Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Mimi nafikiri wakati umefika viongozi wa serikali wawe mfano wa utekelezeji wa operations zote zinazoanzishwa na serikali badala ya wao kubaki wahamasishaji tu bila ya wao wenyewe kushiriki kikamilifu na kwa vitendo kwa kuonyesha mfano.
Mfano zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma liliishia tu kwa watumishi wa kawaida ila sidhani kama viongozi wa juu wa serikali walihusika katika zoezi hili.
Sasa wameibuka na operation ya kuhisi watu fulani ama wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya au wanatumia madawa hayo na kuamua kuwapima na kutangaza hadharani matokeo.
Binafsi nafikiri wakati umefika kwa serikali kuonyesha mfano kwa vitendo na kwa kuanza viongozi wote wa juu waende wakapimwe kama wanatumia madawa haya na vipimo hivyo vifanywe na taasisi zisizo za kiserikali au zilizoko nje ya nchi na matokeo ya vipimo hivyo yatangazwe hadharani na kiongozi atakaebainika kutumia madawa hayo awajibike mara moja kwa kujiuzulu nafasi yake.
Na kama kweli tuko seriuos tutunge sheria inayomtaka kila mtu anaetaka kugombea naafasi mbali mbali za uongozi wa nchi hii shariti kwanza apimwe kama anatumia madawa hayo na akibainika kutumia basi sheria itamke wazi kuwa anakuwa amepoteza sifa ya kugombea nafasi yoyoye ile ya uongozi katika nchi hii.
Hili likitushinda basi tuache kufuatilia na kuwapima baadhi ya watu na badala yake tu-deal na wasambazi na wauzaji wa madawa haya.
Hivi nani kati yetu ana uhakika wote wanaokamata, wanaotoa maagizo watu wapimwe, wanaotoa taarifa za watumiaji na hata wanaopima kama wote hawa hakuna miongoni mwao anaetumia madawa haya?