Kwanini wafanyabiashara wengi wa Dar es Salaam siyo waaminifu?

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
3,052
4,075
Watu wengi wanatamani sana kuagiza bidhaa mtandaoni kutoka Dar sababu bidhaa nyingi ni bei rahisi tofauti na mikoani lakini tatizo linakuja kwa wakazi wenyewe wa Dar wengi sio waaminifu.

Wanunuzi wengi wamekutana na kasumba hii ya kutapeliwa mitandaoni ikiwepo na mimi pia nilishawahi kupigwa nilimpa kazi IT anifanyie mwisho wa siku akapotea mazima, hivyo imefika mahali wengi wamekuwa hawana moyo tena kutaka kuagiza bidhaa wala huduma kupitia mtandaoni.
 
Biashara ya Tanzania imejikita katika uongo na utapeli. Usipotapeliwa utauziwa kitu fake. Usinunue kitu kwenye mitandao ya kijamii. Huko hadi kuna wanaume wanajifanya wanawake...ukijichanganya ukatuma nauli basi inakula kwako. Unakuwa blocked hapo hapo.

Same kuna watu watapost nauza hiki halafu anaweka very attractive price..kumbe mwizi.

Ukitaka kununua kitu, nunua kwenye website. Sasa hivi wafanyabiashara wengi makini wana website zao, na pia kuna marketplace kadhaa.
 
Watu wa Dar wanaishi kisanii sanii tu hawajui kutengeneza mifereji ya pesa kwa mda mrefu. Kila siku anaanza kitu upya unaweza kuta huyo mtu kweli ni IT ila tamaa zinamfanya asiiangalie kesho na kukupiga tu wakati huenda ungempatia michongo mingi zaidi kama angetenda kazi yake kwa uweledi.
 
Back
Top Bottom