Uchaguzi 2020 Kwanini Wabunge wazoefu wa Upinzani hawajaenguliwa?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,265
2,000
Huhitaji kufanya uchunguzi wa kina kugundua kama wapinzani nchini hawajajipanga

Ukiangalia utagundua wabunge wote wa upinzani wa kuchaguliwa ambao wana uzoefu bungeni hawajakutana na "panga" la kuwaengua kwa sababu kuu moja ambayo ni kujua vizuri taratibu za mchakato wa kuchukua fomu, kujaza kwa usahihi na kurudisha kwa wakati unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Uchaguzi.

Baadhi ya Wabunge waliokuwa wa viti maalum pia wameenguliwa kwa sababu nao hawana uzoefu katika mchakato kutokana na kuwa hawakuwahi kujaza fomu za kugombea ubunge bali walipewa ubunge kupitia vyama vyao.

Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao.

Wapinzani wataendelea kulalamika wakati tatizo na ufumbuzi wa tatizo uko ndani ya uwezo wao kama watajipanga vizuri.

Wapinzani kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii wakati masuala ya muhimu kwenye "ground zero" hawayafanyi kwa umakini.

Uchaguzi Mkuu ni mchakato na sio tukio.

Ikumbukwe kuwa Sheria hazina Siasa.

Kilichobaki kwa sasa ni kuhesabu maumivu!
 

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,345
2,000
Umejuaje kama wa upinzani hawasimamiwi na wanasheria wao. Babutale nae anauzoefu wa kujaza fomu yule darasa la nne? acha kuropoka wewe.shida yenu kuwachokoza watu nakuanzisha machafuko yasiyokuwa na msingi..Mwaka huu mbona watawanyoosha.
 

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,666
2,000
Anayewadanganya kuwa huu uchaguzi mtaenda nao katika uhuni huu mnaoonyesha mwambieni akaje upya. Nasema mwambieni akaje upya. Endeleeni na utoto wenu huo huo! Sisi kwa sasa tumeinamisha vichwa chini kama kobe. Muda ukifika tutavinyanyua
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,765
2,000
Unajaribu kusema nini hasa?!

Hivi huko kutojipanga na kutojua huku kwenye kila uchaguzi kupo kwa watu wa upinzani peke yake?!

Yaani ma-CCM haya haya, tunayoishi nayo kwenye mitaa ile ile, tukiwa tumesoma kwenye shule zile zile tukila ugali na wali ule ule, walimu wetu ni wale wale, hospitali tunazotibiwa ni zile zile lakini linapokuja suala la uchaguzi, Wagombea WOOOOOOOOOOTE wa CCM wanageuka kuwa ndio wenye akili peke yao huku wale wa upinzani wakionekana ndio wasiojua?!
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,844
2,000
Kwani wageni ni wapinzani peke yao, hakuna ccm mgeni uchaguzi huu?!

Mbona hawajaenguliwa ccm hata mmoja?!
CCM ilisambaza wanasheria nchi nzima kuwasaidia kujaza fomu .Upinzani kila mtu alikuwa akipambana kivyake
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,265
2,000
Umejuaje kama wa upinzani hawasimamiwi na wanasheria wao. Babutale nae anauzoefu wa kujaza fomu yule darasa la nne? acha kuropoka wewe.shida yenu kuwachokoza watu nakuanzisha machafuko yasiyokuwa na msingi..Mwaka huu mbona watawanyoosha.
Hoja yako imejibiwa ndani ya mada na paragraph hii;
"Tofauti ya wagombea wa upinzani na CCM ni kuwa wagombea wa CCM wanasimamiwa na wanasheria wa chama chao katika kujaza fomu kwa usahihi wakati wale wa upinzani wanajaza peke yao."
 

gTurn

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
347
250
CCM ilisambaza wanasheria nchi nzima kuwasaidia kujaza fomu .Upinzani kila mtu alikuwa akipambana kivyake
acha uhuni ile fom ni ya kiswahili hata mtoti wa darasa la 3 akiamshwa saa 8 usiku anajaza ...narudia ile fom ni uhuni tuu wa ccm na vibaraka wao
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,265
2,000
Anayewadanganya kuwa huu uchaguzi mtaenda nao katika uhuni huu mnaoonyesha mwambieni akaje upya. Nasema mwambieni akaje upya. Endeleeni na utoto wenu huo huo! Sisi kwa sasa tumeinamisha vichwa chini kama kobe. Muda ukifika tutavinyanyua
Nyie inamisheni tu huku mkijua Sheria hazina siasa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom