Kwanini wabunge wanaichambua hotuba ya Mbowe na hawaigusi kabisa ile ya Zitto kuhusu CAG?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,889
2,000
Ikumbukwe kuwa Zitto Kabwe na Freeman Mbowe walitoa hotuba zao siku moja ila walipishana masaa tu.

Zitto Kabwe alijikita kwenye ripoti ya CAG na akaelezea ubadhirifu katika maeneo kadhaa ikiwemo ATCL.

Freeman Mbowe yeye alijikita kuuelezea utawala wa awamu ya tano ulivyohitimika na kuanza kwa utawala mpya wa awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan

Wabunge wengi akiwemo Spika Ndugai wameonekana kuvutiwa zaidi na hotuba ya Mbowe na hakuna anayemzungumzia Zitto Kabwe kabisa.

Najiuliza kwanini?

Ramadhan Kareem!
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,459
2,000
Mimi nafikiri ni kwa sababu hotuba ya C'de. Mbowe ilibeba maudhui mapana juu ya mustakabali wa taifa ilhali hotuba ya C'de ZZK ilijikita tu kwenye mapungufu katika usimamizi wa fedha za umma. Nahisi hivyo!!!
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
7,121
2,000
Mkono mtupu haulambwi, zitto mwenyewe hata hakumbuki alisema nini kwenye ile hotuba yake
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,079
2,000
... tukio kubwa na la kipekee kuwahi kutokea Tanzania ni kifo cha aliyekuwa rais wa awamu ya tano; tukio ambalo kila mtanzania amelichukulia kwa hisia tofauti kutokana na aina ya utawala wa mhusika. Baadhi wanataka "asitiriwe" huku wengine wakitaka "aachwe hivyo hivyo" mjadala ni mzito! Kwa kuwa Mbowe alijikita kwenye eneo hilo, obviously, hotuba yake ita-hit zaidi.
 
Immanuel Simon Mathew

JF-Expert Member
Apr 2, 2020
462
1,000
Hotuba ya Hon.Mbowe ilikuwa imejaa ukweli ambao ni mchungu sana kwa Mataga ndiyo maana wanapambana kuneutralize makali ya ule ukweli ila Message sent and delivered!!
 
SMART GHOST

JF-Expert Member
Feb 3, 2020
299
1,000
Hotuba ya Mbowe iko na hoja nzito, ila zinajadilika hata kwa watu aina ya Kibajaji. Hoja za Zitto Kabwe ni nzito pia, na zinahitaji uelewa mpana wa masuala ya kiuchumi kuzijadili. Ndio maana humsikii Musukuma akiongelea hotuba ya Zitto. Hakuna alichoelewa!
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,756
2,000
Ikumbukwe kuwa Zitto Kabwe na Freeman Mbowe walitoa hotuba zao siku moja ila walipishana masaa tu.

Zitto Kabwe alijikita kwenye ripoti ya CAG na akaelezea ubadhirifu katika maeneo kadhaa ikiwemo ATCL.

Freeman Mbowe yeye alijikita kuuelezea utawala wa awamu ya tano ulivyohitimika na kuanza kwa utawala mpya wa awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan

Wabunge wengi akiwemo Spika Ndugai wameonekana kuvutiwa zaidi na hotuba ya Mbowe na hakuna anayemzungumzia Zitto Kabwe kabisa.

Najiuliza kwanini?

Ramadhan Kare
Wachambue nini wakati Zitto ni CCM? Yumo kitanda kimoja nao Zanzibar. Hivyo, hana tishio lolote kwao wala jipya. Ni sawa na Mrema, Cheyo, Lipumba na wasakatonge wengine.
 
Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
343
1,000
Wachambue nini wakati Zitto ni CCM? Yumo kitanda kimoja nao Zanzibar. Hivyo, hana tishio lolote kwao wala jipya. Ni sawa na Mrema, Cheyo, Lipumba na wasakatonge wengine.
Hivi ww na akili zako unaamini huyu ndo mpinzani wa kweli? Alichokifanya 2015, kuchukua wagombea wa CCM kuja kuwapa nafasi ya kugombea Chadema katika nafasi ya uraisi na ubunge unafikiri lilikuwa swala la bahati mbaya? Hao wote wachumia tumbo, na wapo upinzani kwa masilahi na mikakati maalum

images (3).jpeg
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,756
2,000
Hivi ww na akili zako unaamini huyu ndo mpinzani wa kweli? Alichokifanya 2015, kuchukua wagombea wa CCM kuja kuwapa nafasi ya kugombea Chadema katika nafasi ya uraisi na ubunge unafikiri lilikuwa swala la bahati mbaya? Hao wote wachumia tumbo, na wapo upinzani kwa masilahi na mikakati maalum

View attachment 1753745
Naye ni CCM ila mwenye kuhitaji kupewa kitu mara kwa mara tofauti na wenzake. Kwa ufupi Tanzania hakuna wapinzani. Kama wapo basi wapo humu Jf.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom