Kwanini Vyuo Vikuu na Sekondari za Taasisi za Dini zinatoza ada kubwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Vyuo Vikuu na Sekondari za Taasisi za Dini zinatoza ada kubwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Jun 18, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Taasisi za Dini zinapinga kuondolewa kwa msamaha wa kodi kwao wakati Shule zao na vyuo vikuu vyao vinatoza gharama kubwa.Je ni haki kuwaondolea msamaha wa kodi kama hawapunguzi gharama za huduma zao? Nawasilisha.
   
 2. M

  Magehema JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mi nadhani ungefanya kautafiti kadogo kuona kama kuna uwiano wowote katika suala la gharama vs huduma, then ndio tuanze kujadili... Ni mtazamo wangu tu.
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Soma Daily News la 17/06/2009 utaona takwimu za Bungeni.
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapa mkuu Magehema ndipo wengi wanapokosea wakati wanafanya comparison!

  Ada zinazolipishwa na shule za dini....to me ni ndogo kabisa ukilinganisha na huduma wanazotoa huko! Mimi binafsi nimesoma huko.....bt huduma zinazotolewa acha kabisa! Kwa kifupi...mwanafunzi kuanzia form 1 to 6 anahakikishiwa kuwa na vitabu vyote vya kiada kwenye droo yake, vipindi vyote vinafundishwa, wanahakikisha wapo walimu kwa kila somo, wanafuatilia maendeleo ya mwanafunzi akiwa home au shule, wanatoa mazoezi ya kutosha....ndio maana shule hizi zinafaulisha sana!

  So to me ada yao bado ni ndogo sana ukilinganisha na huduma.....!

  Mmaroroi kama unamtoto jaribu kumpeleka huko....atavuna kilicho bora!
   
 5. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Of course st Augustine Univ ndo the most expensive University in Tanzania.........sasa kazi ya hii misamaha ni nini?
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nilishawahi kusema kuwa Vyuo vya binafsi lazima vipewe ruzuku kama fidia za uendeshaji wake, hata hivyo hivi karibuni serikali ilipokea Billioni ya shilingi toka Benki ya Dunia kwa ajili ya uboreshaji wa Vyuo vya umma, Lakini hakuna cha chuo vya dini wala binafsi walioweza kupata pesa hizo unategemea nini kama sio gharama kuwa kubwa sana,
   
 7. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  bila hivyo hawawezi kujiendesha. pia hawajalazimisha mtu kwenda kusoma pale, ni yule mwenye hela tu. they are not making any profit out of it i tell you. wengi wanapiga vita taasisi za dini, kwasababu tu ya wivu na ufahamu mdogo. hapa ndipo utaona ufahamu wa watz walio wengi ulivyo, hasa katika sakata hili lililopelekwa bungeni.
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ningependa sana kumpeleka Mtoto wangu lakini naogopa kwa kipato changu na ada zao zilivyo juu ataishia njiani.
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nadhani point ni kwamba, kama ada ya sekondari ya shirika la kidini (eg. Loyola) ni sawa na ada ya shule binafsi (eg. Mzizima), ni kwanini shule ya kidini isilipe kodi ambayo shule binafsi inalipa? Sidhani kama kuna tofauti ya huduma inayotolewa Loyola na Mzizima.
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  umesema ukweli, mimi huwa nashangaa sana kusikia watu wanasema kuhusu taasisi za Dini maana bila ya hizo watu wengi leo wangeshindwa kusoma na kupata huduma za afya
   
 11. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kodi gani ambayo hizi shule za dini hazilipi? Naomba kuelimishwa.
   
 12. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mmaroroi....cheap is always expensive mkuu.....mimi binafsi nimesoma huko Ordinary Level.....then high school kaenda Government school..aisee nakwambia kunatofauti kubwa sana sana kwa kila kitu!

  Kuhusu gharama....nimesomeshwa na wazazi wangu ambao ni peasants kwa kipato cha kudunduliza kweli but they managed!

  Try mkuu....hakikisha mwanao anapata elimu bora hasa basic to Ordinal Level!
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  VAT,
  Walikuwa hawalipi hapo awali. Ila bajeti ya mwaka huu inawataka waanze kulipa.
   
 14. Prince Alberto

  Prince Alberto Member

  #14
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebwana kwa kweli pamoja na mchango mkubwa unaotolewa na tasisis za dini hapa nchini,lakini linapokuja swalala adda mfano za shule zao ni juu sana,hebu neenda pale marian girls ,st margareth girls(mbeya),kibosho girls kwa uchache tu halafu uliza ada zao ndio utakapo shangaa ni kubwa mno,kwa hiyo hapa mtu unaweza kujiuliza swali dogo tu kama hawa jamaaa wanapata misamaa ya kodi mbona gharama za ada ni kubwa sana ukilinganisha na hali ya mtanzania wa kawaida ambapo inasemekana kwamba zaidi ya 57% ya watanzania wanaishi chini ya dola moja kwa siku,je uhalali wao wa kusamehewa kodi uko wapi?
   
 15. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ada zimewekwa kwenye level ya ushindani na shule nyingine za private zinazotoa huduma inayofanana. Vinginevyo ikiwa bure watoto woooote watataka kwenda huko na nafasi hazipo za kutosha. Kinachotokea ni kuwachuja kwa uwezo (kiakili, fedha, nk) ili kuwapata hao wachache. Faida itakayopatikana itawawezesha kuanzisha shule nyingine zaidi ili watoto wengi zaidi wapate nafasi. Kumbuka pia kwamba fedha inayopatikana inaelekezwa kwenye huduma mbalimbali nyinginezo sio lazima shule tu (mahospitali, nk) has sehemu za vijijini zilizo less priviledged. Cha msingi ni je, unapata huduma inayoendana na unacholipa?
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Zinatoza ada 'kubwa' kuendana na ubora wa elimu na huduma wanazotoa. nukta.
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Jun 18, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimesoma post zote hapo juu sijaona proper analysis. Unaposema ada kubwa, je, umelinganisha na huduma? Kama hujalinganisha basi bado hujasema chochote. Halafu sijaona mtu aliyetoa takwimu ya hizo ada. Kwa mfano huko St. Marian, St. Margareth, n.k. ada ni shilingi ngapi? Na katika Shule hizo walimu wapo wa kutosha? Vifaa vya kufundishia vipo? Walimu wako committed kiasi gani? Ufaulu wa wanafunzi ukoje? Wanafunzi kimaadili wanafundishwa vizuri? Tafadhali leteni takwimu, otherwise tutakuwa tunajadili kwa hisia hisia tu na tutakuwa kama Mheshimiwa Mkulo alivyokurupuka kufuta misamaha ya kodi lakini baadaye alipoelimishwa akairudisha!
   
 18. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa kabisa. Ukubwa wa ada unatoka wapi na huku nimezunguka na kijana wangu karibia shule zote hizi akina Loyola, Mbagala, nk nikakutana na mbango makuuubwa nje kwamba nafasi za form five zimeshajaa siku nyingi kwaheri. Ada zingekuwa kubwa si wangekosa wateja?

  Kama unaona ada ni kubwa, hii ndio opportunity yenyewe ya kuchangamkia. Ina maana ukianzisha shule yako una uwezo wa kutoza ada kidogo zaidi na ukasaidia watz wengi zaidi. Wahi basi anzisha yako!
   
 19. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania hadi leo hatujafikia kulipia ada ambayo ni thamani halisi ya elimu tunayoipata. Education is expensive bwana. Kwa vile tumelelewa na ujamaa tukiambiwa elimu kwa wote bure bla bla basi ukimtoza mtu ada anaona ni kubwa. Tunataka tutotoe tu watoto kama ndege halafu elimu wapate bure, eti tena elimu bora. Nani kasema.
   
 20. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nakupa kitu kimoja tu; linganisha maabara zao, halafu usiwe mnafiki, uje umwage data hapa.
   
Loading...