Kwanini wadada wengi wakisaidiwa na kutoka kimaisha wapenzi wao, huwasaliti?

Nna rafik yangu analalamika kila siku, kampiga pind demu wake toka yupo o level, kafaulu na sasa yupo 1st year hapo Ardhi, hamtak tena jamaa, anadai alimkubal kwa kumuonea huruma, jamaa analalamika kwamba huruma yake imezidi

inabidi apige moyo konde! Ingawa si virahisi kusahau maana wanaume ndo 2livyo huwez kusahau ki2 kikubwa kama hicho mpaka kufa! Ila hutakuw unakiwaza sana....... Mwambie rafiki yako ampotezee, Mungu ni mkubwa msaada aliompa hata MUNGU anajua, malipo yatakuja baadae na huyo dada atajuta sana kumwacha rafiki yako na kumwona hafai... Kama ye ni mtu wa dini amsamehe kwa kitendo hicho na AMWACHIE MUNGU SASA AFANYE KAZI YAKE.
 
Mara nyingi nimeshuhudia, akina dada wengi wanasaidiwa hasa kupelekwa shule na wapenzi wao, baadaye huwakataa na kuwaona hawafai, hapa tatizo huwa nini? Nawasilisha

Tabia za wakaka zinakuwa zimewaboa! Kwa hiyo msaada wako ndio uwe kifungo chake? Avumilie mateso, loveless kisa ulimsaidia?

Hujasema na vijana wanaotolewa na kina dada, jinsi wanavyo wanyanyasa wenzi wao.
 
inabidi apige moyo konde! Ingawa si virahisi kusahau maana wanaume ndo 2livyo huwez kusahau ki2 kikubwa kama hicho mpaka kufa! Ila hutakuw unakiwaza sana....... Mwambie rafiki yako ampotezee, Mungu ni mkubwa msaada aliompa hata MUNGU anajua, malipo yatakuja baadae na huyo dada atajuta sana kumwacha rafiki yako na kumwona hafai... Kama ye ni mtu wa dini amsamehe kwa kitendo hicho na AMWACHIE MUNGU SASA AFANYE KAZI YAKE.

asante kwa maneno yako ya kutia moyo, nitampa ayasome mwenyewe, naamini ataelewa
 
Maisha ni maigizo..
maigizo mengine yame
base kwenye True story
mengine ni true story
Na mengine ni ku act tu ...

Ikija kwenye swala lako
moja kati ya hayo maigizo yalitumika..
 
If you have outlived your usefulness in your partner's life, you have no choice except to be dumped..., just like a used condom; it is rather sad, but that is the reality
 
Nna rafik yangu analalamika kila siku, kampiga pind demu wake toka yupo o level, kafaulu na sasa yupo 1st year hapo Ardhi, hamtak tena jamaa, anadai alimkubal kwa kumuonea huruma, jamaa analalamika kwamba huruma yake imezidi
Aliombwa kumsomesha huyo demu?kwani hapati bumu wala hana wa kumsaidia kwao home yani wazazi/walezi?
Tatizo unakuta anaetoa msaada ana dhamira yake fulani wakati anaesomeshwa nae ana nia yake tofauti..Ukisaidia usilalamike unless uliombwa msaada ila kama mwenyewe ulijitutumua basi tegemea lolote.
 
Tatizo ni kwamba akili za wanawake zinakua kila apatapo jipya, mfano ukimtoa kijijini akaja mjini akili itapanuka kiasi atagundua kuwa nilie naye ndiye ananifaa au ndo vile nimbwage? Kama utakuwa na bahati mtaendelea maana si wote huchange.

Tatizo lipo kwenye elimu, mwanamke akivuka stage moja ya elimu hadi nyingine na akili ni vivo hivyo. Mfano mzuri ni binti mwenye elimu ya darasa la saba atakubali kuolewa na muuza kahawa mtaani (si kwa dhararu please) na akaenjoy maisha yake vizuri sana but muuza kahawa huyo huyo akamsomesha binti huyo huyo akifika form four yule binti yale maisha hatayataka tena na ataona ni kero kubwa kwake licha ya kuwa ndiyo yamemsomesha. Akienda chuo ndio kabisaa kapotea na kukukataa atakukataa.

Hao ndio wanawake jamani ukiona anvuka stage jitahidi kukimbizana nae unless una kipato kikubwa saana ndiyo watakukubali vinginevyo forget about her!!!

Wanawake wengi (hasa wa kileo) huwa hawana fikra za kuanza kutafuta kuanzia chini hadi kufikia malengo ya juu kabisa thus why shortcut yao ni kukurupukia wenye vipato tayari.

Ni hayo tu jamani
 
Hata mie haya mambo yananishangaza kwani yamemtokea kaka yangu mara2,kwanza alimpenda binti mmoja toka familia isiyokuwa na uwezo ambae alikuwa form 2,akamsomesha kwa kumgharimia kila kitu mpaka akamaliza chuo kikuu,akamfanyia pati kubwa tu ya kumpongeza na kumvalisha pete ya uchumba na siku hiyo wakalala wote hapa kwangu.Asubuhi yake yule dada akamwambia kaka yangu kuwa hampendi na akamrudishia pete yake na alimwambia kuwa hakumpenda toka mwanzo ila alikuwa anataka amsomeshe tu,kaka akatoka cumbani analia akanielezea nilipomwuliza yule dada akasema ni kweli hampendi.Mara ya 2 akampenda binti mmoja aliyemaliza form 4 ambae wazazi wake walikuwa hawaelewani basi akamsomesha shule ya uandishi mpaka akamaliza diploma,naye alipokaribia kumaliza akamtumia kaka sms ya matusi kuwa hakuwahi kumpenda bali alitaka asomeshwe tu.
 
usiombee yakukute haya mambo, japo ni ukwel kwamba hakupendi lakini inauma tena sana
 
inawezekana mliokuwa mnamsaidia mlikuwa wengi, hivo wakati wa kuolewa lazima achague mmoja,c kama awali wakati wa urafiki,una/ana uwezo wa kuhandle wendi. pole kwa kutopewa kipaumbele. marazote 2kijikwaa tunaangukia mbele,ganga yajayo man,delete the past.
 
Sio mwanamke, siku hizi ukimsaidia mtu yoyote akishatoka hana taimu tena na wewe. Wangapi tuna wasaidia hata ndugu zetu lakini wakishapata hata salamu hawakumbuki? We mkopeshe mtu hela, amalize shida zake, halafu uone! Ukimpigia wala hapokei.
 
Mara nyingi nimeshuhudia, akina dada wengi wanasaidiwa hasa kupelekwa shule na wapenzi wao, baadaye huwakataa na kuwaona hawafai, hapa tatizo huwa nini? Nawasilisha

Kama ndo mimi unanifanyia mambo hayo naenda kukushitaki kwa babu yangu Handeni Tanga then subiri baada ya wiki kitachokupata tusilaumiane.
 
Sio mwanamke, siku hizi ukimsaidia mtu yoyote akishatoka hana taimu tena na wewe. Wangapi tuna wasaidia hata ndugu zetu lakini wakishapata hata salamu hawakumbuki? We mkopeshe mtu hela, amalize shida zake, halafu uone! Ukimpigia wala hapokei.

hilo nalo neno
 
Back
Top Bottom