Kwanini wahadhiri hawapelekwi tena kusoma 'postgraduate degrees' kwenye vyuo vyenye hadhi kubwa duniani kama ilivyokuwa zamani?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,518
Habari wadau,

Nimegundua wahadhiri wengi wa vyuo vyetu vikuu wapya kama udsm, udom, mzumbe etc hawaaandaliwi kwa kupewa elimu nzuri kama wazee wa zamani.

Ni kawaida sana siku hizi kukuta lecture cv yake imejaa local university tu kuanzia degree ya 1 mpaka Phd.

Huku ukicheki wahadhiri wazee Ma dr na ma prof waliosoma zamani unakuta top universities kwenye cv zao.

Mfano kina proff mkandala, proff mutahaba etc etc

Unakuta wamesomeshwa world class universities, vyuo kama stanford, university of california, university of illinois, cambridge, university of london,

Zile university ambazo kwenye ranking ya dunia zipo top 100 ndizo ma proff wetu wa zamani wamesoma.

Ila wahadhiri wa vyuo wapya wa sasa ni ngumu sana kumkuta mtu anasomeshwa chuo kikubwa mfano university of michigan, yale ama MIT

Kweli mwalimu wa chuo aliyesoma local university kuanzia cv mpaka u proff anaweza kweli kumfundisha mwanafunzi wa kisasa aweze kushindana kwenye soko la ajira ama kujiajiri? Mfano computer science prof aliyesoma bongo degree zote anaweza kumfundisha mwanafunzi kushindana na soko?
 
Hebu tupe research zao sio kuwasifia tu. Kama walienda Stanford na nchi haijaendelea hadi hakuna haja ya kuendelea kupoteza pesa, waache wasome hapa hapa maana hamna tofauti watakayoileta zaidi ya english ya American.
 
Labda sijakuelewa unamaanisha nini. Kwani hao maprof waliopelekwa top world universities si ilikuwa ni mbegu kwetu kama Nchi. Kwamba waje wawafundishe wengine wengi hapa kwetu.
Bro,
Mpaka leo kuna vyuo China kwa mfano kuajiriwa hata kama ni raia wake ni lazima usome nje ya nchi yao. Kama ni vinginevyo hawakuajiri hata ukiwa na GPA ya 5.0 degree na master's.
Sababu ni moja tu, wanaamini kwenye quality universities ili kupata quality lecturers na professors
 
Hebu tupe research zao sio kuwasifia tu. Kama walienda Stanford na nchi haijaendelea hadi hakuna haja ya kuendelea kupoteza pesa, waache wasome hapa hapa maana hamna tofauti watakayoileta zaidi ya english ya American.
Nakupinga wazi wazi mkuu.
Kuendelea kwa nchi ni political leaders ndio wako liable zaidi. Professors walio vyuo vikuu kazi yao ni kufundisha na kutafiti. Matumizi ya tafiti husika kwa maendeleo ni suala la viongozi wa nchi na siyo wahadhiri
 
Nchi imefika hapa ilipofikia kwa sababu ya majitu vilaza kama akina Msukuma, Kibajaji na Babu Tale. Mpaka wananchi tubadilike kwanza ndipo mambo yatakwenda sawa
 
Back
Top Bottom