Kwanini wafanyabiashara wengi huanza kuyumba mara baada ya kuchukua mkopo?

hii quote huwa ina niacha hoi NYUMBA HII INAUZWA IPO CHINI YA NMB BANK ......WAMI BRANCH MOROGORO...
 
Yan shughuli zako zinaweza kuwa poa.. Ila ukishavuta loan mikosi ndio inaanza hadi mtu unajikuta unashindwa kulipa mkopo.. Why?

Mikosi unamaanisha hali ya kutofanikiwa au kushindwa kufikia malengo? Mikosi unamaanisha hali ya kukabiliwa Na magumu? Vikwazo Na magumu Ni Kwa ajili ya kukufundisha.Ni ngazi ya kukufikisha kwenye ukamilifu.Ni tanuru la kuokea mema Na mazuri.Kama vile dhahabu isivyong'aa bila ya kupita kwenye moto mkali ndivyo nasi tusivyoweza onja mafanikio bila magumu Na vikwazo.Magumu Na mahangaiko ni njia ya kuelekea kwenye faraja.Na hivi mambo hayo yasichukuliwe katika Wanda hasi (negative dimension) bali chanya. Kuna mwandishi mmoja amehitimisha juu ya magumu Na matatizo yoyote yanayoweza kumkabili mwanadamu kuwa yote hayo sio tatizo kuwa nayo Bali tatizo laweza kuwa kutoyakabili.Ni hivi tatizo sio kuwa Na dhahabu yenye impurities Bali mwenye dhahabu kuogopa kuipitisha kwenye moto mkali ili ing'ae.Matatizo Ni daraja.Tatizo sio kukuta daraja njiani Bali kuogopa kuvuka upande wa pili.

Mkopo hugeuka Na kuleta matatizo ikiwa mtumiaji hakufuata sawa sawa kanuni za matumizi.Mkopo huleta magumu ikiwa mtumiaji amekumbana Na mambo ambayo hakuyatarajia.Njaa Kali, mafuriko, kifo, vita, kubomolewa eneo la biashara ghafla, kuibiwa Na mambo mengi uyajuayo usiyoyategemea.
Mkopo Ni pesa tu. Athari ya kitu chochote hudhihiri kutegemea Na mumiliki kakitumia vipi. Pesa sio ndugu yake Na "majini au mapepo" kama wale wa imani mwendokasi wanavyofundisha.Mafanikio ya jambo lolote yamo katika namna ulivyopiga picha ya mafanikio yenyewe.Ndio tuseme picha Ni ndoto.Ukipiga picha ndogo utapata Matokeo madogo.Ukipiga picha kubwa utapata picha kubwa.Ukiweka margin ndogo ya faida wakati unaenda kukopa kukitokea mtikisiko kidogo tu Lazima utaishia kwenda "kuombewa" kuwa biashara yako imetupiwa mizimu, uchawi Na majini.
 
Kukopa kuliko uwezo wa biashara alafu pesa nyingi inatumika tofauti na dhumuni la mkopo.
 
Wenye mabenki hufanya sabotage kwenye biashara yako ili ushindwe kulipa na eventually waichukue ile collateral uliyoweka, which in most cases huwa na thamani mara kadhaa ya mkopo uliochukua, hili liko wazi na linafahamika kwenye banking inner circles
 
Shida inakuja pale umekopa unafungua hotel ya Ml 5 sasa wengine wanaanza kwanza kununua vitu vya ndani makoch,flat screen mpya frij mpya muziki mpya,hujikuta mtaji umepungua ndio hapo hukoroga mambo kabisa
 
wap uko mara nying naziona mj mpya na tushikamane
na kuna jamaa nasikia wameuza gari noah ml 2 kihonda mkundi na kasepa mjin muda sana kamwachia mwanamke soo anadaiwa ml 7.5 kweli hutawala huu nyumba zitauzwa kama njugu....
 
Wengi wakishachukua mkopo wanasahau lengo hasa lililopelekea wakachukua mkopo. Hasa wafanyabiashara wengi hawana elimu ya biashara pia hao hao hawatenganishi faida na hasara ya biashara zao kwani muda huo anakua na hela nyingi za mkopo,pesa zikiisha ndio anakuja kushtuka
 
Back
Top Bottom