Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,795
- 71,214
Nimejaribu kufanya kautafiti nimegundua kiongozi au mwananchi wa kawaida anayetoka CCM na kujiunga kwenye siasa za upinzani anakuwa na heshima kubwa kwenye jamii kuliko wale watokao Upinzani na kujiunga CCM (wengi wanaita kuunga mkono juhudi).
Hebu tumwangalie kubwa lao Lowassa, alipojitoa CCM akapata heshima kubwa kwenye jamii hata hao CCM walikuwa wanambeza kumbe wanamtamani mno. Karudi huko hakuna anayemjali tena pamoja na kupokelewa kwa heshima zote za CCM.
Angalieni Waitara na Bulaya nani anaheshima katika jamii?
Kafulila sio Kafulila tena yule "tumbili" kiboko ya kutetea wanyonge. Ona Gekule kule Babati alivyokuwa mbunge wa Chadema na rafiki wa wanababati na alivyo sasa mbunge wa CCM na adui wa RAIA wa Babati?
Vipi Nyalandu baada ya kuutosa ubunge wa CCM? Mbona heshima imekuwa kubwa mno huwezi kumlinganisha na Dr Mkumbo au yule wa Siha?
Mifano ni mingi mno.
Swali linabaki kwa nini wanaokimbilia CCM wanaonekana ni NJAA TUU zinawaongoza?
Askofu Bagoza kasema ni vigumu kuwaongoza wenye njaa, nami nasema NI VIGUMU KUONGOZWA NA WENYE NJAA NA TAMAA.