Kwanini Wafanyakazi wa TANESCO wananunua umeme ofisini?

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
4,664
4,760
Napenda kujua kwa nini staff wa TANESCO wananunua umeme ofisini?

Mimi nilikwenda pale TANESCO Ilala mkoani kuna dirisha la Teller ambapo Wafanyakazi wote wananunua umeme pale Jumatatu na Jumatano kama sijakosea

Hivi wao wanauziwa umeme bei gani? tofauti na wananchi ? Mwenye kujua anifahamishe
 
napenda kujua kwa nini staff wa tanesco wananunua umeme offisini . mimi nilikwenda pale tanesco ilala mkoani kuna dirisha la teller mastaff wote wananunua umeme pale jumatatu na jumatano kama sijakosea hivi wao wanauziwa umeme bei gani? tofauti na wananchi ? mwenye kujua anifahamishe
Wana unit za bure aisee ni nyingi hatari. Mita zao huwa zinajaa mpaka zinatema
 
Tofautisha azam hata muwe mnabeba lori zima , sio mali ya umma!!kuna kodi yoyote ya mwananchi inatumika hapo?!!kabla hujajibu kitu jaribu ku reason kwanza!
Point yako ni ipi Mkuu? Hao wafanyakazi sio Watanzania?Ni watanzania na ni sehemu ya Umma... Nao wana haki ya kunufaika kama wafanyakazi wengine wa makampuni mengine. Kila mtu ashinde mechi zake. Sio vibaya na wewe ukajipa ofa kwenye shughuli zako.
 
Ni kwanini watumishi wengine wa umma hawana privalage hizo?na hilo limeshaulizwa sana bungeni!!
 
Hivi kwanini masikini wengi wamejawa roho mbaya?
Hivi kwa mfano wafanyakazi wa Tanesco wanavyopewa motisha ya punguzo kwenye umeme wewe inakuathiri nini?
Dah!!
Mkuu kwenye elfu 10 mwanaichi wa kawaida anapata 28 units,lakini staff anapata units 200 kwa hyo hyo elfu 10.
Je hyo ni punguzo? Au uhujumu uchumi?

Tanesco wajitafakari.
 
napenda kujua kwa nini staff wa tanesco wananunua umeme offisini . mimi nilikwenda pale tanesco ilala mkoani kuna dirisha la teller mastaff wote wananunua umeme pale jumatatu na jumatano kama sijakosea hivi wao wanauziwa umeme bei gani? tofauti na wananchi ? mwenye kujua anifahamishe
Tumeweka njia lukuki za mteja kuweza kununua umeme je kuna njia inakukwamisha kununua umeme? Tulishaacha kuuza umeme kupitia ofisi zetu baada ya kuboresha njia mbadala za kununulia umeme,

Endelea kufurahia huduma

Endelea kuwa na amani
 
Tumeweka njia lukuku za mteja kuweza kununua umeme je kuna njia inakukwamisha kununua umeme? Tulishaacha kuuza umeme kupitia ofisi zetu baada ya kuboresha njia mbadala za kununulia umeme,

Endelea kufurahia huduma

Endelea kuwa na amani
Hujajibu Swali hata kidogo.

TANESCO ni SHIRIKA LA UMMA, kama hicho kinachosemwa kipo na mlikiweka kwa mujibu wa Sheria au Kanuni zilizoidhinishwa na Bodi ya Shirika huna hajja ya kuficha. Weka ushahidi wa kanuni au sheria na Useme wazi aina ya Watumishi wanaonufaika si dhambi kusema hilo kuliko majibu ambayo umetoa. It is uproffesional kutoa majibu tope kama uliyojibu hapo juu.
ATCL walikuwa wanatoa TRIP za ndege bureee kwa STAFF wao mpaka JPM alipofuta.
MAJESHI walikuwa wanatoa huduma za MANUNUZI yasiyo na Kodi kwenye SUPERMARKETS zao. Na mashirika mengine pia yana motisha tofauti tofauti wanazotoa kwa Watumishi wao kadri ya Sera za Taasisi.
Hivyo TANESCO hamnabudi kuweka wazi hii motisha yenu kwa Wafanyakazi wenu na mkafafanua ililenga nini hasa.
 
Back
Top Bottom