Kwanini vyombo vya habari kama Televisheni na Redio za Tanzania havina habari za biashara

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Habari za Biashara zinawafungua wananchi wakiwemo wakulima, wafanyabiashara na wafanyakazi juu ya mwenendo wa masoko. Sasa hapa Tanzania je ni kwanini hakuna kituo cha Televisheni au Redio chenye Habari za mashiko za Biashara kama vile Mwenendo wa Masoko ya Hisa ya Tanzania na Afrika Mashariki, mwenendo wa Bei za masoko ya bidhaa zikiwemo bidhaa za kilimo, nakadhalika.

Ina maana kwamba vyombo vyetu vya habari vinatuona watanzania hatuhitaji aina hii ya habari?

Sio habari za Biashara tu lakini pia hakuna Utabiri wa Hali ya Hewa ni kwanini je hakuna sheria ya kuwalazimisha vyombo vya habari kubeba aina hii ya habari kama wanavyolazimishwa kwa mujibu wa sheria kurusha vipindi vya watoto na elimu?
 
Sijafuatilia TV muda mrefu lakini nakumbuka ITV alikuwa na Habari za Uchumi na Biashara kabla ya habari za michezo, pia na utabiri wa hali ya hewa, umefatilia kabla ya kuleta hii thread?
 
Back
Top Bottom