Kwanini vyama vya upinzani vinakua halafu vinakufa kwa aibu hapa Tanzania?

daza steven

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
359
357
Juzi tuliambiwa tena na viongozi wakubwa wa Chadema kuwa CCM ikinusulika katika uchaguzi wa Octoba 2015 watajiudhuru siasa nasasa tunaona kila dalili ambazo zilizovikuta vyama kama CUF, NCCR MAGEUZI, TLP zinainyemelea CDM.

1995 viongozi wa NCCR MAGEUZI kama Mbele Malando na Lamwai waliwai kusema "ningumu kwa CCM kunusurika katika uchaguzi huu. Muda si muda kikawa chama doro.

Na ukiangalia hawa viongozi wetu wa upinzani wanafanana sana katika namna za uendeshaji wa vyama, Mfano hawa wahishimiwa wanafanana kabisa kama Prof. Haruna Lipumba, John Momose Cheyo, Zito Kabwe, Freemani Mboe, James Mbatia, Hashimu Lungwe, Agustino Lyatonga na Maalim seif.

Tuchangie hili tupate upinzani makini.
 
Yapo mengi ya yanayosababisha yote hayo.

Miongoni mwayo ni unafiki wa wanasiasa na Mfumo wa ujamaa tulioupitia hapo awali ambapo mpaka sasa Polisi na baadhi ya idara nyingine zimeendelea kutumikia chama tawala.
 
Vinakufa au vinauliwa? Kuna dhamira ya dhati kuwa na upinzani wa kweli nchini? Kuna uwanja sawa wa kufanya siasa kati ya vyama vya upinzani na chama tawala? Hebu kua mkweli kwa nafsi yako
 
1. Hawana mikakati/mioango
2. Wanahujumiwa
3. Tamaa ya madaraka
4. Wanaongozwa na mihemko
5. Wana lumbana/minyukano ya ndani
6. Wametanguliza maslahi binafsi
7. Wanatumiwa (baadhi yao)
 
Juzi tuliambiwa tena na viongozi wakubwa wa Chadema kuwa CCM ikinusulika katika uchaguzi wa Octoba 2015 watajiudhuru siasa nasasa tunaona kila dalili ambazo zilizovikuta vyama kama CUF, NCCR MAGEUZI, TLP zinainyemelea CDM.

1995 viongozi wa NCCR MAGEUZI kama Mbele Malando na Lamwai waliwai kusema "ningumu kwa CCM kunusurika katika uchaguzi huu. Muda si muda kikawa chama doro.

Na ukiangalia hawa viongozi wetu wa upinzani wanafanana sana katika namna za uendeshaji wa vyama, Mfano hawa wahishimiwa wanafanana kabisa kama Prof. Haruna Lipumba, John Momose Cheyo, Zito Kabwe, Freemani Mboe, James Mbatia, Hashimu Lungwe, Agustino Lyatonga na Maalim seif.

Tuchangie hili tupate upinzani makini.
Orodhesha kwanza vyama vilivyokufa
 
Adui mkubwa anayeuwa upinzani Tanzania ni CCM

CCM imeuwa Cuf.....Zanzibar-Jecha...Tanganyika-Lipumba

CCM imeuwa TLP......kada mtiifu Mrema

CCM Imeuwa NCCR .....ikapandikiza kijiji cha wanafiki

Sasa hivi ccm inapambana mchana na usiku kuiuwa cdm....bahati mbaya kwa ccm kikwazo kikubwa ni mbowe nasasa wanazusha kila aina ya ushenzi.....
 
Tatizo ni tiss, NEC na police, hawa ndio wanaua vyama vya upinzani tanzania, maana wamevaa gwanda na ccm kwa lengo la kufanya siasa kwa lengo la kuua upinzani, na hili halijaanza leo wala jana, mchonga aliviua alipoingia madarakani mara tu baada ya uchaguzi wa vyama vingi uliomuweka madarakani, na mpaka sasa warithi wake wanafanya hivyo kwa kutumia vyombo vya usalama.
 
Juzi tuliambiwa tena na viongozi wakubwa wa Chadema kuwa CCM ikinusulika katika uchaguzi wa Octoba 2015 watajiudhuru siasa nasasa tunaona kila dalili ambazo zilizovikuta vyama kama CUF, NCCR MAGEUZI, TLP zinainyemelea CDM.

1995 viongozi wa NCCR MAGEUZI kama Mbele Malando na Lamwai waliwai kusema "ningumu kwa CCM kunusurika katika uchaguzi huu. Muda si muda kikawa chama doro.

Na ukiangalia hawa viongozi wetu wa upinzani wanafanana sana katika namna za uendeshaji wa vyama, Mfano hawa wahishimiwa wanafanana kabisa kama Prof. Haruna Lipumba, John Momose Cheyo, Zito Kabwe, Freemani Mboe, James Mbatia, Hashimu Lungwe, Agustino Lyatonga na Maalim seif.

Tuchangie hili tupate upinzani makini.
Ili ukue vizuri inategemea mazingira ya malezi yako (makuzi)
 
Vinakufa kwa sababu ya unafiki, uzandiki na uongo. Haiwezekani mtu mliyekuwa mnamtuhumu kuwa ni fisadi kabla ya kujiunga na chama lakini baada ya kujiunga chamani mkaanza kumsafisha kwa nguvu zote.
 
Juzi tuliambiwa tena na viongozi wakubwa wa Chadema kuwa CCM ikinusulika katika uchaguzi wa Octoba 2015 watajiudhuru siasa nasasa tunaona kila dalili ambazo zilizovikuta vyama kama CUF, NCCR MAGEUZI, TLP zinainyemelea CDM.

1995 viongozi wa NCCR MAGEUZI kama Mbele Malando na Lamwai waliwai kusema "ningumu kwa CCM kunusurika katika uchaguzi huu. Muda si muda kikawa chama doro.

Na ukiangalia hawa viongozi wetu wa upinzani wanafanana sana katika namna za uendeshaji wa vyama, Mfano hawa wahishimiwa wanafanana kabisa kama Prof. Haruna Lipumba, John Momose Cheyo, Zito Kabwe, Freemani Mboe, James Mbatia, Hashimu Lungwe, Agustino Lyatonga na Maalim seif.

Tuchangie hili tupate upinzani makini.

Jibu ni mmoja tu katiba mbovu
 
"Wana CCM msiwe na hofu kwamba chama hiki kinaweza kuondolewa madarakani ktk uchaguzi huu WA mwaka huu NA hata hizo chaguzi zitakazofuata, Mimi nimewatuma marafiki zangu ili waende wakahamasishe upinzani ili kutimiza matakwa ya wakubwa wanaotutaka tuwe NA mfumo WA vyama vingi. Wote IMF, WB, UN wanatutaka tuwe NA mfumo wa vyama vingi kama bado tunapenda kuendelea kupata Mikopo yenye masharti nafuu kutoka kwao:"

Haya ni maneno yaliyonukuliwa kutoka kwenye hotuba ya Mwalimu J.K.Nyerere, 1995 aliyoitoa kwenye mkutano WA Kampeni ya Urais ktk Uchaguzi Mkuu WA Kwanza Tz, mjini Morogoro akimnadi B.W.Mkapa.

Ushauri:-

AKILI kumkichwa na UJINGA nao kumkichwa
 
Mimi naona kunakitu kinaitwa dhambi ya asili ambayo inakozi natura death, kwani sababu kubwa ya kuletwa kwa mfumo wa vyama vingi ni kuexasaizi democrasia nchi yaani vyama pinzani vifanye demorasia kuzidi CCM lakini imeonekana kuwa aibu kwa wapinzani kufanya kilichosababisha waje. Ni ujanja ujanja tu wanafanya hakuna chaguzi za kidemocrasia kama CCM.
Wenyeviti ni walewale tangia kuanza kwa vyama vingi, wengine wanamiaka zaidi ya 20 katika kiti. ACT Wazalendo chenyewe kikamaliza kabisa kwa kuweka kiongozi mkuu wa chama yaani mmiliki wa chama.
 
Back
Top Bottom