KWANINI VIONGOZI WETU HAWAANDIKI AUTOBIOGRAPHIES au BIOGRAPHIES???

galiya

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
302
131
Viongozi karibu wote wa nchi hii hawana utamaduni wa kuandika AUTOBIOGRAPHIES/BIOGRAPHIES {Historia ya maisha yao) kama walivyo viongozi wa nchi nyingine. Je ni kwasababu gani hawafanyi hivyo?

AUTOBIOGRAPHY ni pale mtu anapoandika historia ya maisha yake yeye mwenyewe na BIOGRAPHY ni pale mtu mwingine anapoandika maisha yako kwa jinsi anavyokujua au unavyomuelezea. Kuandika AUTOBIOGRAPHY AU BIOGRAPHY ni kitu MUHIMU SANA hasa kwa kiongozi. Ieleweke pia AUTOBIOGRAPHY/BIOGRAPH sio tu inaongelea maisha binafsi ya mtu bali pia hua na mambo mengine muhimu hata yenye manufaa kwa taifa. Mwalimu Nyerere, Sokoine, karume, Mwinyi, Mkapa na wengi wengineo hawa hawakuandika.

Nampongeza Mh Rais wetu mpendwa J.KIKWETE ambaye ana BIOGRAPHY ambayo ina mambo mengi. Pia Marehemu R.M. KAWAWA nae ana BIOGRAPHY. Katika BIOGRAPHY ya Kawawa kuna mambo mengi ambayo hayajaandikwa popote mfano ameeleza kwamba katika maasi ya 1964 yeye na Mwalimu walikimbizwa kufichwa Kigamboni kwenye nyumba ya mzee mmoj ambae miaka ya baadae walimpa zawadi ya baiskeli. Kulikua na uzushi mkubwa kwa miaka mingi kuhusu mahali Mwalimu na Kawawa walikokimbilia kwa siku mbili za maasi.. Wengine wanawezakuona hili si jambo la maana lakini ni muhimu sana kwa wanahistoria. Mzee G. KAHAMA ambae huenda ndie Mtanzania aliyekua waziri kwa miaka mingi kuliko mwingine yeyote nae ana BIOGRAPHY yake nzuri iliyoandikwa na mwanae na kuna mambo mengi ya muhimu kwani ameelezea hata harakati za kupigania uhuru.

Mh P. MSEKWA ni hodari sana wa kuandika vitabu na katika kitabu chake kipya alichotoa mwaka huu (AUTOBIOGRAPHY) ameeleza mambo mengi muhimu. Mojawapo ambalo ameliweka sawa na ambalo limekua likikosewa sana na viongozi wengi pamoja na Waandishi ia kuhusu kujiuzuru kwa Mh A.H. Mwinyi mwaka 1977.Ukweli ni kwamba Mwinyi alikua Waziri wa Mambo ya Ndani . Yakatokea mauaji Shinyanga na Mwanza. Baada ya wiki mbili ikasikika taarifa ya habari kua Mwinyi amejiuzuru kutokana na vitendo hivyo vilivyofanywa na watu wa chini yake. Wengi wamekua wakiamini Mwinyi ndie alieamua willingly kujiuzuru mara tu baada ya matukio hayo. Hii si sahihi.. Kwa mujibu wa Msekwa ni kwamba Rais Nyerere alimwita Mwinyi Msasani na kumwambia INABIDI UJIUZURU. Baada ya majadiliano marefu Mwinyi akakubali. Mwinyi akaenda kuandika barua NZURI SANA ya kuomba kujiuzuru. Barua hiyo ilimfurahisha SANA Nyerere kiasi kwamba aliwaandikia barua Mawaziri wote na Wakuu wa Mikoa wote huku akiambatanisha barua hiyo. Kutokana na hilo, Nyerere mara moja akamteua Mwinyi kua Balozi wetu Misri.

Viongozi wanapoandika vitabu husaidia kuweka wazi mambo mengi.Binafsi nimesoma AUTOBIOGRAPHIES za MARAIS 12 WA US na AUTOBIOGRAPHIES za MARAIS NA WATU MAARUFU DUNIANI na FIRST LADIES WENGI na nimejifunza mambo mengi. Watanzania wengi hawana culture ya kujisomea vitabu, sijui kwanini? DEE LEE, HAVARD CFP Financial Educator aliwahi kuandika article kuhusu jambo hili;
"The more you read, the more you know. The more you know, the smarter you grow. MOST BLACKS
never read. The best way to hide something from BLACK PEOPLE is to put it in a book. Now we live
in the information age. There are numerous books available in bookshops and via internet, yet they
refuse to read... They stupidly say they are too busy.. Dont worry about any blackman knowing the contents
of this Article, THEY NEVER READ...."

Hata Mwalimu Nyerere alikua msomaji mzuri wa vitabu kama Mh B. Mkapa alivyosema tarehe 21.10.1999
JK Nyerere was a voracious reader of books. While we are always advised to read at least 50 books a year,
he was reading not less than 100 books a year! What helped to pursuade him to accept a bigger house,
in his own words spoken light heartedly, was because he had run out of room for books in his former
smaller house. He was a man of great vision, he had exceptional intellect and wit..."

Hivyo basi,Great thinkers, kwanini Viongozi hawaandiki AUTOBIOGRAPHIES/BIOGRAPHIES na kwanini hatupendi kusoma vitabu??
 
Busy sana... na maisha maana ukikaa usome vitabu na hii nchi da gama utalala njaa au mtoto hatoenda choon na shule pia
 
biography ya jk hawajaweka vitu vingi mfano,.suti tano alizohongwa na waarabu,manufacturing of teachers,foleni dsm ni ishara ya maisha bora kwa kila mtanzania,.jinsi alivyoingia madarakani kwa hela ya wizi ya EPA,nk,nk,nk
 
ISMAIL
Kwahiyo ni kweli alichosema DEE kwamba mnajifanya mko bize sana??
 
Back
Top Bottom