Kwanini viongozi wa upinzani akina Zitto, Mbatia, Mbowe nk hawahudhurii shughuli za kitaifa?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,750
139,546
Kwa sasa imekuwa ni vigumu sana kuwaona na hata kuwasikia viongozi wetu wakuu wa upinzani katika matukio muhimu.

Kwa mfano katika shughuli muhimu kama msiba wa balozi Kijazi au katika tukio la kuapishwa Katibu mkuu kiongozi mpya balozi Bashiru walipaswa kuwepo lakini hawajaonekana.

Ni Prof Lipumba pekee ndiye amewahi kuonekana kwenye sherehe za siku ya sheria lakini Mbatia, Zitto Kabwe, mzee Cheyo na Mbowe ni kitambo sasa hawaonekani.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa sasa imekuwa ni vigumu sana kuwaona na hata kuwasikia viongozi wetu wakuu wa upinzani katika matukio muhimu...
Yaani viongozi wa upinzani wakashiriki kwenye msiba wa viongozi wezi wa kura, huku wapiga kura wao wakiwa wameuwawa ili ccm wakae madarakani kwa shuruti?

Katika vitu nitawadharau hao viongozi wa upinzani, ni kushiriki kwenye shughuli za wezi wa kura. Kiongozi wa upinzani anayejitambua hawezi kushirikiana na wezi na wamwaga damu.
 
..washiriki ili wabezwe na kukejeliwa na Jiwe?

..hukumsikia Jiwe akimkejeli Prof.Lipumba kwamba amenenepa baada ya uchaguzi?
 
Kwa sasa imekuwa ni vigumu sana kuwaona na hata kuwasikia viongozi wetu wakuu wa upinzani katika matukio muhimu...
Bwashee naomba ufafanuzi wa maana ya shughulu za kitaifa.

Pia naomba kueleweshwa kama kuna utaratibu wa viongozi wa kitaifa kushiriki/kushirikishwa katika shughuli hizo za kitaifa.

Na kama kuna utaratibu, je ni utaratibu gani? Je utaratibu huo unafuatwa?
 
Yaani viongozi wa upinzani wakashiriki kwenye msiba wa viongozi wezi wa kura, huku wapiga kura wao wakiwa wameuwawa ili ccm wakae madarakani kwa shuruti? Katika vitu nitawadharau hao viongozi wa upinzani, ni kushiriki kwenye shughuli za wezi wa kura. Kiongozi wa upinzani anayejitambua hawezi kushirikiana na wezi na wamwaga damu.
Ruzuku mnapokea? Kama mnamachungu na wapiga kura waliowawa mbona mlijiunga na Suk?
 
Umewahi kuniona naunga mkono huo uhuni uitwao SUK? Weka ushahidi wa ruzuku kuchukuliwa, halafu ruzuku sio pesa ya ccm.
 
Unataka ushahidi gani juu ya ruzuku kuchuliwa?

Weka ushahidi namna ulivyoibiwa kura?

Video za bi kidude?
 
Kwa sasa imekuwa ni vigumu sana kuwaona na hata kuwasikia viongozi wetu wakuu wa upinzani katika matukio muhimu.

Kwa mfano katika shughuli muhimu kama msiba wa balozi Kijazi au katika tukio la kuapishwa Katibu mkuu kiongozi mpya balozi Bashiru walipaswa kuwepo lakini hawajaonekana.

Ni Prof Lipumba pekee ndiye amewahi kuonekana kwenye sherehe za siku ya sheria lakini Mbatia, Zitto Kabwe, mzee Cheyo na Mbowe ni kitambo sasa hawaonekani.

Maendeleo hayana vyama!
Mbona unamruka Mzee Rungwe?
 
Umelala nini?

Kwenye mitano tena amka MAENDELEO YANA CHAMA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom