SoC01 Kwanini Wabunge hushangaa bajeti na sheria za ajabu walizopitisha wao wenyewe Bungeni?

Stories of Change - 2021 Competition

cilla

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
369
296
Moja ya sababu inayofanya wabunge kushangaa sheria au bajeti walizopitisha wao wenyewe ni kwasababu ubunge haujakaa kama taasisi.

Ibara 67 ya katiba ya Tanzania inaeleza sifa za mbunge ni kujua kusoma na kuandika.Na ibara ya 63 na 64, kazi ya mbunge ni kushiriki kwenye kutunga sheria na kusimamia na kushauri serikali yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Na katiba hiyo hiyo inaeleza maana ya serikali kuwa ni taasisi ya juu katika nchi .

Serikali ambayo ni taasisi ni kitu kikubwa sana kilichosheheni wabobezi ,wataalam, na wasomi mbalimbali katika nyanja zote uchumi, elimu, biashara, sheria, uongozi ,teknolojia nk.

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi katika bunge ambalo linashughulikia masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi wa Tanzania. Mbunge kama mtu tunategemea akawakilishe wananchi katika maeneo mbalimbali kama elimu, sheria, afya, uchumi na usalama.Si ajabu kwamba sio rahisi mbunge kama mtu kuwa na umahiri katika maeneo hayo yote. Tena kwa mujibu wa katiba yetu mbunge anaweza akawa na elimu ya darasa la saba jambo ambalo linaweza kukwamisha uwakilishi wenye tija katika maeneo yanayohitaji umahiri na utaalamu.

Hii inamaana gani? Hii ina maana kuwa ubunge kwa mujibu wa katiba yetu ni vigumu kuwa na uwakilishi wenye tija sana kwasababu ubunge kwetu sio taasisi ni ofisi ya mtu.Changamoto ya mbunge kama mtu ni kwamba hawezi kuwa mahiri katika maeneo yote ya uwakilishi, anapougua muda mrefu jimbo lake linakosa uwakilishi, katika maeneo yanahitaji umahiri kama sheria ni vigumu mbunge kuwa na mchango wenye tija hasa inapokuwa sio taalamu yake.

Serikali kama Taasisi inapopeleka hoja au mswada bungeni yenyewe kama taasisi inakuwa imeshirikisha wataalamu wake katika nyanja husika.Mswada au hoja inapotinga bungeni hujadiliwa na kupitishwa na wabunge ambao kwa sehemu huwa si mahiri katika maeneo husika yanayopaswa kujadiliwa.Mfano mswada wa sheria unapokuja bungeni na mbunge wako ni mtaalamu wa kilimo unafikiri mchango wake unaweza kuwa na tija?Bila shaka anaweza kuchangia kwa sehemu ndogo sana kutokana na uelewa wake katika mambo ya sheria.Na hata wakiwepo wenye taaluma ya sheria wawili au watatu bado wanaweza wasiwe na ushawishi kwa wabunge wengine au uwezo wao katika masuala ya sheria ukawa uko chini.

Uwepo wa kamati za bunge zinaweza kuwa na msaada kwa sehemu ndogo kwasababu kamati zinatokana na wambunge na wabunge hawachaguliwi kwa taaluma zao kwahiyo kunauwezekano baadhi ya kamati zikawa na mtu mmoja au hakuna kabisa mwenye umahiri au utaalamu katika kamati husika.

Kama nchi tunahitaji kuwa na Mbunge kama mtu lakini ni taasisi inayomuwezesha na kumjengea uwezo katika kuwakilisha wananchi wake vizuri katika masuala mbalimbali.Uwepo wa ubunge kama taasisi itasaidia Mbunge kuajiri washauri mbalimbali ambao watamsaidia katika kuchambua masuala mbalimbali katika jimbo lakini pia katika nchi.uwepo wa taasisi kutasaidia Mbunge kufanya tafiti mbalimbali, kutafsiri takwimu mbalimbali, kusimamia miradi katika jimbo lakini pia itasaidia kushughulikia na kupokea maoni na kero mbalimbali za wananchi hata kama mbunge hayupo jimboni.pia hii itamsaidia mbunge anapokuwa anaumwa na hawezi kuchangia mijadala mbalimbali basi taasisi ya mbunge itapokea miswada na kuchakata na kutoa maoni kwa niaba ya mbunge na kuuliza maswali kwa niaba ya mbunge pia.

Mbunge ana siku chache za kukaa jimboni na kushughulika na maendeleo ya jimbo lake ukilinganisha na siku anazokuwa katika mikutano ya bunge na kamati zake. Pia wabunge hawapati muda wakutosha wakuchakata hoja mbalimbali zinazoletwa bungeni kutokana na shughuli nyingi za kibunge .Mbaya zaidi mbunge anapokuwa waziri ubize huongezeka na hivyo kushindwa kufanya uwakilishi wake vizuri.Njia pekee yamfanya mbunge awe na tija katika uwakilishi na kuihoji serikali ni kuifanya ofisi ya mbunge kama taasisi kwa maana ya kuwezeshwa kuwana vitendea kazi muhimu pamoja na wataalamu mbalimbali kwaajili ya kumshauri mbunge, kumwakilisha, kufanya tafiti kama ilivyo katika wizara zetu ambazo Waziri anaweza kuwa na taaluma ya umeme lakini akawa waziri wa afya na akafanya kazi zake vizuri kwasababu ana watu chini yake katika wizara wenye taaluma husika wanaomshauri .

Serikali kama taasisi inahitaji mbunge kama taasisi ndogo iliyokamilika katika nyanja zote. Tukiweza kumfanya mbunge kuwa na vitendea kazi kama taasisi basi uwakilishi wetu wananchi utakuwa na nguvu katika bunge.
 
Mbunge ni mjumbe wa baraza la madiwani linalounda Halmashauri, unaposema ubunge uwe taasisi na uwe na watalaam mbalimbali wa kumshauri unamanisha nini?

Halmashauri ni taasisi iliyosheheni watalaamu mbalimbali, kwa hiyo mbunge amezungukwa na watalaam wote kwa mjibu wa mtizamo wako.
 
Mbunge ni mjumbe wa baraza la madiwani linalounda Halmashauri, unaposema ubunge uwe taasisi na uwe na watalaam mbalimbali wa kumshauri unamanisha nini?

Halmashauri ni taasisi iliyosheheni watalaamu mbalimbali, kwa hiyo mbunge amezungukwa na watalaam wote kwa mjibu wa mtizamo wako.
baraza la madiwani linawajibika kwa mbunge? wataalamu wa halmashauri si wataalamu wanaowajibika kwa mbunge. Nilicho maanisha hapa ni kwamba mbunge anapaswa kuwa na wataalamu kwenye ofisi yake ambao watawajibika kwake na watakuwa na kazi ya kuchambua hoja na miswada kwa niaba ya mbunge ,Mbunge anaweza asiwe mtaalamu au msomi wa masuala ya kiuchumi au sheria lakini akiwa na watu wenye taaluma hizo ni rahisi kumsaidia mbunge kuchambua ,kufanya tafiti, na kumpa mwanga mbunge juu ya kile anachoenda kuwakilisha bungeni. Mbunge anapokuwa mgonjwa au hayupo jimboni hawa watu pia watahusika kufuatilia miradi na kupokea maoni ya wananchi na kuyawakilisha bungeni kwa njia ya maandishi tofauti na sasa mbunge akiumwa miaka 5 na uwakilishi wake bungeni unakuwa umekufa pia. Jambo nililozungumza hapa sio geni kuna nchi zinafanya hivyo kwa kuwa na mbunge taasisi kwa maana kuwa anakuwa na watu wanaomsaidia kuchambua na kufanya tafiti mbalimbali kwa niaba ya mbunge.
 
Tufike sehemu posho na mishahara yao ikatwe kodi ili wa-feel kama sisi

wakatwe
Payee
NHIF
 
Back
Top Bottom