Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Kuna ripotii nimeangalia jana na kuona kuwa kumbe katika Tanzania watu wengi walioambukizwa HIV ni wale walioko kwenye mahusiano ya kudumu (ndoa). HIvi ni kwanini hili na wanandoa wanaweza vipi kujikinga bila kuonekaana hawaaminiani? Tena niliona na inaonesha pia kuwa ni watu wenye elimu zaidi ambao wameambukizwa zaidi.
Sasa katika mazingira haya wana ndoa wanafanya nini?
Je, mwenza wako asikishauri muanze kutumia kinga unafikiria nini? kwamba yeye siyo mwaminifu au anakushuku wewe siyo mwaminifu?
Je, mwanammke katika ndoa anaweza akashauri waanze kutumia kinga bila kujitakia matatizo?
Je, mwanamme ukirudi nyumbani na kukuta mke kanunua box la condom kwa ajili ya matumizi yetu utafikiria nini?
Na kwa upande mwingine, kwa wale wasio katika ndoa au mahusiano ya kudumu ukienda kwa mwanammke na ukakkuta ana condom ndani utaichukuliaje hilo?
Je ni utaratibu mzuri kwa mume na mke kwenda kupima mara kwa mara kwa ajili ya kupeana imani au kutaka kupima mara kwa mara ni ishara kwamba yumkini kati yao yupo asiye mwaminifu?