Kwanini Wabunge wa CHADEMA hawawaaliki viongozi wenzao na Wananchi Bungeni?

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, amani iwe kwenu.

Imekuwa ni kawaida kwa wabunge hususan wa chama tawala, CCM kuwaalika viongozi mbalimbali waliopo kwenye majimbo yao kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabunge hao wa CCM huonesha hisani kwa viongozi wenzao na wananchi ambao ni wapiga kura wao kwa kuwagharamia usafiri wa kwenda na kurudi Dodoma, chakula na malazi. Hali hiyo imekuwa ikiwapa fursa viongozi ambao si wabunge kuweza kutembelea bunge hilo na hivyo kuweza kupanua fikra zao juu ya bunge hilo. Viongozi ambao mara kwa mara wamekuwa wakialikwa na wabunge wa CCM ni wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, madiwani, Maafisa Watendaji wa kata na kijiji, viongozi wa CCM ngazi ya wilaya, kata na kijiji, wawakilishi wa asasi za kiraia, mashirika ya kidini, wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi, watumishi wa serikali wa kada mbalimbali Pia wananchi wa kawaida wamepata fursa ya kutembelea bunge hilo. Hali hiyo inaonesha kuwa wabunge hao wanaishi vizuri na viongozi wenzao na wananchi. Pia kitendo hicho cha wabunge hao kimewapa fursa ya kupongezwa hasa na Spika na Naibu Spika kuwa wanafanya kazi nzuri bungeni na hivyo watu hao wanaoalikwa kuoeleka message nzuri kwenye majimbo yao. Nakumbuka kuna siku Mchungaji Msigwa alilalamika kuwa eti Naibu Spika anawapendelea wabunge wa CCM kwa kuwapa sifa tele anapotambulisha wageni wao. Sasa wewe Msigwa na wabunge wenzako mnapolia lia kutaka kupongezwa ilhali hamfanyi vizuri na wala hamuwaaliki wapiga kura wenu mna haki ya kudai hivyo?

Hali hiyo imekuwa tofauti kabisa kwa wabunge wa CHADEMA. Sijui ni ubahiri, uchoyo au kutokuwa na mafungamano mazuri na viongozi wenzao na wananchi? Sijapatapo kusikia hawa wabunge wa CHADEMA wakialika viongozi hata wa chama chao kutoka kwenye majimbo yao. Hii ni aibu kubwa sana na ni dhahiri kuwa hawa wabunge waliingia bungeni kwa malengo yao tu. kuna siku nilicheka sana. Eti John Mnyika, Mbunge wa Ubungo aliwaalika wanachama wa CHADEMA kutoka UDOM. Hii ni aibu kubwa sana kwani hao wanachama wa UDOM hawawezi kumsaidia kwenye harakati zake za kutetea jimbo lake. Angekuwa mwerevu kama angewaalika wanafunzi wa UDSM ambao wapo kwenye jimbo lake na ambao walimsaidia kushinda uchaguzi wa 2010. Ila jamaa kapiga hesabu weeeee akaona kuwa kuwagharamia wale wa UDOM inakuwa rahisi sana kuliko wa UDSM.

Kubwa kuliko wote ni huyu kiongozi wa Kambi ya Upinzani (KUB), Freeman Mbowe. Kwa level yake huyu, anastahili hata kuwaalika wapinzani wenzake kutoka nchi nyingine kuja kutembelea bunge la Tanzania. Pia kwa nafasi yake, anaweza kuwaalika japo viongozi wa chama kutoka mikoa yote. Hii ingemsaidia sana kujenga mshikamano wa kichama. Uzoefu uliopo ni kuwa pale wabunge wa CCM wanapoalika watu na viongozi kutoka majimbo yao, wanatumia nafasi hiyo hasa wakati wa dinner, kuelezana changamoto zilizopo kwenye majimbo yao na kupanga mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto hizo. Na hii ndiyo imekuwa siri kubwa ya mafanikio ya wabunge wengi wa CCM. Mbowe amekuwa mbinafsi sana. Mbowe yupo tayari kutumia fedha zake kufanya ziara zisizo rasmi huko Dubai, Kenya na Rwanda lakini si kuwaweka pamoja viongozi wenzake. Yaani nikimtathmini Mbowe hakika nashindwa kummaliza. Pia sielewi hata kidogo malengo yake kisiasa ni yepi.

Mwisho niwapongeze wabunge wote wa CCM kwa kuhamasisha mshikamano ndani ya majimbo yao na niwahurumie wabunge wa upinzani na hasa CHADEMA kwa kukosa ubunifu. Sitarajii kuna msukule wa CHADEMA atakuja hapa kunishambulia. Ni ushauri tu nautoa kwenu kuwa unapokuwa mbunge maana yake ni kuwa una dhamana kubwa sana na unapaswa kushirikiana vema na viongozi wenzako ndani ya jimbo lako na wananchi kwa ujumla.
 
Huwezi ukaalika wageni na viongozi wengine wa chama, waje kushuhudia ukishindwa kushindana kwa hoja na hatimaye ukaamua kupigana, kuzomea, kususa, kutumia kejeli na kuropoka ropoka tu. Wenye uwezo wa kualika wageni wana sifa za kuwa wenyeji kwa wageni wao na sifa hizo zinaanzia kwenye tabia nzuri na uwezo wa kujenga hoja na kuzisimamia.
 
Huwezi ukaalika wageni na viongozi wengine wa chama, waje kushuhudia ukishindwa kushindana kwa hoja na hatimaye ukaamua kupigana, kuzomea, kususa, kutumia kejeli na kuropoka ropoka tu. Wenye uwezo wa kualika wageni wana sifa za kuwa wenyeji kwa wageni wao na sifa hizo zinaanzia kwenye tabia nzuri na uwezo wa kujenga hoja na kuzisimamia.
Kweli mkuu hawa watu wanahofu aibu kwa matusi na fujo wanazofanya bungeni.
 
Nini umuhimu wa kutembelea bungeni zaidi ya kuuza sura? Badala ya kufanya kazi unataka hisani za kwenda kuuza sura kupitia TBC? Ama kweli ukiwa MwanaCCM wa zama hizi lazima tumbo lishikilie akili.......:frusty:
 
ccm ni chama cha wahuni na washenzi wakubwa hawana akili sisi wananchi tunataka maendeleo siyo porojo cha wanafiki ccm
 
Wanajua bungeni hawana wanachoongea zaidi ya matusi ndiyo maana hawaaliki kwa kuhofia aibu.
Au inaelekea wanawaalika lakini waalikwa wanakataa kutokana na matusi wanayoporomosha waalika?
 
moja kati ya upuuzi wa wabunge ni kualika wageni wao kwenda bungeni!hiyo hela wangefanyia mambo mengine ya maendeleo,narudia kusema ni upuuzi.
 
Nini umuhimu wa kutembelea bungeni zaidi ya kuuza sura? Badala ya kufanya kazi unataka hisani za kwenda kuuza sura kupitia TBC? Ama kweli ukiwa MwanaCCM wa zama hizi lazima tumbo lishikilie akili.......:frusty:
Mbona chadema kuuza sura ndiyo kipau mbele kwao,hawa huuza sura mpaka misibani na kwenye majengo yaliyoanguka.
 
moja kati ya upuuzi wa wabunge ni kualika wageni wao kwenda bungeni!hiyo hela wangefanyia mambo mengine ya maendeleo,narudia kusema ni upuuzi.
Nikuulize Mkuu, hivi fedha wanazopata akina Lema, Sugu, Msigwa na Mnyika zinafanya nini kwenye majimbo yao? Ina maana hujui maana nzima ya dhana ya kualika watu bungeni?
 
Mtu kama Mnyika licha ya fedha nyingi anazopata zikiwemo zile anazopewa na Mbowe kwa sababu zinazojulikana lakini wapiiii! Sijui anazitumia kwa kazi gani
 
Back
Top Bottom