Kwanini Wabunge hawakumlilia Kawambwa naye awajibike kuhusu matokeo mabaya ya elimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Wabunge hawakumlilia Kawambwa naye awajibike kuhusu matokeo mabaya ya elimu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, May 8, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sikutaka kulileta hili lakini inaonekana sina ujanja. Katika kikao kilichopita wabunge wetu wengi walionekana kukerwa zaidi na ripoti za CAG na zile za kamati kuhusiana na mambo mbalimbali. Wizara kadhaa zilinyoshewa kidole na hatimaye mawaziri wake wakaondolewa. Hata hivyo, binafsi naamini hakuna kashfa yenye madhara ya moja kwa moja na ya kudumu kama iliyoko kwenye elimu.

  KUanzia elimu ya msingi na sekondari kuna changamoto ambazo kwa kweli ni dhambi kwa watoto wetu. Cha kuudhi zaidi inaonekana wabunge wetu wamekubali hali ilivyo na sijasikia wengi wakitaka waziri wa elimu Bw. Shukuru Kawambwa awajibike pia kama walivyowajibishwa wale wa sekta ya afya. Ni kwanini? Ni kweli hawajaona uovu uliopo kwenye sekta hiyo? ni kweli wabunge wetu hawajaona hali ilivyo kwenye shula za kata na mamia ya shule za msingi vijijini na mijini?

  Hivi, inakuwaje Ngeleja anawajibishwa lakini Kawambwa anaachwa? Ni kweli sekta ya nishati ina umuhimu mkubwa kuliko elimu? Ni kweli madhara ya kukosa umeme wa kudumu kwa asilimia 14 ya wananchi wetu ni makubwa zaidi kuliko kukosa elimu bora na mazingira bora kwa asilimia zaidi ya tisini ya watoto wetu? Ni kweli kwamba wabunge wetu hawajasoma ripoti mbalimbali za elimu ambazo zimetolewa na CAG taasisi nyingine.

  Kwanini, hata upinzani hauonekani kukerwa na kushindwa kwa sera ya elimu ya serikali ya chama cha mapinduzi na badala yake na wao wako kimya kutaka watu wawajibike? Hivi ni mpaka walimu na wanafunzi nao wagome ndio tutajua kweli kuwa tatizo letu ni kubwa kuliko tunavyodhania?
   
 2. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,813
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  mkuu haujasomeka, tufafanulie zaidi
   
 3. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Me naona wabunge wetu hawako makini na jambo la elimu,yaani elimu kwao haina umuhimu kabisaa na ndio maana wabunge wengi ni vilaza,hili swala la elimu linatakiwa lianze kupigiwa kelele na sisi wenyewe majimboni kwetu,kwa sababu bungeni wanalikwepa kana kwamba halina umuhimu.
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hapa tanzania ndio kitu ambacho sikiilewi...ukiangalia nchi nyingi zilizoendelea Elimu na Afya ndio priority ya kwanza katika kila serikali hapa duniani...Hapa tanzania Sekta ya Elimu na Afya...oh my!! sijui hata nianzie wapi. Tumeshakua na wasomi wengi sana wanaongoza hii wizara ya elimu bt Elimu yetu bado haiendi mbele ukilinganisha na nchi zingine...hasa mikoani inatisha na kusikitisha sana....huyu waziri wa elimu hii CAG report haikumpitia but she's culpable just like the rest of them...:disapointed:
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mzee Mwanakijiji, hata mimi nimeshangaa sana wizara ya Elimu kutoguswa. Lakini kilichonijia kichwani kwa haraka haraka ni maslahi binafsi ya wabunge. Watu (Wabunge) wana maslahi yao kwenye wizara kama za Nishati, Viwanda, Fedha nk, wanaona kwenye wizara ya Elimu hakuna dili kubwa kubwa zaidi ya kumfaulisha mtoto wa ndugu yako kwenye mtihani, hawapati faida ya haraka kama kwenye Nishati na madini.
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  mitihani iliwahi kuvuja na watu wakapaza sauti kutaka mama ndalichako ajiuzulu, lakini akasema hang'oki na hakung'oka. na hajafanywa kitu.
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Wabunge walikuwa warespond to report ya fedha ya CAG ambayo haihusu matokeo ya wanafunzi.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa sababu;
  1. Wengi wa wabunge hawakuona link kati ya elimu ya madudu yaliyowafanya wawalilie wale wengine
  2. Wengi wa wabunge hawakuwa na hoja 'zao'... wengi walisimama kwenye ripoti za CAG kuwalilia wale wengine
  3. Labda walijua itakuwa ni kazi bure kwa sababu wanajua kuwa ni mtu wa mkubwa -- si tunaona jinsi anavyozungushwa wizara kwa miaka hii 6 iliyopita
   
 9. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Mkuu Hata wabunge wameshabaini kwamba tatizo ni CCM na JK! hayo mengine ya Ngeleja,Nundu Kawambwa ni zao la tatizo kuu nililotaja hapo awali
   
 10. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kawambwa wakwetu kutoka bagamoyo hata kama wangelia machozi ya damu wabunge hakuna kitu,zamu yetu watu wa mkoa wa pwani,ingawa ukweli kawambwa anapwaya......
   
 11. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Watoto gani?

  Hawa wanaovaa suruali za Pink mlegezo, viatu vya ulimi? na vi skin tight wanazunguza mitaani mida ya shule?

  Nadhani wakuwajibishwa ni wazazi!
   
 12. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  lazima mtu kutoka bagamoyo awepo kwenye baraza la mawaziri hata kama chizi
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwanza wizara ziko mbili zinazoshughulika na elimu, ikiwa ni pamoja na TAMISEMI ambayo aliyekuwa waziri wa nchi, Mkuchika, kahamishiwa kungine pamoja na madudu mazito kwenye wizara hii!
  Pili, watoto wa wabunge na wazito wengine nchi hii hawasomi tena shule hizi. Shule za serikali ni kama vile zimetelekezwa makusudi kabisa kwa kuwa wamiliki wa shule binafsi ni hawa wanasiasa, wazito serikalini na asasi zao. Shule za serikali zinadumazwa ili wazito hawa wafanye biashara ya elimu.
  Ninyi hamshangai ipo EWURA kwa ajili ya nishati na maji; ipo SUMATRA kwa ajili ya usafiri; ipo TCRA kwa ajili ya mawasiliano na utangazaji; ipo SSRA kwa ajili ya mifuko ya hifadhi ya jamii lakini hakuna chombo kama hicho upande wa ELIMU!
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,129
  Likes Received: 6,617
  Trophy Points: 280
  Mimi mkuu naungana na wewe,
  watoto wanaingia sekondari hawajui kusoma wala kuandika,
  hivi hilo ni kosa la mzazi au la wizara.

  Kawambwa ana mzizi mkali wa kuwafanya watu walisahau jina lake.

  Hata Mhesh. Zitto Zuberi Kabwe hawezi kukataa kuwa kwenye jimbo lake
  elimu ni hovyo hovyo.
   
 15. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Kwa hakika hili ni eneo ambalo TUNAJI-LISHA UPEPO NA kujifanya vipofu. lakini uhalisia wa madhara yake ni makubwa huko tuelekeako.
   
 16. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Elimu haina tatizo Tanzania.. PhD za bure kila mbunge akitaka anapata. Mrema anayo, Nagu anayo, Kikwete anazo zaidi ya 10. Sasa kwa nini wapige kelele na sekta isiyokuwa na shida????

  Shida ni sekta za pesa bwana.. na hiyo ndiyo Tanzania yetu, kichwa cha Mwenda kuzimu...
   
 17. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,685
  Trophy Points: 280
  Binafsi ninaweza kusema hivi, nadhani tunaongozwa na Rais msukule ambaye ubongo na mwili wake ni kama umekufa na hauwezi kufanya kazi isipokuwa kuwe na msukumo toka nje.
  Nimetumia neno gumu kidogo (msukule), lakini hii ni lugha ya picha nikiamini wengi wenu mtaelewa kirahisi kwa kuwa kila mmoja anajua kile msukule hufanya ama kufanyiwa.
  Suala la utendaji mbovu wa wizara za serikali, ulianza kuonekana tangu awamu ya kwanza ya utawala wa Kikwete. Mbaya zaidi matatizo mengi yanayosababishwa na mawaziri wake amekua akiyafumbia macho na kuziba masikio ili mradi tu alinde maslahi ya wahusika.
  Ugumu wake wa kutoa maamuzi kwa kuwa yeye ndiye "boss" wa baraza la mawaziri umekuwa ni wa kusuasua mpaka pale mambo yanapoharibika basi ndio utamuona kwa kujilazimisha anafanya uamuzi uliompasa kuufanya kabla.
  Mimi kwa lugha nyepesi kabisa,naamini huyu bwana nchi ilishamshinda muda mrefu hii ni kutokana na uwezo mdogo alionao kuongoza taasisi kubwa kama NCHI, anachofanya ni bora liende muda wake umalizike ili aendelee kula pensheni yake milele.
   
 18. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Hoja za wabunge hazikusimamia kwenye utendaji halisi bali kwenye kashfa za ufujaji / upotevu wa fedha basi. Ulikuwa ni mtazamo finyu na pengine ni kwa vile ripoti ya CAG ilikuwa imetoa ushahidi usioweza kubishiwa na hivyo kuwapa nguvu ya kuitisha serikali. Kuhusu utendaji halisi watadai kila sekta/wizara ina upungufu labda uwajibishe serikali yote ama uamue kwa vigezo dhanifu (subjective) kuhusu nani kazidi awajibishwe na nani ana nafuu aachwe.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  HIvi inawezekana kuwa na mafanikio katika nyanja nyingine bila kuwa na mafanikio katika elimu?
   
 20. d

  dada jane JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yetu macho na serkari hii. Huwezi kuamini kwamba serkali sasa hivi haitoi pesa zilizokuwa inazitoa yaani capitation. Kwahiyo matumizi mbalimbali sasa hivi hakuna kama vile chaki, vitabu vya kufundishia nk kwa sasa tunapiga lecture primary, mnashindwa kulipia maji taasisi kama shule ya watoto wadogo inakosa hata maji ya kunywa na matumizi mengine muhimu. Kwa ujumla hali si nzuri. Walimu tumeanza kuhakikisha watoto na vizazi vyetu hawawi walimu. Kwani wazazi wao tumeonja joto la kutosha. Inatosha!
   
Loading...