Kwanini viongozi wa upinzani wasiachane na siasa na kufanya biashara nyingine ?

Watanzania ndo maana tunafeli hata mitihani
Mwenye uzi anapaswa kupingwa kwa Facts siyo matusi

Anyway Urais ni zaidi ya alivyovitaja hapo
1.Tunataka uhuru wa kujieleza na kuongea
2.Tunataka amani itamalaki hatutaki watu kupotea kwa kutekwa
3.Elimu bure nakubaliana na wewe. Ila ni Elimu Mbovu sana, mitaala aiendani na maisha halisi ambayo Mtanzania anatakiwa kuyaishi baada ya shule
4.Makadirio mabaya ya ushuru na kuwaumiza wafanya biashara,
5.Utumbuaji majipu pengine bila kufuata utaratibu,
6.Haki za Raia ziko wapi
7.Demokrasia iko wapi
8.Upendeleo ndani ya Viongozi wa Serikali,
9.Mikopo ya Elimu ya Juu umeendelea kuwa wimbo
10.Uchumi umeyumba bwana
Dah ni Mengi sana
Mkuu huyu jamaa hana hoja,ndo maana watu hawamjibu kistarabu kama ulivyomjibu wewe. Nina uhakika hata haya majibu yako hatayaelewa.
 
Kwa usawa huu ni ndoto sana upinzani kushinda serikali za mitaa na hata tu uchaguzi wa udiwani , ubunge , Urais ! Ni kama tu hawatashinda tena. Washukuru awamu zilizopita za kudekezana mpaka watu wanaitwa Ikulu kunywa juice baridiii...

Ni DED / DC /DAS / R C /RAS / RPC gani ndani ya nchi hii atakubali kuwa na chembe ya mpinzani eneo lake ? Ni nani atakubali mpinzani atangazwe na aapishwe ?

Ni ngumu sana mpinzani kushinda kwa Tanzania hii ya JPM kwa haya makubwa anayofanya :-

1. Reli ya SGR

2.Elimu bure

3. Mradi wa Stigler's George

4. Ununuzi wa ndege ATC

5. Uwajibikaji na adabu kwa watumishi wa umma

6. Mahakama ya mafisadi

7. Miradi ya umeme , maji , barabara , mazingira

8. Serikali kuhamia Dodoma

9. Ufufuaji wa viwanda nchini

10. Kupunguza safari za nje zisizo na tija

11. Kuzuia siasa ili watu wafanye kazi kwa nguvu

12. Viwanja vya ndege

13. Kufufua shirika la reli TRC

Kama unataka maendeleo unataka nini zaidi ?

Wapinzani watatoboaje kwenye game hili ?

Kwanini wasitumie mtaji walioupata ili kufanya kazi zingine ?

Kuna ulazima sana wao kuendelea kufanya siasa ?

Watafute miradi ya kufanya.

JPM atosha.
Maneno ya Jomo Kenyatta aliyo mwambia Nyerere yalikuwa sahihi kweli.
Alisema hivi, Mwalimu una ongoza RAIA ambao wengi wao ni maiti.
Jee ukifikiri kwa kina Mzee Jomo alikukosea?
 
Kwa usawa huu ni ndoto sana upinzani kushinda serikali za mitaa na hata tu uchaguzi wa udiwani , ubunge , Urais ! Ni kama tu hawatashinda tena. Washukuru awamu zilizopita za kudekezana mpaka watu wanaitwa Ikulu kunywa juice baridiii...

Ni DED / DC /DAS / R C /RAS / RPC gani ndani ya nchi hii atakubali kuwa na chembe ya mpinzani eneo lake ? Ni nani atakubali mpinzani atangazwe na aapishwe ?

Ni ngumu sana mpinzani kushinda kwa Tanzania hii ya JPM kwa haya makubwa anayofanya :-

1. Reli ya SGR

2.Elimu bure

3. Mradi wa Stigler's George

4. Ununuzi wa ndege ATC

5. Uwajibikaji na adabu kwa watumishi wa umma

6. Mahakama ya mafisadi

7. Miradi ya umeme , maji , barabara , mazingira

8. Serikali kuhamia Dodoma

9. Ufufuaji wa viwanda nchini

10. Kupunguza safari za nje zisizo na tija

11. Kuzuia siasa ili watu wafanye kazi kwa nguvu

12. Viwanja vya ndege

13. Kufufua shirika la reli TRC

Kama unataka maendeleo unataka nini zaidi ?

Wapinzani watatoboaje kwenye game hili ?

Kwanini wasitumie mtaji walioupata ili kufanya kazi zingine ?

Kuna ulazima sana wao kuendelea kufanya siasa ?

Watafute miradi ya kufanya.

JPM atosha.

Hayo maendeleo uliyoyataja umeyataja kama sehemu ya kuhalalisha dhuluma ya hao DC, RC nk kwamba hawatakubali kuwa na chembe ya mpinzani kwenye maeneo yao. Yaani kwa maneno marahisi hakutakuwa na uchaguzi bali uchafuzi.
 
Hakuna biashara inalipa kama siasa,hao wajinga wanadai et fulani anaweza kuacha siasa na akaishi maisha blah blah ni uzwazwa unawasumbua.
 
Back
Top Bottom