Kwanini viongozi wetu hawapambani na walanguzi kama sokoine? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini viongozi wetu hawapambani na walanguzi kama sokoine?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Mar 14, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nimetafakari kwa kina nimeona niliwasilishe suala la mfumuko wa bei kwenu wanaJF ili tulijadili huenda likaishtua Serikali yetu inayoitwa sikivu.


  1. Mfumuko wa bei za Vyakula

  Bei za vyakula zimekuwa zikipanda kila kukicha, sababu ya kupanda kwa bei hizi tunaelezwa kuwa ni gharama za usafirishaji. Najua mnafaham jinsi ambavyo wakulima wanabanwa huko vijijini na walanguzi. Sasa kama hali ni hiyo. Kwanin tunalanguliwa vyakula ambavyo wakulima wanaviuza kwa bei ya chini sana tena kwa kutumia mizani rubunifu????Kwanini middlemen wanaweka cha juu kuliko bei ya producers????Kwanini serikali inafumbia macho walanguzi???Sokoine aliwezaje kudhibiti hili serikali hiyo hiyo ya CCM sasa hivi inashindwa???Ipo wapi ile sheria aliyoitumia Sokoine wakati ule?????Wabunge kwanini hamtungi sheria kuwabana walanguzi???Hapa Dar es salaam kila duka lina bei yake kwa bidhaa hiyo hiyo, kwanini iwe hivyo??mbona mafuta ya petrol kuna bei elekezi??inashindikana nini kuwa na bei elekezi kwenye bidhaa mbalimbali??iwekwe level ya wauzaji wa mwisho kuset price jamani. Ikifanya hivyo wauzaj wa mwisho watawabana mamiddlemen au watapunguza chain ya mamiddlemen.uweke utaratibu wa kupunguza middlemen


  2. Suppliers wa Bidhaa Serikalini

  Hapa kuna wizi mkubwa sana ambao unasupportiwa na Sheria yetu ya manunuzi, Hii sheria ningelikuwa na mamlaka ningeichoma moto au kuitupilia mbali. Unakuta mtaani bei ya rim la karatasi ni Tsh 10,000, rim hilo hilo likiuzwa kwenye maofisi ya serikali linakuwa Tsh 20,000/30,0000. Ukiuliza utaambiwa quotation ya bei ya chini ilikuwa ni Tsh 20,000/30,000. Huu ni upumbbavu jamani. Hatuwezi fika kwa utaratibu huu. Hiyo hela yenyewe inaifikia serikali kwa tabu, then ikishafika hazina matumiz yake yanakuwa niyakipumbavu sana. Kwanini tunajikomoa wenyewe???Kweli tunahitaji faida, lakin kupata faida 500% pia sio sahihi, ni wizi kama wizi wa kuku/fedha za EPA au ni kama mtu aliyeamua kutemper na mzani ili kumrubuni mlaji. Kwanini serikali hailioni hili???Wabunge mbona hamurekebishi sheria hizi za kifisadi???Mawaziri/Rais mnaenda sana nje ya nchi, haya si ndiyo mambo ya kujifunza kwa wenzetu na kuyaiga????Kwanini tunaishia kuiga kuvaa tu na sio kuiga mambo yenye manufaa kwa wananchi????

  Kwanini Serikali isiwe na sheria itayoweka wazi kuwa si ruhusa mtu/mfanyabiashara kuweka cha juu/commission zaidi lets say 5%/10%/25% ya bei halisi???Kwanini mtu aweke cha juu 300% na serikali inaangalia tu??Hiki si ndicho kigezo cha kuwabana walanguzi ambacho Sokoine alikuwa anakitumia???Kwanini serikali imeacha utaratibu huu kumlinda mlaji na kudhibiti matumiz mabaya ya fedha za umma???Kina Pinda hii si ndiyo kazi mnayotakiwa kuifanya kwa watanzania???Mmetoka wapi na kazi za kuuza ardhi ya serikali kwa wawekezaji????mliteuliwa kuwa wauza ardhi tena kwa USD 0.25 kwa heka hapa nchini???Haya mnayotutendea yatawaeleleza hapa hapa dunia mana watanzania waliwaamin kuwa mtawakomboa instead mmegeuka watu mnaowadidimiza watanzania, very bad.

  WanaJF naomba mchangie hoja juu ya mambo haya, mimi naimani lazma kuna kitu cha kuongea tu katika haya
   
Loading...