Kwanini waganga wakubwa na wachawi wa kike kwa wakiume hawakosi magonjwa makubwa na ni maskini sana

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Nimejiuliza sana, kati ya waganga nilio wahi kuwafahamu au kuwatembelea na wale ambao marafiki zangu wachache wali wahi kuwaona hakuna ambaye nimewahi kutana naye ambaye hana magonjwa makubwa kama Presha, HIV, au kwa wanawake wana matumbo makubwa utadhani ni wajawazito, na ni maskini sana.

Ukienda kwao watakwambia wanatibu hayo magonjwa ila kwenye familia zao au wao wenyewe wanayo hawawezi kujitibu na kuwatibu wana familia wao.

Watakwambia tutakupa dawa ya biashara ili ufanye biashara upate pesa zaidi huku wao wenyewe hawamiliki biashara au ndugu zao hawamiliki biashara, familia zao zinakuwa ni maskini sana, je pesa alizowahi kukusanya kwenye uganga au uchawi haiwezi kuanzisha biashara ili na wao waitumie dawa ili wapate hela nyingi.

Watakwambia atakufanyia dawa ili uwe tajiri umiliki mapesa mengi sasa unajiuliza kwanini akufanyie wewe wakati yeye, ndugu zake na watoto wake wana maisha duni sana kwanini asiwafanyie nao wapate hayo mapesa.

HIVI SISI HUWA NI VIPOFU AU TUMELOGWA KUDANGANYWA
 
unajua nikwasababu gani pamoja na huo uwongo wao kujionesha wazi lakini bado wana exist?

nikwasababu wajinga wapo na wanaendelea kuzaliana

imagine umemjua mganga kupitia tangazo alilolipia pesa ndefu litangazwe kwenye redio au TV halafu anakuja kukuambia eti ana dawa ya kuwavuta wateja na wewe unakubali

kwanini mganga alipie tangazo kwa pesa nyingi ili kuwapata wateja wakati mamluki yamejaa tele kwenye tunguli?
 
Ni kwasababu wanajua ugumu wa masharti ya kuupata huo utajiri. Kosa moja unageuzwa nyama ya shetani.
 
Nikipata muda ntaandika kuhusu biashara na waganga. Haya Mambo tunaelewa sie tulioajiriwa na kitu biashara! Dunia Ni zaidi ya ujuavyo.
 
Bado hujakua na kuifahamu dunia! Hao unaowaita waganga ndo waliiwezesha Afrika kuishi vyema kabla ya ujio wa Waarabu na Wazungu Afrika!

Walitabiri na mambo yakatimia, walionya wakasikilizwa.
 
Back
Top Bottom