Kwanini wafanyakazi wenzangu wanaepuka kukaa nami kwenye basi la kazini?

FUTURE HUNTER

JF-Expert Member
Apr 30, 2018
1,726
2,000
Ha haaaa iko nuka domo kama sio kwapa bhebhe!!!!😄😄😄😄
Natania mkuu huenda bado watu hawakuelewi vizuri mazingira ya kazi.Watu hawapendi kuwa karibu na mtu ambae hawamjui vema
 

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
16,951
2,000
Kuna watu huwa hawaoengei sana wanaitwa "introverts" kuna wale wanaoongea sana wanaitwa "extroverts". Kajifunze zaidi kwa muda wako. Hiyo "ana kanyaro" futa kichwani kwako na wasaidie huko Bukoba na Rwanda kufuta vichwani mwao.

Huyo siyo introvert, rudi kajifunze characteristics zao.

Huyo ana ringa na ana dharau.
 

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
3,927
2,000
Kwani wewe jinsia gani na hao wafanyakazi wenzako ni jinsia gani?, na ni watu wa rika gani?

Kama ni binti labda hawajakuzoea au mrembo sana na wanaogopa kuongea na wewe bila hata sababu ya msingi au wanahisi hautaonesha ushirikiano

Au labda ni waume za watu wanaona wasije hatarisha ndoa zao au wanamuogopa bosi labda anapitamo, who knows!

Ila kama mkuu wewe ni mwanaume, labda ni mdogo sana kiumri sasa wafanyakazi wenzio wanakuona bado mtoto mtoto hivi kama ni watu wa makamo wenye stress zao.

Kwani unajipulizia sana marashi?, ujue kuna marashi yanaweza kutenga na watu bila hata sababu za msingi basi tu hawakuchukii wala nini ni basi tu marashi yanaeakimbiza. Embu badili aina ya marashi uone itakuwaje.

Mwisho, jitahidi kusalimia wafanyakazi wenzio, kuwa na mtu wa furaha onesha tabasamu, changamka na usipende kutumia sana simu kubonyeza bonyeza ukiwa na wafanyakazi wenzio.
 

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
3,927
2,000
Aise kumbe tunatofautiana mimi ni mkimya kama wewe nikipanda kwenye gari nitafurahi kama sitakaa na mtu yeyote wala kuongeleshwa kifupi sipendi story isiyo na mwisho wa kuniingizia pesa mfukoni.

Hahah mkuu hii story imekuingizia shilingi ngapi kwani hahah, isije ikawa ni haupendi story kutoka kwa watu fulani fulani ila haujajijua
 

Kingfisher

JF-Expert Member
May 22, 2015
3,382
2,000
IMG_3212.jpg
 

Teenager

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
1,405
2,000
Mkuu just mind your own business na amini kila mtu ana opinions zake hivyo hutakiwi kuishi kwa ajili ya maneno na opinions za watu wengine bali uishi kwa ajili yako.

Uko too emotional jaribu kukaza.

Sijui una umri gani lakini ukifika 60 utagundua hakuna aliyekuwa anakuangalia unaishije au unafanya nini.
Na utagundua ulipoteza muda wako kuishi opinions na perspective za wengine.

I think Steve Jobs alisema life's too short to live someone's life.
And he's dead now kama angeishi maisha yake kuishi maisha na opinions au perspective za wengine basi leo apple isingekuwepo.
Na ukumbuke huwezi kucontrol mtu mwingine sababu binadamu ni wabinafsi.

So ukisikia sijui mtu anakwambia wewe huongei au bubu au unaringa au wanakutenga na blah blah za opinions and stupid perspectives za wengine.

Just say who the hell cares?

Mkuu inaonekana uko too emotional na ukiendelea hivyohivyo basi utaishi kwa tabu sana considering life's too short.

Btw mimi ni mkimya kupitiliza na sioni shida yoyote na wala sijawahi kujiuliza maswali kama yako.
Hakuna kitu wala binadamu yoyote atanisumbua juu ya maisha or chochote kuhusu mimi easy like that.

Jaribu kukaza kidogo mkuu.
 

Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
2,481
2,000
Assumptions
1.Cheki usafi wa kwapa na mdomo wako( watu wakimya hunuka midomo kwasababu ya kutoshughulisha kinywa kwa muda mrefu).
2.Utoto:- huenda una mambo ya kitoto sana yanayowakera wenzio( hii ni kutokana na uandishi wako hapo juu, unaonekana unapenda watu wakuogope)
3. Huenda wanakuhisi mchawi/mshirikina.

"Usiku mwema"
 

mmewadadako

JF-Expert Member
Mar 29, 2019
493
1,000
Aise kumbe tunatofautiana mimi ni mkimya kama wewe nikipanda kwenye gari nitafurahi kama sitakaa na mtu yeyote wala kuongeleshwa kifupi sipendi story isiyo na mwisho wa kuniingizia pesa mfukoni.
hahaaa mimi pia mkuu hua napitia hii...sio muongeaji asee na mtu akiniongelesha naona kama namaliza energy

Kuna siku nilipanda daladala nikiwa nmevaa jezi ya Man U ...sasa jamaa mmoja akaja akakaa pembeni yangu alivyoona nmevaa ile jezi akaanza kuleta stori za mpira ...mara ooh jana naona mmempiga mtu tatu bila,.. mi nikawa namuitikia tu "noma sana","balaa","hatari tupu","aseee sio mchezo"mpaka akakaa kimya mwenyewe
 

Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
16,889
2,000
Angalia mdomo wako hautoi harufu? Muulize ndugu yako wakaribu, au muulize mtu wako wakaribu kuwa unamapungufu gani kwamaana wewe huwezi jijua
 

Mr. JF

Member
Dec 14, 2015
64
125
Mwanzoni sikuwa nachukulia serious hadi miezi ya hivi karibuni ilipotokea nimebadilisha makazi.

Kifupi mimi ni kijana, mtanashati, ila sio muongeaji sana kwa watu nisio na mazoea nao au katika mazingira mapya. Pia huwa sipendi kuzungumzia mambo mepesi mepesi kuhusu watu au vitu. Ni mara nyingi nimewahi kusikia kuwa watu husema Mimi ninaringa sana.

Sasa kuna kitu Kama nimekinotice siku za hivi karibuni. Nimehamia eneo lingine kikazi. Na asubuhi tunatumia Bus la kazini kwenda ofsini. Ila kuna kitu nimekiona na imekua Kama trend flani hivi. Nikiwa kwenye bus ambapo Kuna nafasi wazi tu ila watu wakiingia huwa as if wanakwepa kukaa seat niliyopo hadi seat yangu iwe last option. Hii imeibua maswali ndani yangu kwa nini iko hivyo wakati niko mazingira mapya !!

Je umewahi kukutana na hali hii? Na nini tafsiri yake?
Waweza jiona mtanashati lakini unatoa harufu kali zaidi ya beberu, na bahati mbaya waweza kuta husikii harufu yako, na the way you don't talk with people, no one atakuambia zaidi ya kukaa mbali na wewe! Kanunue perfume nzuri!

Otherwise utakua umetupiwa JINI kimavi, check na watu kama Mshana Jr watakusaidia zaidi!
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,589
2,000
Aise kumbe tunatofautiana mimi ni mkimya kama wewe nikipanda kwenye gari nitafurahi kama sitakaa na mtu yeyote wala kuongeleshwa kifupi sipendi story isiyo na mwisho wa kuniingizia pesa mfukoni.
Daah basi mpk sa hivi utakua bilionea aisee,maana kila anayekuongelesha ni story za mapesa tu.
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
5,634
2,000
Wewe utakua mchawi, mbinafsi, mjinga, mpumbavu, mpuuzi, na mwenye maringo ndio maana watu wanaku avoid at all costs.
Hata mtaani watu hawapendi wachawi na wapumbavu.
Unaweza ukawa umesoma lkn hujaelimika. Hata ndoa itakushinda.
Pia utakua unanuka mdomo kwasababu huongei. Pia unanuka kikwapa Piga mswaki Mara mbili kwa siku.
 

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
695
1,000
Sasa kuna kitu Kama nimekinotice siku za hivi karibuni. Nimehamia eneo lingine kikazi. Na asubuhi tunatumia Bus la kazini kwenda ofsini.
Acha kujishtukia! Umeshasema umehamia eneo lingine la kazi! Kwa maana nyingine tayari umekuta wafanyakazi ambao tayari wamesha-bond to each other! Sasa chukulia enzi unasoma, na-assume umesomea mjini kama Dar es salaam! Ile unafika kwenye daladala, unakuta siti kadhaa zenye mtu mmoja mmoja; je utakaa siti yoyote ile au utaangalia siti ambayo kuna mshikaji mnayefahamiana vizuri?!

Kuhusu kuringa, inawezekana ni kweli unaringa manake hapa wala sioni sababu iliyokufanya ujitambulishe kwamba wewe ni kijana mtanashati!!! Yaani hapo tu tayari umeshajenga dhana kwamba watu wanakuona unaringa kwa sababu tu wewe ni mtanashati!!! Na kama unajenga hiyo dhana, basi hata katika kujichanganya na watu unajichanganya kwa kusukumwa na hiyo dhana iliyopo kichwani mwako kwamba "usiniguse, utanichafua"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom