Kwanini wabunge wa CCM wanatumia hoja za wapinzani walizotoa Bunge lililopita? Hakuna hoja mpya?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kwanini hoja zilezile zilizotolewa kwenye bunge Mwaka 2015-2020 ndizo zinazoibuliwa leo na wabunge wa CCM wakati kipindi zinatolewa walizipinga?
Hoja ya kutumia taskforce kukusanya kodi iliezwa vyema bunge lililopita na wabunge wa CCM na uongozi wa Bunge pamoja na Mawazir waliipinga vikali.

Hoja ya biashara kufa ilijadiliwa sana tunaambiwa hakuna biashara inayofungwa, wanaofunga ni mafisadi.

Hoja ya ubovu wa mfumo wa elimu Mbatia ameimba for years akipingwa na Wana ccm, je leo imegeukaje kuwa agenda yao?

Viwanda navyo waliambiwa wanafanya siasa kipindi kile Cha Mwijage na Tanzania ya viwanda, lakina ilikataliwa na kuonekana kama watoa hoja wanapinga kila kitu, Leo viwanda vipo wapi?

Kilimo ndo kabisa taadhari ilitolewa kuanzia mbaazi, korosho, kahawa, mahindi nk tulifunga masikio tusisikie ila Leo imegeuka agenda...

Hoja hizi na nyingine nyingi zingezingatiwa na kupatiwa ufumbuzi hali isingekuwa kama ilivyo Sasa. Wanatojitokeza kushauri Sasa baada ya awali kukosea kuishauri serikali wana kila sifa ya uhujumu uchumi.

Lini tutaamua kuweka maslahi mapana ya Taifa mbele? Lini tutaanza kuwazungumzia wananchi? Tuchutame
 
Wabunge wengi wa ccm hawana uwezo wa kujenga hoja.

Hata juzi spika wao Ndugaye aliwashangaa kuwa wapiga makofi na vigeregere badala ya kuibua hoja mbali mbali za kimaendeleo.
 
CCM ni kama kenge. Hadi wapigwe masikio yatoke damu ndiyo wanaelewa.
 
Kipindi kile ni walitega misumari barabarani kwa jirani wakiamini itadhuru gari lake wakasahau kuna siku watapita njia iendayo kwa jirani! Bakora za 5 tena ni kali Jiwe shikilia hapo hapo!
 
Back
Top Bottom