Uchaguzi 2020 Kwanini Wabunge wazoefu wa Upinzani hawajaenguliwa?

Huhitaji kufanya uchunguzi wa kina kugundua kama wapinzani nchini hawajajipanga

Ukiangalia utagundua wabunge wote wa upinzani wa kuchaguliwa ambao wana uzoefu bungeni hawajakutana na "panga" la kuwaengua kwa sababu kuu moja ambayo ni kujua vizuri taratibu za mchakato wa kuchukua fomu, kujaza kwa usahihi na kurudisha kwa wakati unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Uchaguzi.

Baadhi ya Wabunge waliokuwa wa viti maalum pia wameenguliwa kwa sababu nao hawana uzoefu katika mchakato kutokana na kuwa hawakuwahi kujaza fomu za kugombea ubunge bali walipewa ubunge kupitia vyama vyao.

Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao.

Wapinzani wataendelea kulalamika wakati tatizo na ufumbuzi wa tatizo uko ndani ya uwezo wao kama watajipanga vizuri.

Wapinzani kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii wakati masuala ya muhimu kwenye "ground zero" hawayafanyi kwa umakini.

Uchaguzi Mkuu ni mchakato na sio tukio.

Ikumbukwe kuwa Sheria hazina Siasa.

Kilichobaki kwa sasa ni kuhesabu maumivu!

Kwamba ndo tumeanza jaza fomu mwaka huu mbna awamu zilizopita hawakukatwa
 
CCM ilisambaza wanasheria nchi nzima kuwasaidia kujaza fomu .Upinzani kila mtu alikuwa akipambana kivyake

Kwa hiyo mlisaidia madiwani wenu na wabunge ila mkuu wenu mkashindwa mjazia fomu🤔 mbona yeye aliboronga pia
 
Maccm majitu ya ajabu kweli unakuta jitu Kama Nape ,Mwigulu yanaogopa ushindani kwenye sanduku la kura , Mwigulu anahangaika kumwengua Jesca Kishoa aibu kweli haya majitu
Screenshot_20200828-204023.png
 
CCM ilisambaza wanasheria nchi nzima kuwasaidia kujaza fomu .Upinzani kila mtu alikuwa akipambana kivyake
Unachokisema kwa kiasi Fulani ni sahihi,kuna waliofanya makosa ya kijinga,nadhani pia chama hakikuwa serious na swala hili ingawa kuna wengine" wamehujumiwa" kwa namna moja au nyingine.
 
Kwani wageni ni wapinzani peke yao, hakuna ccm mgeni uchaguzi huu?!

Mbona hawajaenguliwa ccm hata mmoja?!

CCM hawajaenguliwa kwa sababu wakati wa kujaza fomu wanasheria wao(wanasheria wa CCM) wanawaongoza. Period.
 
Kwani Kati ya Mgombea urais wa ccm na chadema ni Nan alie kosea mashart ya form ikapelekea mpaka kutoka ukumbin usiku????
Kama mwanasheria namba moja wa uchaguz Tanzania ameshindwa kujaza vip Hao wengine
 
Hicho ndicho,ninachoshangaa, wala hawajasumbuliwa kama wengine. Kidogo prof.J walimsumbua. Lakini wapya wamesumbuliwa sana. Nadhani labda CCM walikuwa wanawakomaza kwanza
 
Back
Top Bottom