Kwanini Wabunge hawavai barakoa wakiwa Bungeni?

Fatma-Zehra

Senior Member
Oct 18, 2020
192
1,062
Bunge limeanza asubuhi hii, hakuna mwenye barakoa. Je, wanamdharau Rais Samia au wanaiona barakoa kama sanaa?
 
Mdharau mwiba mguu huwota tende,wacha wasivae uwone watakavyopukutika, india sasa hakuna hata kuni za kuchomana wanafanya mass grevu
 
Mdharau mwiba mguu huwota tende,wacha wasivae uwone watakavyopukutika, india sasa hakuna hata kuni za kuchomana wanafanya mass grevu
Nyie mnajua kuvaa barakoa tu wala hamjui matumizi sahihi ya barakoa kitu ambacho kinaweza kuwa sababu kubwa ya maambukizi.
 
Mbona Zezeta lao lilikataa kunywa uji pale Mzena
Nasema hivi kama watapukutika kwa kutovaa barakoa basi wangekuwa washaisha wabunge wote mule na sio wabunge tu hata huyo Mama Samia tungekuwa tushamzika siku nyingi kama Maalim seifu, maana hizo barakoa toka aanze kuvaa hata mwezi haufiki.
 
Bunge la wabunge walioingizwa bungeni kwa jitihada za mwendazake bila kuchaguliwa na wananchi hivyo lazima wamuenzi boss wao.
 
Bunge la wabunge walioingizwa bungeni kwa jitihada za mwendazake bila kuchaguliwa na wananchi hivyo lazima wamuenzi boss wao.
Sijui kwanini watu mnapenda kumuhusisha Jiwe, nakumbuka kipindi kile cha level seat watu walikuwa wanapanda na kujificha chini wasionekane na traffic na wengi hawakuwa na barakoa, huku mtaani hakukuwa na tofauti yeyote watu walijiachia tu kama kawaida mpaka wengine hawakuona maana ya kufunga shule maana hao wanafunzi huku mtaani walijiachia tu na mimba zikapatikana za kutosha. Sasa watu wa aina hiyo ndio inakuwaje apewe lawama Magufuli kuonekana ndio kawafanya wawe hivyo?
 
Nasema hivi kama watapukutika kwa kutovaa barakoa basi wangekuwa washaisha wabunge wote mule na sio wabunge tu hata huyo Mama Samia tungekuwa tushamzika siku nyingi kama Maalim seifu, maana hizo barakoa toka aanze kuvaa hata mwezi haufiki.
Ninyi na utaalamu wenu wa kujifukiza Mizizi na Viungo Vya pilau na Mbinu zenu za Kichawi mlizokuwa mkipromoti Tume ya Covid imemwambia Mama kuwa hazifai

Ubishi na Ujinga wenu umesababisha Wazee wetu wafe kwa wingi mimi mwenyewe nimepoteza karibu 12 ndani ya muda mfupi
 
Mkuu kuhusu vifo sidhani kama tumefikia nchi za wenzetu huko ambako tulisikia hadi sehemu za kuhifadhi maiti zilijaa na hao hawakuwa wakifanya ujinga kama sisi, sasa sijajua huo wingi unaousema ni wingi wa kiasi gani uliyosababishwa na ujinga wetu na ambao haujawafikia wingi usiosababishwa na ujinga maana wao walikuwa wakitumia sayansi?

Tume haijatuambia tumeathirika vp kwa kipindi chote hiki tulichofanya ujinga zaidi tu imependekeza tufuate mfumo mwengine waliyoutumia wenzetu wakati sisi tunafanya ujinga.
 
Mkuu kuhusu vifo sidhani kama tumefikia nchi za wenzetu
Si kwa sababu huvihesabu ngoja huu utaratibu wa Mama wa Kupima na kuweka Data za wanaokufa kwa corona uanze uone, tatizo wanaokufa sana ni kundi la watu wazima wenye maradhi
 
Si kwa sababu huvihesabu ngoja huu utaratibu wa Mama wa Kupima na kuweka Data za wanaokufa kwa corona uanze uone, tatizo wanaokufa sana ni kundi la watu wazima wenye maradhi
Yani sehemu za kuhifadhi maiti kujaa kama wenzetu ni hadi uhesabu ndio uone hizo sehemu zimejaa? yani kuwa na uhitaji mkubwa wa mashine za kusaidia kupumua kama tunavyoona kwa wenzetu ni hadi uhesabu?

Wewe unajua takwimu vifo za hao watu wazima wenye maradhi zilikuaje before corona? kwa sababu hao watu wazima tunacheza nao bao na kunywa nao kahawa huku mtaani,tunapanda nao daladala na kuabudu nao kwenye nyumba za ibada, sasa kama kuna uongezeko la wingi wa vifo vyao kuzidi takwimu za vifo vyao vilivyo basi tungeona tofauti.
 
Mbona mashuleni wanafunzi awavai na wapo salama tu mpaka majumbani endelea kuiamini barakoa propaganda tu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom