Sidhani kama ni lazima wewe unione barabarani na bango ndipo ujue kwamba naunga mkono madai, nafikiri uliona mgomo wa Walimu (watumishi wa Umma), Uliona jinsi Muhimbili ilivyokuwa mfano kwenye mgomo n.k Hoja hapa ni kwani wafanyazai wa Umma wapo kimya kwenye madai ya marekebesho ya sheria mpya ya mafao? Majibu yangu na ya watu wengine ni kwamba ni kwa sababu watumishi wa Umma wanaoongozwa na sheria ya Utumishi wa Umma na kanuni zake wanalazimika kustaafu/kupata pension miaka 55 kwa hiari na 60 kwa lazima. Hoja ya kupinga sheria mpya ina mantiki kwa sababu ukiajiriwa Private unakuwa chini ya masharti ya NSSF (10/10) na unaweza kufukuzwa muda wowote. Sasa kwanini usubiri mpaka miaka 55? Wakati Mtumishi wa Umma anapoajiriwa anaambiwa kabisa pension yak ni after 55 au 60 years kupitia LAPF, PPF, PSPF na GEPF (5/15). HOJA YA KUDAI MAREKEBISHO NI YA MSINGI SANA MKUU NA KILA MTU ANAIUNGA MKONOmr liverpool! madai yako mengi! mfano: dr uli na mukoba, hawa jamaa! si watumishi wauma! ila angalia wanachokifanya, watumishi wenyewe kuuza sura tu! au na wewe mr liverpool umo?