Uchaguzi 2020 Kwanini viongozi wetu wa Dini wanatusisitiza sana tudumishe amani yetu, lakini wanashikwa na kihoro kuwaambia wanasisiasa wetu watende haki?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,130
Imeandikwa kwenye Biblia takatifu, katika kitabu cha Mithali, sura ya 14:34 nanukuu kama ifuatavyo "Haki huliinua Taifa, Bali dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.

Kwa maandiko hayo ya kwenye Biblia takatifu, maana yake ni kuwa huwezi kuitenganisha HAKI na AMANI na kwa maana nyingine vitu hivyo ni sawasawa na chanda na pete.

Hata hivyo tumekuwa tukiwasikia mara nyingi, viongozi wetu wa kidini wakituhimiza sana sisi waumini wetu tuidumishe amani ya nchi hii, tena wamekuwa wakienda mbali zaidi na kutuonya kuwa amani ya nchi hii ikitoweka, kuirejesha itakuwa ngumu sana!

Ndipo hapo ninapowauliza hao viongozi wa Dini, ambao naamini wao wanavisoma sana hivyo vitabu vya dini na wana uelewa mkubwa zaidi yetu sisi waumini wa madhehebu hayo, kuwa ni kwanini wanatusisitizia sana sisi waumini wao tudumishe amani ya nchi hii, lakini wanashikwa na "kigugumizi* kuwasisitizia sana viongozi wetu wa kisiasa, nao watimize wajibu wao muhimu sana wa kutenda haki, pale wanapolitumikia Taifa hili?

Hivi ni nani asiyejua kuwa viongozi wetu wa kisiasa, wanaziminya waziwazi HAKI za wananchi, wanapotekeleza majukumu yao?

Tunafahamu pia nchi yetu imepata msamiati mpya, katika utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 ya " watu wasioujulikana" ambao haukuwepo katika awamu za serikali zilizopita!

Tunaambiwa na Jeshi letu la Polisi, kuwa waliomwua aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo, miaka zaidi ya 4 iliyopita, ni WATU WASIOJULIKANA. Kwa kuwa hadi Leo hawajapatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Tunaelezwa pia na Jeshi letu la Polisi kuwa watu waliomteka, msaidizi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeaman Mbowe, BenSaanane, zaidi ya miaka 4 iliyopita, ni WATU WASIOJULIKANA!

Tumejuliishwa pia na Jeshi letu la Polisi nchini, watu waliomteka, mwandishi wa habari maarufu nchini, Azory Gwanda, zaidi ya miaka 3 iliyopita, ni WATU WASIOJULIKANA!

Tunaelezwa pia na Jeshi letu la Polisi nchini kuwa watu waliomminia risasi mfululizo zaidi ya 15 mwilini mwake, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu, eti na wao, ni WATU WASIOJULIKANA!

Tunaambiwa na Jeshi letu la Polisi nchini kuwa watu waliomteka, mfanyibiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji, eti na hao ni WATU WASIOJULIKANA!

Matukio ya kuuawa watu, kutekwa na kupotea, ni mengi sana, katika utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 na umevunja rekodi ya serikali zote za awamu zilizopita, tokea tupate Uhuru wetu!

Tumeshuhudia pia Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally, akitamba kuwa chama chake, kitaendelea kutumia vyombo vya dola vilivyopo nchini, ili kuendelea kubaki madarakani!

Hivi hayo maneno aliyoyatamka Dkt Bashiru Ally ni ya kuyatamka hadharani au ni ulevi tu wa madaraka?

Ni dhahiri kuwa maneno hayo aliyoyatamka Dkt Bashiru Ally hadharani, ndiyo yanayochochea kwa kiasi kikubwa, uvunjifu wa amani hapa nchini na kutaka kuikimbiza amani tuliyo kuwa nayo hapa nchini tokea tupate Uhuru wetu toka kwa mkoloni
 
Jukumu namba moja ya Jeshi letu la Polisi, ni kulinda uhai wa raia na mali zao.

Kama jukumu hilo limewashinda, ni kwanini IGP Sirro anaendelea na kazi na hafukuzwi kazi?

Kuna ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwa kuna "conspiracy" kati ya Jeshi letu la Polisi na watawala wetu wa CCM katika kufanya uharamia huu unaoendelea hapa nchini
 
hivyo tumekuwa tukiwasikia mara nyingi, viongozi wetu wa kidini wakituhimiza sana sisi waumini wetu tuidumishe amani ya nchi hii, tena wamekuwa wakienda mbali zaidi na kutuonya kuwa amani ya nchi hii ikitoweka, kuurejesha itakuwa ngumu sana
Kwahiyo, kwa maoni yako kauli hizi zina exclude wanasiasa!?
 
Kuwajibika kumekuwa ni msamiati mgeni kabisa katika uongozi huu wa utawala wa serikali ya awamu ya 5.

Nakumbuka katika uongozi wa awamu ya kwanza, chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere, kuwa Waziri wa Mambo ya ndani wa enzi zile Alhaj Ali Hasaan Msingi, alijiuzulu wadhifa wake kutokana na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia yaliyotokea mkoani Shinyanga.

Ni kwanini katika uongozi huu wa utawala wa serikali ya awamu ya 5 wanaendelea na mambo yao "as usual" wakati raia mbalimbali wakipoteza maisha yao, sehemu mbalimbali nchini?
 
Kwahiyo, kwa maoni yako kauli hizi zina exclude wanasiasa!?
Nina wa-include pia na wanasiasa wetu wanaotuhimiza tudumishe amani, bila kuwaasa wanasiasa wetu nao watende haki wanapotekeleza majukumu yao
 
Haki ni msamiati katika serikali ya CCM. Tuchange hela tuwqnunulie kamusi waelewe maana ya haki na kuwa kupita bila kupngwq ni upindishaji wa haki za binadamu.
 
Wanajua tatizo lipo kwenye meza kuu waliyokaa lakini shida nani aanze kusema!
Tunajua kweli kuwa tatizo lipo kwenye "the highest office in our country" kwa huyo Jiwe.

Lakini viongozi wa dini walipaswa wamwambie ukweli huyo mtu kuwa HAKI huinua Taifa na dhambi ni aibu kwa watu wote, badala ya kumwogopa kupita kiasi.
 
Mimi sijui Sana Habari za viongozi wa dini ya Kikristo ila kwa viongozi wetu wa kiislamu tatizo ni UNAFIKI na NJAA
Mfano:

Mwanaharakati mkubwa wa kiislamu Sheikh Issa Ponda kabla kidogo ya kampeni alitoa '' waraka wa maimamu' wenye kurasa 30!!! Pomoja na mambo mengine alizungumzia mamia ya masheikh waliopo jela bila dhamana wala kupelekwa mahakamani na akazungumzia mateso wanayo tapata mpaka wengine wamehasiwa kabisa na wengine kua vichaa kwa sababu ya mateso makali kama haitoshi kaelezea vizuri kuhusu wale 72 walikamatwa na SMZ kabla ya JPM kua rais na jinsi gani walivyoletwa Tanganyika..

Vile vile ameeleza Kwa ufasaha jinsi wimbi la kamatakamata lilivyo anza kila mkoa Tanganyika mpaka kufika kuonyesha takwimu ya mamia waliopo jela na namba za kesi zao... Utafiti unaonyesha kuanzia mwaka 2016 Tanzania pamekamatwa watu wengi kwa tuhuma za ugaidi kuliko Afghanistan!

Matokeo yake Sheikh Ponda alikamatwa na kupelekwa sehemu isiojulikana baada ya muda akaonekana anaendesha BMW mpya na mambo yake Safi Sana.

Hivi Sasa yeye na jopo lake ni wanaharakati mkubwa wa JPM na hata ile michango ya kuwasaidia Familia za waliopo jela imepigwa stop 🛑 maana wanaamini inaweza kuleta hisia za kumchukia JPM.

Hawa ni "viongozi wa dini'' we have long way to go
Hapo bado BAKWATA ukisikia vituko utashangaa
 
Kama wanalazimishwa kwenda kinyume na taratibu za dini zao, unategemea watasema nini? Cha kushangaza wanahubiri amani wakati wakijua kabisa sheria ni mbovu kama samaki aliyechina.
 
Tunajua kweli kuwa tatizo lipo kwenye "the highest office in our country" kwa huyo Jiwe................

Lakini viongozi wa dini walipaswa wamwambie ukweli huyo mtu kuwa HAKI huinua Taifa na dhambi ni aibu kwa watu wote, badala ya kumwogopa kupita kiasi.
Wewe unaweza kuwa wa kwanza kumwambia? Jaribu uone.
 
Tumbo. Wamewekwa mfukoni mwa shati na wanasiasa, wengi ni vibaraka na wanaridhika na tu msaada tu dogo tu dogo hasa wale wa upande wa pili njaa kali
 
Wewe unaweza kuwa wa kwanza kumwambia? Jaribu uone.
Hata hivyo asimgeuze Mungu wetu kama mtani wake..........

Dawa.yake ni wananchi tujitokeze tarehe 28 mwezi huu kumpigia kura yule mwenye Sera ya maendeleo ya watu na tuimwage kabisa Pombe ambayo ni "unfit for human consumption"
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom