Kwanini wafamasia wa maduka ya dawa hawalipi kodi? Serikali iwamulike watu hawa

Puma yetu

Senior Member
Sep 23, 2016
111
125
Kama kuna mahali serikali inapigwa ni hapa, hivi inakuaje hawa wanaoitwa mafamasia wanaojihusisha na shughuli za kutumia vyeti vyao kwenye Mafamasi makubwaa hawalipi kodi!inakuaje mtu analipwa manilioni mengi ya pesa bila kodi? Serikali inalijua hili?

Cha kushangaza ni kwamba wanalipwa pesa nyingi sana kuanzia milioni moja na kuendelea kila mwezi, tena wanataka walipwe kuanzia miezi 3 na kuendelea kwa mkupuo. Kama mfamasia aliyeajiriwa serikalini analipwa mshahara unaokatwa kodi inakuaje kwa malipo ya mfamasia ambaye cheti chake kinatumika famasi alikatwe kodi? Tena inakuaje kwa wengine mtu ni mwajiriwa serikalini halafu anakua na mkataba mwinigine wenye pesa nyingi tuu? Sheria inaruhusu mwajiwa wa serikali kua na mkataba mwingine?
Yeye ni nani hasa?

Hili jambo Pharmacy council wamelufumbia macho makusudi na ndio wanakula dili na hawa watu, inakuaje unamdai mtu mkataba wa ajira kwenye famasi halafu unajua ni mwajiriwa wa serikali? Kama ni hivyo ni kwanini malipo yake bayana makato?

Kinachoshangaza ni kwamba mtu anapotaka kufungua famasi ni lazima apeleke na mkataba wa kumlipa mfamasia huyu ambaye malipo yake hayana kodi.Na wao ndio waliojipangia kulipwa manilioni haya bila utaratibu wowote, hakuna sheria yeyote inayoidhinisha malipo kwa watu hawa utafikiri serikali hailioni hili.

Nimejaribu kufuatilia hawa watu kwa karibu muda mrefu, wanavuna pesa nyingi sana na kugeuza vyeti vyao kua biashara kubwa. Kama mama ntilie tu analipia leseni ya biashara inakuwaje hawa watu wanavuna bila kuichangia serikali? Kama ni suala la kulipia leseni zao za professional hata manesi, maabara na gani zingine wanalupia leseni zao.

Sina wivu na professional ya mtu, lakini linapokuja suala la kulichangia taifa ni lazima tuwajibike wote! Serikali iwe macho na hili, ikiwa tu hata madalali tu wanatakiwa kulipa kodi kwani wasomi hawa wasilipe kodi?
 
Acha roho.mbaya acha roho ya kutu we kijana, ukizeeka wewe lazima uwe mchawi.

Kwani wewe roho inakuuma nini, kasome.na wewe, hivi nyie wafrika mna matatizo gani, ulaya mtu anaajiriwa na kampuni hadi tatu kwa mkataba na kwa kutumia elimu aliyo nayo cha msingi tu aweze kugawa muda wake na boss wake aridhike kazi yake.

Wewe ni masikini wa tumbo hadi akili. Badala uangalie namna ya kujiongezea kipato na wewe unatolea macho liziki za majirani zako. Toa utumbo wako hapa. Umenikera kweli.

Huoni mawakili wanavyoishi?

Ma injinia je?

N.k
 
Ndugu mfamasia ni bora ukamsaidia mleta uzi kwa hoja kuliko kumshambulia , mueleweshe taratibu tu .
 
Mtoa mada jua hata serikali ikiweka kodi, mwenye duka ndio atalipa......... Kiaje?....... Mfano alikuwa analipwa millioni1, akiwa analipa kodi si ataongeza kiasi alicholipia kodi?......... Utakuja tena kulalamika?

Halafu wanasheria/mawakili wakitoza fee za kuendesha kesi hivi wanalipa kodi?.......... Madali hua wanalipa kodi?
Mwalimu akifundisha tuition inabidi alipe kodi?
Ukiwa na daktari wako consultant, let say family medicine........ Kila akija nyumbani kwako kutoa huduma, inabidi alipe kodi?

Hivi mtoa mada kuhusu hayo malipo let say mukakubaliana na mfamasia ukawa unatumia cheti chake bila malipo yeyote kuna tatizo? au hili duka likawa la kwako na mke wako ndio mfamasia kutahitajika malipo yeyote yale kuhusu hiko cheti?

Turudi kwa hao wafamasia.......... Sheria za nchi sinasemaje kuhusu wao kulipa kodi?......... Kwani hiyo hela wanayolipwa kama hakuna kazi wanayoifanya kwa nini walipwe na mwenye duka?, kwa sheria ipi? ..........sheria inalazimisha mfamasia alipwe ama duka ni lazima lisimamiwe na mfamasia? Wenye duka walishawahi kushtaki kwenye mamlaka husika TRA, wizara ya afya kuhusu huo wizi(kama kweli upo).......... Kwa hiyo sababu mfamasia anapata mshahara mkubwa serikalini basi hatakiwi apate pesa nyingine tofauti na mshahara wake?

Mi nadhani hayo malipo ni makubaliano tu kati ya mfamasia na mwenye duka........ Lakini sheria ni lazima duka lisimamiwe na mfamasia.......... Kuhusu litasimamiwaje na mfamasia, sasa hayo ndio makubaliano ya mwenye duka na mfamamasia, kulingana na ukubwa wa duka, uchache ama wingi wa wafamasia......... Kumbuka wafamasia wakiwa 10 na maduk 5 lazima fee iwe ndogo tu(demand and supply theory), mahali duka lilipo etc
 
Huyu jamaa hata Pharmacy Act huijui,unaleta wivu kwa watu na taaluma zao.Niko kwenye usafiri..nitakujibu vizuri nikifika nyumbani.

Cha msingi acha kupotosha umma.
 
Yaani hawa ndo wale wa kusema wengine wanaishi kama malaika bora tuwashushe wote ili tuwe sawa mashetani! Kwendraa nenda kasome uwe nawe mfamasia! Roho ya korosho imekujaa.
 
Kama kuna mahali serikali inapigwa ni hapa, hivi inakuaje hawa wanaoitwa mafamasia wanaojihusisha na shughuli za kutumia vyeti vyao kwenye Mafamasi makubwaa hawalipi kodi!inakuaje mtu analipwa manilioni mengi ya pesa bila kodi? Serikali inalijua hili?

Cha kushangaza ni kwamba wanalipwa pesa nyingi sana kuanzia milioni moja na kuendelea kila mwezi, tena wanataka walipwe kuanzia miezi 3 na kuendelea kwa mkupuo. Kama mfamasia aliyeajiriwa serikalini analipwa mshahara unaokatwa kodi inakuaje kwa malipo ya mfamasia ambaye cheti chake kinatumika famasi alikatwe kodi? Tena inakuaje kwa wengine mtu ni mwajiriwa serikalini halafu anakua na mkataba mwinigine wenye pesa nyingi tuu? Sheria inaruhusu mwajiwa wa serikali kua na mkataba mwingine?
Yeye ni nani hasa?

Hili jambo Pharmacy council wamelufumbia macho makusudi na ndio wanakula dili na hawa watu, inakuaje unamdai mtu mkataba wa ajira kwenye famasi halafu unajua ni mwajiriwa wa serikali? Kama ni hivyo ni kwanini malipo yake bayana makato?

Kinachoshangaza ni kwamba mtu anapotaka kufungua famasi ni lazima apeleke na mkataba wa kumlipa mfamasia huyu ambaye malipo yake hayana kodi.Na wao ndio waliojipangia kulipwa manilioni haya bila utaratibu wowote, hakuna sheria yeyote inayoidhinisha malipo kwa watu hawa utafikiri serikali hailioni hili.

Nimejaribu kufuatilia hawa watu kwa karibu muda mrefu, wanavuna pesa nyingi sana na kugeuza vyeti vyao kua biashara kubwa. Kama mama ntilie tu analipia leseni ya biashara inakuwaje hawa watu wanavuna bila kuichangia serikali? Kama ni suala la kulipia leseni zao za professional hata manesi, maabara na gani zingine wanalupia leseni zao.

Sina wivu na professional ya mtu, lakini linapokuja suala la kulichangia taifa ni lazima tuwajibike wote! Serikali iwe macho na hili, ikiwa tu hata madalali tu wanatakiwa kulipa kodi kwani wasomi hawa wasilipe kodi?
Unawashwa mkuu, au nikuulize unaishikashika ni yako,??? Pembana na Hali yako achana na mambo ya watu
 
Hiyo sheria ya duka kusimamiwa na mfamasia ni uwongo mtupu.Mtu anaweka cheti tu halafu unahudumiwa na mtu asiye hata na mafunzo ya dawa.Ushahidi upo mwingi,wanapaswa kulipa kodi,bodi yao ya wafamasia ndio inawalinda.Maana mikataba yote wanayo na wanajua kuwa kodi hailipwi.Hapa hata TRA ni wa kulaumu Maana hivi ndio vyanzo vya mapato.Ila ni muhimu kuanza na msajili wa wafamasia Maana analea huu ukwepaji na uzembe wa kusimamia famasi.
 
Ni wizi mtupu, bora angekaa hapo full time.
 
Polee sana kijana..!! Itakua kuna mwenzio katusua mfamasia bhasi Karohoo kanakuuma afuu unawashwa washwaa... Babaa kama hukusoma pambana na hali yakoo...
 
Back
Top Bottom