Kwanini wafanyakazi wa mabenki wamewasaliti wenzao ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wafanyakazi wa mabenki wamewasaliti wenzao ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, May 4, 2010.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  May 4, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usaliti wa Wafanyakazi wa Mabenki na Taasisi za fedha.KAMA ulikuwa hujui basi kuna udugu mkubwa kati ya wenye mabenki/taasisi za fedha,mangimeza wetu, wafanyakazi wao, wanasiasa na wafanyabiashara.UBIA huu ni ule wa kuhakikisha kuwa pamoja na sera nzuri za maneno ni wao tu ndiowanaopata fursa ya kula na kuishi vizuri hapa nchini na sio wewe au mimi?Ni ubia unaojengwa kwa kuandaa pia vizazi rasmi vya kifalme katika makundi hayo hapojuu. Hii ina maana kwamba wewe kama mtoto wa Mtanzania wa kawaidia hata uwe nadigrii ngapi kama baba yako si mwenyebenki au mfanyakazi wa benki, mfanyabiashara,mwanasiasa au mangimeza sahau kabisa kupata ajira ya maana kwa sababuwatakaofikiriwa kwanza ni watoto wao wenyewe. Sawa ?Kwa hiyo sio jambo la kushangaa kuona wafanyakazi wa mabenki na waajiri waowameamua kuwasaliti wafanyakazi wenzao. Wewe utategemea nini wakati ambapo tarishiwa benki analipwa milioni moja; dereva milioni mbili; mpika chai laki tano....unashangaa..... basi hujayajua mabenki.Kwa maneno mengine, mabenki yanatukaanga sisi wafanyakazi wengine kwa mafuta yetuwenyewe. Dawa iwe nini? Viongozi wa TUCTA niwaambieni kitu kimoja ? Migomo ndugu zanguimepitwa na wakati. Ninaunga mkono kutomualika Mheshimiwa Rais kwenye sherehe zetu-safi sana. Maana hana shughuli yoyote hapo na angekuja angetia ndogongogo zakampeni za kurudishwa tena. Arudishwe lakini asiwe na shughuli yoyote na sherehezetu za wafanyakazi. Wageni wetu rasmi wanastahili kuwa wastaafu mbalimbali kutokandani na nje ya nchi ili waje watupe mikakati ya kupambana na wanasiasa na waajiri.Waalikwa wanaoweza kuchangia kubadili maisha yetu na sio kuendelea kutukandamiza nakutufanya tuamini tunastahili kulipwa tunacholipwa.Waheshimiwa viongozi wa TUCTA nasema migomo imepitwa na wakati kwa sababu kazi yenuleo inastahili kuwa ni nyie kupambana hadi tuwe na vitu vifuatavyo:1. Benki ya Wafanyakazi na Wajasiriamali Tanzania;2. Mfuko wa Huduma wa Afya wa wafanyazi wenyewe na sio ule tunaoibiwa na mangimezawa serikali;3. Hifadhi ya Jamii ya Wafanyakazi Wenyyewe chini ya chama chao cha wafanyakazi nasio ile ya kitaifa ambayo kazi yake ni kutuibia na haitusaidii chochote tukiwa hai;4. Hospitali zetu wenyewe tutakazoziendesha kwa ubia na madaktari na manesiwatakaojilpa vizuri na bado watoe huduma safi kwa wafanyakazi na ziada ya kujengamambo mengine.5. Vyuo vikuu na shule zetu wenyewe ili tuwaepuke wenye mashule ambao leo nao niwezi wa mchana kwa kutulipisha ada kubwa kuliko inavyostahili;6. Kuwa na mahoteli na migahawa yetu wenyewe ambao wafanyakazi watakula vizuri nabado tukapata faida ya kuwekeza na sio vyakula vibovu tunavyolishwa na matajirimjini;7. Wanamichezo wakijiajiri nao wawe sehemu ya wafanyakazi na sisi kama wafanyakazituwe na stadium zetu wenyewe ambazo zitatuingizia kitu fulani;8. Tuwe na majengo ya ghorofa kama lile la walimu pale Ilala kila mkoa;9. Tuwe na mabasi yetu wenyewe yanayoendeshwa kibiashara lakini kistaarabu nakiungwana.10. Tujiingize katika biashara mbalimbali ambazo zikisaidiana na benki yetututawaonesha hao wafanyakazi wasaliti wa mabenki na taasisi za fedha ni kwa kiasigani wananufaika na wanavyoweza kuathirika kama sisi WAFANYAKAZI HURU TUSIORIDHISHWANA MAKOMBO YA WAAJIRI WETU tukiamua kuwa huru kweli kweli! Mungu wabariki wanyongena maskini wa Tanzania, Mungu wabariki wafanyakazi wa Tanzania,Delete & Prev |
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Bongo hii kaka kila mtu anajali masilahi binafsi! Wafanyakazi wa mabenk kwa ujumla wana kaunafuu! Lakini kwa sababu ubinafsi wao wanaona kama watu wa TGSD hawawahusu! Mgomo huu kwangu mimi nautazama kama mwanzo mzuri! Umefika wakati sasa watz tukatae kuburuzwa! Tusimamie haki zetu hata kama ni kwa kukaa barabarani na kuumwa na mbu!
  Miaka mitano TUCTA inalalamika lakini hawasikilizwi halafu leo hii unaitisha majadiliano! Mara huna pesa ya kuwalipa! wakati unatoa misamahaya mabilioni ya mafuta kwa wawekezaji mjenga nchi unamkamua kwa kodi kubwa katika hicho kidogo anachopata! still unaanza kunyoshea kidole Oooh Mgaya! Oooh Mgaya! Inasikitisha sana kuona kiongozi wa nchi anayezungukwa na washauri kibao kuongea upuuzi kama huo! Eti anasusia kura zao! Utaokota huko kwa kina mbumbumbu mzungu wa reli!
   
 3. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kaka hao ndio wachangiaji wakuu wakati wa kipindi kileee
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Umesahau lingine! Hivi unafikiri hela ya kifisadi ikiingia kwenye account ya mkubwa na mfanyakazi wa benki akaamua naye kuhamishapo kamilioni kuna atakayekuja kudai? Maana wote ni wizi tu au teller akiamua kupunguza kwenye mabunda ya manoti kuna atakayegundua na hata akigundua atakwendaje kudai? akaseme kuwa katika zile billion moja taslimu mlizonipa nimekuta milioni moja inakosa! Hawathubutu. Hivyo mbali ya kuwa wafanyakazi wa mabenki tayari wako juu ya kile tunachodai, bado nao wanashiriki katika ufisadi! -Si wenzetu hawa.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sina hakika kama hatujateleza katika kuwalaumu wafanyakazi wa mabenki. Pamoja na kwamba nao ni wafanyakazi kama hao wengine lakini mgomo kama namna ya kushinikiza mabadiliko ni lazima uguse kero ya huyo anayetaka kugoma. Sasa kama wafanyakazi wa benki hawana kilio kinachofanana na wengine ni lazima wagome? wanagomea nini ilhali vichocheo vya mgomo haviwahusu? Mimi nafikiri kama dhana ya kugoma kwao ni kuunga mkono harakati za wale wanaonyanyaswa basi hiyo ni hiyari yao na wanapoamua kutoitekelza hiyari hiyo wasionekane wasaliti.

  Mimi nafikiri watu hao waachwe wapumzike kwani mafanikio ya mgomo huo yasingekwazwa kwa hao wachache ambao wameamua kutogoma. hata hivyo TUCTA wenyewe ambao walikuwa wana beep wameshatngaza kusitisha au kufuta mgomo huo!
   
 6. k

  kausha Member

  #6
  May 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 73
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wajinga ndio waliwao mimi ni mmoja kati ya wanachama walioadhimisha mei mosi Mnazi mmoja kiliichotupata mimi na wenzangu ni kushindwa kugundua siri na agenda ya viongozi wetu waliyokuwa nayo ukweli ni huu :- Baada ya sisi Baadhi ya mashirika ambayo tumeingia kwenye mgogoro ama na serikali au menejimenti za makampuni yetu kwa sababu mbalimbali chama chetu cha kisekta ambacho ni TUICO Kimekuwa dhaifu katika kuyashughulikia matatizo yetu kwa nia ambayo tulidhani ni nzuri wajaja wakaunda chama kingine cha kisekta sambamba na Tuico ambacho ni FIBUCA wakatangaza sera zao na kwa kuwa wengine tulikatishwa tamaa na TUICO tulijiunga ili kuiengua bila kuangalia nyuma tukidhani Fibuca itafanya kilichoishinda Tuico lakini wengi hatukujua kwamba chama hiki tulichojiumga nacho si mwanachama wa TUCTA tumejua hivyo wiki ya sherehe lakini pamoja na kujua hivyo bado tuliamini matatizo yetu kama wafanyakazi ni yaleyale tulitarajia ujumbe ambao ungetolewa na viongozii wetu ungekuwa ni sawa na wa TUCTA ajabu na kweli viongozi wetu wameonyesha udaifu ambao unanifanya nione aibu kuwa mwanachama wake badala ya kujenga mshikamano Fibuka inataka ipewe uwezo wa kuwa chama mpinzani wa TUCTA aibu kuvunja mshikamano Nadhani viongozi wako kwenye pay roll ya ............... wana JF msituhukumu
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,587
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Tatizo fibuca.
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mie naomba nitofautiane na wewe. Mimi ni muajiriwa wa serikali kwa hiyo miongoni mwa wale tunaoishi wa TS nini hizo. Lakini naongea binafsi yangu kwa jinsi ninavyoamini. Ukweli kabisa nisingegoma. Sikwasababu ya hotuba ya Rais, la hasha. Sikuona kama kuna haja ya kugoma. Yaani mantiki ya kugoma kwangu sikuyaona. Hv ni lini na wapi mshahara uongezeke kwa asilimia 300. Yapo mengi ambayo tungeyatumia kuonyesha ugumu wa maisha unaotukabali. Mf maandamo/mgomo juu ya inflation na ufisadi uliokithiri. Hili naamini lingeleta maana. Ila suala la kutaka mshahara wa zaidi ya 300,000 haliwezekani. Maana ukimaliza kulipa tu jiandae na inflation ya ajabu. yapo mambo ya msingi ila la mshahara TUCTA hawakufikiria.
   
 9. G

  Godwine JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  siku si nyingi watu watafahamu ukweli
   
 10. k

  kausha Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 73
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hayo yangetosha kuwa ujumbe wa Fibuca sio kudai nyadhifa za uwakilishi serikalini au kupewa msaada wa kujitenga na Tucta naweza kukubaliana na wewe swala la mishahara sio tatizo la Fibuca kwa kuwa hakuna taasisi mwanachama wake mweneye kima cha chini cha 104,000 baadhi kima cha chini ni 200,000 na wengine 325,000 ni upuuzi kwa mwanachama wa Fibuca kugoma kwa sababu ya kima cha chini wakati hicho kitakacholipwa bado ni kidogo kuliko anachopata sasa lakini je kodi vipi ? mifuko ya pensheni vipi zaidi ya kumkopesha waziri mkuu mstaafu wewe umekopa ngapi ? mafao yanayotolewa na mifuko hiyo yanawiana na uwekezaji wako? vitega uchumi vinavyo wekezwa kwa michango yako vinakunufaishaje? FIBUKA WABADLISHE MTAZAMO WASIJEKUWA TUICO II
   
Loading...