kama milioni 15 ili aweze kufanya ukarabati sambamba na ujenziwa nyumba yake.

Mbagala ipo jimbo gani vile? Madiwani na mbunge wao wanatoka chama gani vile?! Wakati wa uchaguzi hawakuiweka hii kama ajenda mojawapo?! Wana haki ya kulipwa, lkn hakuna mtu atawaletea haki yao kwenye sahani wakiwa wamekaa. Wakawaulize wazee wa EA.

Ulipukaji wa mabomu katika kambi ya mbagala mwaka 2009 mwezi wa tano ulileta maafa hususani kwa wakaazi wa eneo hilo na viunga vyake,nyumba za wananchi zilibomoka kwa kupigwa na mabomu,zingine zilipata nyufa kubwa ambapo ni hatari kwa maisha ya wakazi hao,lakini cha kushangaza wale ambao hawajapata maafa makubwa wamelipwa hela nyingi za kuweza hata kununua kiwanja kingine na hata kujenga nyunba ingine nzuri kabisa ya kifahari,hapa kuna aina ya kaufisadi fulani kanakotembea kama kizungumkuti fulani.

nilijaribu kumhoji bwana fulani(jina lake tunaweka kapuni)alisema fedha alisema nyumba yake ni kubwa na ina hitilafu kubwa sana lakini kalipwa fedha kidogo sana kiasi hatakuweka mabati mapya ni tatizo,hata kubomoa nyuimba ili ajenge ipya pia hawezi kwa sababu hela aliyolipwani kama milioni moja hivi na elfu hamsini na sita wakati nyumba yake ilitakiwa alipwe kama milioni 15 ili aweze kufanya ukarabati sambamba na ujenziwa nyumba yake.

Kwanza jifunze kiswahili kabla ya kubandika vitu. Hawaitwi wahanga ila waathirika. Mhanga ni mtu aliye tayari kutoa uhai wake kwaajili ya imani, ushabiki nk

Hawajalipwa kwa sababu wanaadhibiwa kwa kuwachagua magamba kuongoza. Hiyo ndio shukrani ya magamba kwa wapiga kura wake. Next time watafanya maamuzi ya busara zaidi.

waziri mkuu wa japan amejiuzuru kuhusiana na maswala ya fukushima, mabomu mbagala, mabomu gongolamboto, waathirika mpaka leo hawajalipwa, waziri wa ulinzi yupo anawaza urais 2015

Unadai hao watu walipwe ww hujui gharama za tishert, kofia na yale mabango makubwa ya picha za JK, ulidhani vilitoka wapi?

waziri mkuu wa japan amejiuzuru kuhusiana na maswala ya fukushima, mabomu mbagala, mabomu gongolamboto, waathirika mpaka leo hawajalipwa, waziri wa ulinzi yupo anawaza urais 2015

atajitetea kuwa hiyo ni kaz ya Hazina.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom