naa
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 783
- 1,056
Leo nlikua nasikiliza radio fulani nikasikia wanasoma barua zilizoandikwa na watoto waliokimbiwa na baba zao. Hii ikanifanya nikumbuke maisha yangu ambayo me pia nimekumbwa na mkumbo huu wa kukimbiwa na baba yangu ki ukweli roho imeniuma sana nmebaki kujiuliza ni sababu ipi kubwa na ya msingi inawafanya wakimbie majukumu yao?? Au huwa wanafeel vipi pale wanapowatelekeza wamama na watoto bila msaada wowote?? Tena wengine hata ukiaamua kuwatafuta akat tayar una akili zako bado wanakupotezea,Hapa hua nazidi kuona wanaume ni wakatili sana jamani hua natamani sana kujua sababu znazowafanya wawe hivi.