Kwanini wachungaji, ma shekhe na waganga wa kienyeji hawachezi BIKO na TATUMZUKA

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,343
2,000
Wana Jamvi nina hija ya msingi na maswali ambayo nahitaji wahusika humu na wenye upeo kutujuza wengine. Swala ni kuwa kwanini Wachungaji, Makundi ya maombi, ma Askofu, ma Shekhe na Waganga wa kienyeji hawachezi BIKO na TATUMZUKA? Endapo wapo na wameshashinda sana tu michezo hii sijawahi kuwasikia wakijitambulisha kwa kazi zao kuwa wameshinda, Endapo watatoa sababu kuwa BIKO na TATUMZUKA ni kamari hawawezi kucheza, je hawana uhitaji mkubwa wa fedha ambazo zinazotolewa na Makampuni haya kwa ajili ya familia zao na kuendeleza miradi ya maendeleo katika maeneo wanapofanyia kazi?
Endapo watasema fedha hizo ni haramu niulize ni mara ngapi wanapokea fedha za Zaka, Sadaka na misaada mbali mbali ambazo zinakuwa ni haramu bila ya wao kutambua, wasiseme ni kheri kupokea usicho kitambua au kujua kilipotoka badala ya kupokea unachojua kabisa kilipotoka.
Je, mwenyezi Mungu huwa hawapi ufahamu na roho ya utambuzi kujua fedha zinazoletwa na waumini au wateja ili waweze kuamua kuzipokea au kuzikataa. Endapo watasema wataziombea au kuzitakasa au kuzifanyia lolote lile ili ziwe halali basi ni dhahiri kuwa:
Hata fedha za BIKO na TATUMZUKA baada ya kuzipata wanaweza wakaziombea, kuzitakasa au kuzifanyia lolote ili ziwe halali na hivyo ziwasaidie pamoja na familia, kwa maendeleo ya makanisa, miskiti na majumba yao.
Sasa basi tuseme kwamba makundi haya wanao uwezo wa au upeo au wana karama ya kubashiri namba sahihi kwa ajili ya kushinda BIKO na TATUMZUKA kama wanavyo watabiria watu wao au waumini maono au kuwapigia lamli kwa mambo yao mbali mbali (kwa wanao amini haya).
Je hizi namba za kubashiri za TATUMZU na makampuni mengine ya kubashiri hawawezi kutabiri, kupiga lamli au kufanya lolote lile ili kupata namba sahihi na ya uhakika ili wakicheza tu na washinde au wawasaidie basi waumini na wateja wao ili wapate fedha hizi.
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
22,055
2,000
Picha alijaisha mkuu subiri mwakani magu kasema itakua zaidi ya hapa so kila mtu atacheza hadi wanaochezesha nao watacheza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom