Kwanini waathirika wengi ni watu wa ndoa au wanaoishi pamoja?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kuna ripotii nimeangalia jana na kuona kuwa kumbe katika Tanzania watu wengi walioambukizwa HIV ni wale walioko kwenye mahusiano ya kudumu (ndoa). HIvi ni kwanini hili na wanandoa wanaweza vipi kujikinga bila kuonekaana hawaaminiani? Tena niliona na inaonesha pia kuwa ni watu wenye elimu zaidi ambao wameambukizwa zaidi.

Sasa katika mazingira haya wana ndoa wanafanya nini?
Je, mwenza wako asikishauri muanze kutumia kinga unafikiria nini? kwamba yeye siyo mwaminifu au anakushuku wewe siyo mwaminifu?
Je, mwanammke katika ndoa anaweza akashauri waanze kutumia kinga bila kujitakia matatizo?
Je, mwanamme ukirudi nyumbani na kukuta mke kanunua box la condom kwa ajili ya matumizi yetu utafikiria nini?

Na kwa upande mwingine, kwa wale wasio katika ndoa au mahusiano ya kudumu ukienda kwa mwanammke na ukakkuta ana condom ndani utaichukuliaje hilo?

Je ni utaratibu mzuri kwa mume na mke kwenda kupima mara kwa mara kwa ajili ya kupeana imani au kutaka kupima mara kwa mara ni ishara kwamba yumkini kati yao yupo asiye mwaminifu?
 
Huaminiana na kwenda kavu kavu akishazoea siku akipata cha nje condom kwake sumu anatwanga kavu matokeo ndo hayoo
 
Kwa kuwa wakwenda kavukavu na kwa kuwa ndoa nyingi siku hizi mmoja au wanandoa wote wawili wanatoka nje na huko nje kwa kuwa wamezoea kavu wanapiga kavu na kurudi wao kwa wao wapigana kavu so tatizo ni kupiga kavu
 
hii mwana sio bongo tuu hata nchi nyingine zimegundua hilo....sasa hapa cha singi ni kujifunza kuwa kwenye ndoa wat sio wahaminifu.
mbaya zaidi ni kwamba pamoja na ktoka nje ya ndoa bado wanakuwa hawana akili ya kjiinga.....
sasa bwana mie ndio maana nasema kuwa wewe kikuta kuwa bwana/mke wako kacheat bora chukuwe chako maana unaweza letewa gonjwa wakati wewe umejilinda miaka yote hiyo.

na statistically malaya ndio the safest kugonga!!!!
 
Kwa ujumla uaminifu katika ndo nyingi ni sifuri. Kama uaminifu upo ni kwa kipindi kifupi tu; miaka miwili hadi mitatu baada ya ndoa. Baada ya hapo ni fungulia mbwa tu!

Kuhusu kutumia kinga; hapa tunadanganyana zaidi kuliko kawaida. Ukiwauliza watu wanaotoka nje ya ndoa zao atakwambia anatumia kondom. Lakini muda si mrefu, mpenzi wake ana mimba!!! Yaani hapo hapafai kabisa. kwenye matumizi ya zana uongo ni mwingi kuliko ukweli. Yaani in public watu wengi wanasema wanatumia, lakini in privacy hawatumii kabisa.

Ila wenye ndoa wengi (wanaume kwa wanawake) si waaminifu katika ndoa zao. Tena wanawake ni zaidi. Fuatilia angaza, kuna kesi nyingi sana ambapo wanawake wanavyo, waume zao hawana!! Sehemu zote wanakopima hizi statistics ni sahihi, ndo maana wanakuambia overall wanawake ni wengi zaidi wenye virusi (Na wengi ni wale walio kwenye mahusiano ya kudumu - kama ndoa).

Huo ndo ukweli, ingawa hapa ukizua mjadala watu wanakwambia wanawake wengi ni waaminifu. Kwa wale walio makazini, tunayaona maofisini jinsi wake za watu wanavyobadilisha mabwana maofisini!

Wanaume wengi walio kwenye ndoa ndo wako kwenye prime time zao; yaani wana mapato ya ziada na wana privacy ya kutosha (hawako maofisini na wake zao) hivyo hutumia muda wa kukaa maofisini kuendeleza ngono. Kumbuka ofisini nyingi Tanzania (hasa serikalini) watu hawako busy kihivyo! Watu wanatoka ofisini muda wowote tena bila ruhusa na kurudi muda anaojisikia. Hii yote huchangia mambo haya na takwimu hizi
 
Sababu ni cheating. Wapenzi wa kawaida as long as walipima afya kabla ya affair wanakuwa ni waaminifu sana kuliko wanandoa hasa wanaume. Wanaume wengi kwenye ndoa ni wazinzi.
 
Sababu ni cheating. Wapenzi wa kawaida as long as walipima afya kabla ya affair wanakuwa ni waaminifu sana kuliko wanandoa hasa wanaume. Wanaume wengi kwenye ndoa ni wazinzi.

Si kweli, ukifanya utafiti utathibitisha kuwa kwenye ndoa wazinzi zaidi ni wanawake kuliko wanaume! Jiangalie zaidi!
 
Unaona wanawake ni wazinzi zaidi kwa kuwa ni si kawaida kwa mwanamke kucheat ila kwa mwanaume ndio uanaume. Am also working, jamii inawashangaa sana wanawake wenye affair ndio maana ina magnify tatizo. Jaribu kuchunguza ratio ya wanaume wanaocheat waliokuzunguka na wanaume afu kuwa mkweli kwa hili.

Wengi wanapima kabla ya kuoana lakini bado wanaingia majaribuni tu. Ni vigumu sana kusema kwa uhakika jinsia ipi inaongoza kwa kucheat.....wanaume hawajifichi sana kwenye hili lakini wanawake ni wasiri kweli. Ni vema kuzingatia pia kuwa ngono inahusisha jinsia zote mbili (mwanaume/mwanamke hafanyi ngono peke yake, anahitaji mtu wa jinsia nyingine).
 
Unaona wanawake ni wazinzi zaidi kwa kuwa ni si kawaida kwa mwanamke kucheat ila kwa mwanaume ndio uanaume. Am also working, jamii inawashangaa sana wanawake wenye affair ndio maana ina magnify tatizo. Jaribu kuchunguza ratio ya wanaume wanaocheat waliokuzunguka na wanaume afu kuwa mkweli kwa hili.

Si kweli kwamba tatizo linakuwa "magnified" wakati halipo. Mimi nimeshafuatilia kwa undani sana suala hili hadi nikafikia conclusion kuwa wanawake (has working class) wanatoka nje zaidi kuliko wanaume (working class). Ukisema vijijini wanaume ni zaidi, naweza kubali sababu sijaifanyia utafiti wa kutosha. Ila kwa working class ndungu yangu, wala hata sihitaji kufikiri mara mbili - wanawake ni zaidi!
 
Labdaa ofisi unayo fanya wewe kazi, na wanacheat na nani? Mimi nilikofanya kazi kwote wanawake cheaters hawafiki wawili. Lakini wanaume kama wapo walotulia hawafiki wawili pia. Na wanaume wanacheat na mabinti ambao hawajaolewa in most cases.

Back
Top Bottom