Kwanini waajiriwa wengi wa Afrika hatuna utamaduni wa 'career break'?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,518
habari wadau..

najua wengi ni neno geni.. nilikuwa nafanya kazi ubalozi mmoja nyeti nilikuwa nashangaa sana wazungu wana career break... mtu anaacha kazi kabisa anapumzika hata 2 years bila kutafuta kazi yeyote.. anakwambia ana have fun tu.. kusafiri na kufanya hobbie zake tu.. unakuta accountant.. anapumzika uhasibu hata miaka miwili anafanya hobbie yake mfano anakuwa mpiga picha tu

kisha baada ya 2 year anarudi sokoni anasaka ajira mpya na anaendelea na career yake.. anakwambia anaji rejuvinate ki career

mfano hai.. ceo wa voda aliemaliza muda wake amejipa career break

https://tz.linkedin.com/in/ian-ferrao-65b8301

je ni njaa au utamaduni unatufanya waafrica tufanye kazi miaka 30 au 40 mfululizo bila kupumzika pumzika ....
 
Watakufa njaa ndugu...

Ukiacha kazi bongo, kupata kazi inakua vwita .....

Nchii hii inabadirika badirika kama kinyonga
 
njaa kisingizio tu.. wengine ni matajiri kabisa hata bila kazi anaishi maisha yale yale.. mfano mtoto wa mengi, bakhressa etc.. au mtu kama ridhwani kikwete.. nae utasema atakufa njaa

kuna watoto wa kishua kibao kwenye mashirika ila hawajipi career break pia
 
Hao ulio wataja una uhakika gani kuwa hawajipiki hiyo kitu ?

Lakini pia ujue tofautisha na aina ya kazi mkuu, sio kila kazi hii kitu inakua applied hata huko ulaya napo si kila mtu ana break
 
habari wadau..

najua wengi ni neno geni.. nilikuwa nafanya kazi ubalozi mmoja nyeti nilikuwa nashangaa sana wazungu wana career break... mtu anaacha kazi kabisa anapumzika hata 2 years bila kutafuta kazi yeyote.. anakwambia ana have fun tu.. kusafiri na kufanya hobbie zake tu.. unakuta accountant.. anapumzika uhasibu hata miaka miwili anafanya hobbie yake mfano anakuwa mpiga picha tu

kisha baada ya 2 year anarudi sokoni anasaka ajira mpya na anaendelea na career yake.. anakwambia anaji rejuvinate ki career

mfano hai.. ceo wa voda aliemaliza muda wake amejipa career break

https://tz.linkedin.com/in/ian-ferrao-65b8301

je ni njaa au utamaduni unatufanya waafrica tufanye kazi miaka 30 au 40 mfululizo bila kupumzika pumzika ....
Umesema ceo hatamie naweza pumzika. Tena wakwetu anaenda kupunga upepo ubalozi mfano Dr.Dau
 
Utamaduni wetu hauruhusu. Chukulia mfano Tanzania watu wengi huanza kuwa na malengo na kutunza fedha baada ya kupata kazi, lakini wenzetu tangu mtu anasoma anajifunza kuweka akiba benki
 
Mkuu hicho ni kitu kizuri sana kama umeajiriwa ila kama umejiajiri maana yake umejiangamiza
 
njaa kisingizio tu.. wengine ni matajiri kabisa hata bila kazi anaishi maisha yale yale.. mfano mtoto wa mengi, bakhressa etc.. au mtu kama ridhwani kikwete.. nae utasema atakufa njaa

kuna watoto wa kishua kibao kwenye mashirika ila hawajipi career break pia
Ukweli wabongo hawana tabia za kubarizi ukisikia kasafiri basi kaenda msibani au kasafiri kikazi. Ndio maana muda mwingine tunamawazo ya kienyeji. Ukienda arusha then kigoma utajifunza mengi kuanzia jiografia hadi maisha ya wenyeji
 
Utamaduni wetu hauruhusu. Chukulia mfano Tanzania watu wengi huanza kuwa na malengo na kutunza fedha baada ya kupata kazi, lakini wenzetu tangu mtu anasoma anajifunza kuweka akiba benki
Tunalo tatizo la mfumo wa maisha ukipata kazi ndo kwanza unatafuta nyumba ya kupanga. Kiwanja una plan kununua gari. Unaanza kuwaza harusi ada za shule
 
Sisi ambao hatukusoma na tumeajiriwa kwa kiwango cha chini kabisa hatutathubutu kufikiria kitu kama hicho.
 
Nyerere alisema "we must run while they walk".

Kawawa alisifiwa kwamba hakuchukua likizo kwa miaka na miaka.

Nikamuona mzee ngangari.

Baadaye nikaja kupewa story alikuwa anachukua mikopo kwa niaba ya chama mashirika ya umma, halafu hataki kulipa, anawaambia aliowakopa "weka mkopo kwenye bad loans ledger".

Sasa mtu kama huyo hata likizo kuchukua anaogopa. Anaona akichukua likizo, mtu atakayekuja kukaa badala yake ataona madudu.

Sasa mtu kama huyo umwambue habari za career break wakati hata likizo hachukui, itakuwa habari ngumu.

Nilivyokuja Marekani nikakutana na habari za likizo ya kazima. Ukifanya kazi miezi fulani, kama miezi 11 hivi, ni lazima uende likizo ya lazima angalau wiki tatu. Kama unafanya madudu akija mwenzako kufanya kazi yako ayaone.

Labda ndiyo funatimiza falsafa hizo za Nyerwre za "we must run while they walk".

Labda ndiyo tunatimiza falsafa za Kawawa za kuficha madudu.
 
Majority mishahara ni laki 7 hapo bado bodi ya mikopo haijakata,nssf,NHIF,makato benk etc

Wengi hio career break wataipatia kaburini labda.
 
Back
Top Bottom