Kwanini wahandisi wazuri sana duniani (Magari, Mitambo) wanapatikana nchini Ujerumani? Siri yao ni ipi hasa?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini ENGINEERS wazuri sana duniani (Magari, Mitambo) wanapatikana nchini Ujerumani? Siri yao ni nini hasa?

asdfdfdfgf.jpg


Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba;

Moja (1) Siku ya Ijumaa ilee ya wiki iliyopita nilimsindikiza mjomba wangu mmoja kule kariakoo kwenda kununua kipuri (spare) moja ya mshine ya kusagia unga kwa ajili ya kupeleka kijijini kwao kwa maana hii ndio biashara yake miaka nenda rudi.

Sasa baada ya kufika katika duka la baba mmoja mtanzani mwenye asili ya bara la asia (al maaruf kama mhindi) tukakuta ni kweli anayo spare ile ila zipo za aina tatu. Moja ni kitoka nchini Singapore, nyingine nchini China na ya tatu ni kutoka nchini Ujerumani. Sasa yeye akawa anamsisitiza mjomba wangu kwa lafudhi ya Kiswahili cha kihindi "chukua hii baba ipo genuine kabisa fresh from german" basi uncle akanunua, akalipa kisha sisi haoooo tukarudi zetu home.

Mbili (2) Vile vile inasemekana kwamba, mtu akianza kuendesha gari za Kijerumani kama vile Mercedes Benz, BMW, Audi au VolksWagen kwa namna zinavyokuwa nzito na kutulia sana barabarani, mtu huyo kamwe hatotamani tena maishani mwake kuendesha gari za Kijapan kama vile Toyota na Nissan.

Volkswagen-Mercedes-Benz-Audi-BMW-composite-badge-image-01-620x386.jpg


Tatu (3) Bila kuishia hapo, huku mitaani pia mara nyingi kumekuwepo na msemo maarufu kwa mfano utamsikia mtu akijigamba kwa rafiki yake kwamba "daaah mwanangu hii pasi tangia niinunue huu ni mwaka wa 8 sasa na sijawahi kuipeleka kwa fundi, chuma cha mjerumani hiki mzee baba"

Nne (4) Msafari wa Rais wa Russia ndugu Vladmir Putin umejaa gari za kijerumani tupu. Kuanzia BMW motorcycles; and Mercedes G-Class, Mercedes E-Class, S-Class mpaka BMW 5 Series. Tazama picha ya msafara wa Putin hapo chini.

5a103c45fc7e93d6218b4567.jpg


Sasa kwa kuzingatia scenario hizo zote nne (4) ndio nikajawa na maswali mengi sana akilini mwangu kwamba WHY ARE GERMANS SO GOOD AT ENGINEERING?

Kuna baadhi ya watu hapa watakuja kusema ninaisifia sana Ujerumani kwa maana ninauza vitabu vyao hahahahaaaaaa

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Mkapa.jpg


PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.
 
I am also wondering why Tanzania engineers are of the poorest quality. Look at tanesco engineers. Look at Tanroad engineers. Kukiwa na barabara ya kutengenezwa maengineer wa Tanroad watafuatilizia mule mule ilipo barabara iliyobuniwa na wananchi. Mfano. Mbezi Goba Mbezi beach. Mbezi Maramba majumba sita. Buza kwa Mpalange to Buza kwa lugola.
 
I am also wondering why Tanzania engineers are of the poorest quality. Look at tanesco engineers. Look at Tanroad engineers. Kukiwa na barabara ya kutengenezwa maengineer wa Tanroad watafuatilizia mule mule ilipo barabara iliyobuniwa na wananchi. Mfano. Mbezi Goba Mbezi beach. Mbezi Maramba majumba sita. Buza kwa Mpalange to Buza kwa lugola.
Why Buza?
 
Mkuu Hakika Mada Ina AFYA Sana Hasa KIPINDI HIKI Cha kuwa na RAIS mzalendo na mwenye maono ya KUSIMAMA WENYEWE na kutotegemea WAJOMBA WASIOKUWEPO huko nje....

Germany is a very interesting country...Kuna ya kujifunza....

1.Kiteknolojia
2.Kielimu
3.Kiviwanda

Wajerumani Wana msemo wao kuntu:
Wieetwas nutztsowirdes geputzt

Yaani "atumiaye kitu huking'arisha daima"............
 
I am also wondering why Tanzania engineers are of the poorest quality. Look at tanesco engineers. Look at Tanroad engineers. Kukiwa na barabara ya kutengenezwa maengineer wa Tanroad watafuatilizia mule mule ilipo barabara iliyobuniwa na wananchi. Mfano. Mbezi Goba Mbezi beach. Mbezi Maramba majumba sita. Buza kwa Mpalange to Buza kwa lugola.
Wahandisi wa TANESCO wao wana shida gani,huja tudokeza hilo.
 
Ukiacha UKOLONI.....

Vita viliwasaidia.....

Baada ya Vita ya Kwanza ya MABEBERU(Mimi siiti kuwa ya DUNIA)....
Wajerumani waliikuza HOFU DHIDI YAO.....WAKAIOGOPA HATARI KIVITENDO...WAKATAKA HAMU YA KUWA WAMOJA(SI HAWA CHADEMA wanaotaka machafuko na mifarakano mitandaoni)

Waliiogopa hatari ya kuwa DHAIFU KITEKNOLOJIA km vile aogopavyo JIRANI yetu PK...

Hofu iliwafanya WAAMUE kuwekeza kwenye ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU

ELIMU BORA....

Bahati Yao walikuwa na walimu wengi wa sayansi...

CHEMISTRY NA PHYSICS si siasa.........
 
Hao jamaa kabla ya tuzo za NOBELI KUTOLEWA walikuwa na walimu km kina MAGUFULI kibao....

Tuzo zilivyoanza KUTOLEWA WAKAZIZOA...WAKAZIBEBAAA WEE usiseme tuzo za MATUSI NA KUDHARAU MAREHEMU zinazotolewa pale mtaa wa UFIPA laa khasha....ni tuzo za CHEMISTRY na fizikia.......

Wao ndo waongozao kuchukua NOBELI...
 
Ujerumani haikufanya haya kwa bahati lakini kutumia vizuri mawazo, fikra na utendaji wa akili. Ni taifa linalohusudu zaidi elimu ya vitendo kushinda propaganda na maneno.

Ukiacha shule za awali na mwanzo, shule za kati na juu zinaelekeza zaidi utendaji.
 
I am also wondering why Tanzania engineers are of the poorest quality. Look at tanesco engineers. Look at Tanroad engineers. Kukiwa na barabara ya kutengenezwa maengineer wa Tanroad watafuatilizia mule mule ilipo barabara iliyobuniwa na wananchi. Mfano. Mbezi Goba Mbezi beach. Mbezi Maramba majumba sita. Buza kwa Mpalange to Buza kwa lugola.
Natamani ningesema kitu hapa lakini haya mambo ni ya vigogo ulichosema upo sahihi sana hiyo njia wanajua wenyewe ni nn wamefanya.
 
Lowassa alisema ELIMU ELIMU ELIMU..
HIKI ni kipindi Bora kbsa amsaidie magufuli KWA kumpa Siri ya ALIYOTUKUSUDIA ktka Yale MAFURIKO yaliyomzoa mwenyewe akiwa UKAWA....

Elimu ya ukweli ndio nyenzo wadau.....

Mwaka 2014 walipitisha SERA ya kutoa elimu ya vyuo Vikuu kuwa BURE...kwa watoto wa MALOFA...

Madogo kibao wanajibwedea mteremko wa kusoma BURE HATA kwa nchi maskini....
Nawashangaa CHADEMA,BAVICHA wanapata VINAFASI kupitia CDU...wao wakienda wanasoma VIKOSI VYA SIASA....bure kabisa hawa😥😥😥😥
 
Siri ya mafanikio ya wajerumani Ni
1. Kufanya kazi kwa weledi na kuthamini ujuzi wa mtu.
2. Ukweli na uwazi.
3. Bidii na kujituma.
4. Kuweka mbele maslahi ya taifa
5. Patriotism (kiswahili chake kimenitoka)
Saaaafiii.....
Oooo patriotism...UZALENDO...si kunywa faru john usiku huu halafu kesho WATU WAKAFANYE VURUGU AIRPORT KISA LISSU ANAKUJA....MIJITU haina UZALENDO hata ya kumkumbuka BABA YAO MKAPA aliyewaletea Sera ya utandawazi...Wana tandaa usiku huu kutukana watu afu kesho wapambane na POLISI daaaah

Where is patriotism guys?

Are we really SANE?!!!

UZALENDO UZALENDO UZALENDO Ni TUNU NI TUNU NI TUNU YA TAIFA LOLOTE....
 
Back
Top Bottom