MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Huhitaji kufanya uchunguzi wa kina kugundua kama wapinzani nchini hawajajipanga
Ukiangalia utagundua wabunge wote wa upinzani wa kuchaguliwa ambao wana uzoefu bungeni hawajakutana na "panga" la kuwaengua kwa sababu kuu moja ambayo ni kujua vizuri taratibu za mchakato wa kuchukua fomu, kujaza kwa usahihi na kurudisha kwa wakati unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Uchaguzi.
Baadhi ya Wabunge waliokuwa wa viti maalum pia wameenguliwa kwa sababu nao hawana uzoefu katika mchakato kutokana na kuwa hawakuwahi kujaza fomu za kugombea ubunge bali walipewa ubunge kupitia vyama vyao.
Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao.
Wapinzani wataendelea kulalamika wakati tatizo na ufumbuzi wa tatizo uko ndani ya uwezo wao kama watajipanga vizuri.
Wapinzani kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii wakati masuala ya muhimu kwenye "ground zero" hawayafanyi kwa umakini.
Uchaguzi Mkuu ni mchakato na sio tukio.
Ikumbukwe kuwa Sheria hazina Siasa.
Kilichobaki kwa sasa ni kuhesabu maumivu!