Kwanini Waandishi maarufu wa vitabu Tanzania wengi wao bado uchumi haujakaa sawa?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Nadhani ni wengi hapa tumewahi kununua vitabu katika safari zetu za elimu.

Unakuta kuna kitabu flani karibu kila mwanafunzi alikuwa nacho.

Ila sasa ukija kuangalia hali za maisha za hao waandishi unakuja kugundua vitabu hivyo haviwasaidii sana kiuchumi.

WHAT IS THE PROBLEM?
 
Wanaofaidika ni wachapishaji. Mwandishi analipwa kwa nakala 5,000 mchapishaji anachapa 50,000 au zaidi akiona kitabu kinauzika. Mwandishi anaachwa kwenye mataa. Hata matoleo mengine ya kitabu yakija kutolewa sijui kama waandishi wanapata malipo ya maana. Na mwandishi akifa, sijui kama familia yake inapata cho chote. Vitabu vya marehemu akina Aristablus Musiba (Njama, Kikosi cha Kisasi, Hofu, Hujuma n.k), Euphrase Kezilahabi (Rosa Mistika, Gamba la Nyoka, Dunia Uwanja wa Fujo, Kichwamaji, Nagona, Mzingile, Kichomi, Karibu Ndani, Dhifa, Kaptula la Marx n.k), Shaaban Robert (Adili na Nduguze, Kusadikika, Wasifu wa Siti Binti Saad n.k), Mohammed Said Abdullah (Kisima cha Giningi, Siri ya Sifuri, Mwana wa Yungi Hulewa, Duniani Kuna Watu n.k), Ben R. Mtobwa (Dar es salaam Usiku, Pesa Zako Zinanuka, Tutarudi na Roho Zetu? n.k); na wengineo sasa vinachapwa na kuuzwa kiholela tu. Sina uhakika kama familia zao wanalipwa cho chote.

Na tatizo hili haliishii kwenye waandishi tu. Tunaliona hata kwa wasanii. Wengi hawafaidiki na kazi zao kwa sababu hakuna mifumo imara inayohakikisha kuwa kazi zao haziibiwi. Kwa ujumla jamii yetu ni jamii iliyojaa wizi wizi tu na ujanja ujanja kuanzia kwenye siasa na katika mifumo yote ya maisha.
 
Naona hawa wachapishaji hawajaonja joto kabisa hata kipindi cha Magu, Hakuna sheria za kuwabana??
 
Hili ni tatizo la jumla mkuu. Hata kama sheria zipo lakini si umewaona akina Kigwangalla. Wamefanywa nini?

Wasanii wana BASATA. Waandishi pia naamini wana chombo chao. Na naamini misheria kibao ipo. Tatizo laweza kuwa ni utekelezaji wa misheria hiyo!
 
Haki miliki ni tatizo pia wabongo wengi hatupendi maandishi
 
Back
Top Bottom