Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,580
Hii si mara ya kwanza kwa wabunge wa CCM kubakia bungeni wakati wabunge wa vyama vingine wanapotoka nje ya ukumbi vinapofanyika vikao vya bunge kupinga jambo fulani. Kubaki kwao na kuendelea na vikao vya bunge huwa kuna ujumbe fulani tunatakiwa tuupate sisi wananchi tuliowachagua.
Kwa mfano wakati UKAWA walipotoka bungeni kupinga kubadilishwa kwa mfumo wa serikali uliokuwa kwenye Rasmu ya Katiba iliyowasilishwa Bungeni na Tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya wabunge wa CCM walibakia bungeni na kuendelea na vikao vyao.
Lakini likatokea tatizo la kufikia akidi ya kura toka Zanzibar, hapo tukaona kila aina ya sarakasi ili kukidhi haja ya waliobakia kikaoni. Na mojawapo ya sarakasi hizo ni lile la kusema kuwa wajumbe waliokuwa Hajji nao pia walipiga kura!! Swali la kujiuliza kama wao walijua kuwa ni lazima hoja zao zipitishwe ije mvua lije jua ni kwa nini walipoteza muda na fedha za wananchi kujifanya wanafanya majadiliano ilhali walikuwa wamebaki wenyewe?
Hivi sasa iko hoja ya Wabunge wa upinzani kukataa kuongozwa na Tulia Akson kama Naibu spika wa bunge hilo. Kila siku tunaona wabunge wa upinzani wakitoka na wa CCM wakibakia bungeni. Lakini wanabaki wakifanya nini?
Kitu gani cha maana wanachofanya wabunge wa CCM hadi kuhalalisha kubaki kwao bungeni?