Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Nimekuwa nikifuatilia waandishi wa habari wa nchi hii, nikagundua kuwa zile habari muhimu sana, zenye maslahi mapana kwa Taifa hili hawaziandiki na badala yake, wao Kila siku ni kuandika "mapambio" ya kusifu na kuabudu viongozi walioko madarakani!
Waandishi wa habari wa nchi yetu, wamejijengea tabia ya kuwa hata kama ni "minor issue" ilimradi lmefanywa na watawala wetu wa CCM, basi watai-report kwa ukubwa Sana, wakati "big issues" kama hizo za kuuawa kwa raia zenye utata, wakizifukia!
waandishi wa habari Wana dhamana kubwa Sana ya kutuhahabarisha sisi wananchi kuhusu matukio mbalimbali yanayotokea hapa nchini.
Nikitoa mfano ni wa habari hii ilivyotokea majuzi ya Mauaji ya watuhumiwa watatu wa Mauaji wa ujambazi, yaliyotokea huko Serengeti, Mkoani Mara, ambapo uongozi wa Chadema, umetilia shaka Mauaji hayo, baada ya taarifa ya RPC wa Mara, kuwa watuhumiwa hao wa ujambazi, waliuawa, baada ya kurushiana risasi na askari.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chadema, kwa waandishi wa habari, ni kuwa taarifa hiyo inatia shaka Sana, kutokana na "circumstancial evidence" ya Mauaji hayo yalivyotokea.
Tufahamu pia wajibu namba moja wa Jeshi letu la Polisi, ni kutulinda sisi raia pamoja na mali zetu.
Kwa hiyo uongozi huo wa Chadema, umemuomba Rais Samia, aunde Tume ya Majaji, kuchunguza Mauaji hayo.
Uundwaji wa Tume hiyo ya Majaji, kwa tukio lenye utata, haitokuwa jambo geni, kwa kuwa kama mkumbukavyo, wakati wa utawala wa awamu ya nne, ya Jakaya Kikwete, aliunda Tume ya aina hiyo, baada ya Mauaji ya watu, ambao Polisi wetu walitoa taarifa kuwa waliwaua "majambazi" hao wakati wakijibizana risasi.
Hata hivyo baada ya Tume hiyo kutoa ripoti yake, ikaeleza kuwa hao waliotajwa na Jeshi letu la Polisi, kuwa walikuwa majambazi, hawakuwa majambazi, bali walikuwa wafanyibiashara halali wa madini, toka Ifakara!
Ili kuujua ukweli wa Mauaji yanayoendelea nchini kwetu, siku hadi siku, kwa madai ya Polisi, kuwa wameuawa baada ya kujibizana kwa risasi, inabidi Rais Samia, aunde Tume hiyo ya Majaji, Ili kuondoa utata huu, kwa kuwa kwa mfumo wetu wa utawala, mhimili pekee unaoweza kutoa hukumu ya kifo ni mhimili wa Mahakama baada ya kupokea ushahidi.
Kwa maana hiyo, kwa mujibu wa sheria zetu, hakuna mtu mwingine yeyote aliyepewa mamlaka hiyo ya kuua raia bila kwanza kupata ushahidi usiokuwa na shaka.
Kuendelea kuruhusu mtindo huu wa Polisi kujichukulia sheria mkononi, Taifa hili tunaliingiza kwenye hatari kubwa, kwa kuwa leo yamewakuta hao raia wa Serengeti, nani anayejua who is next, may be it can be you or me🥺
Mungu ibariki Tanzania