Kwanini viongozi wa kitaifa hupenda kula Sikukuu DSM badala ya Dodoma yalipo makazi yao?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,873
Nauliza tu maana Dodoma wamebakia akina mzee Mgaya na mzee Ndugai wengine wote wametimkia Dar es salaam kula sikukuu ya Eid El Fitr.

Ni kwamba Dodoma ni padogo au bado ni mashambani hakufai kusherehekea sikukuu zenye amsha amsha?!!

Eid Mubarak!
 
Watatumia wapi fweza zao.
 
Nauliza tu maana Dodoma wamebakia akina mzee Mgaya na mzee Ndugai wengine wote wametimkia Dar es salaam kula sikukuu ya Eid El Fitr.

Ni kwamba Dodoma ni padogo au bado ni mashambani hakufai kusherehekea sikukuu zenye amsha amsha?!!

Eid Mubarak!
DSM ndiyo habari ya mjini. Dodoma hata baada ya miaka mia haitaifikia DSM!!!
 
Wengi pia familia zao zipo bado huku na walijiwekeza huku, Dodoma wapo kikazi tu. Imagine hata Ndugai familia yake ipo salasala nadhani pia alikuwa na nyumba Tabata kule aliishi zamani. So ni vijimambo tu.
 
Sikukuu unakula ukiwa Nyumban sio Kazini

Dodoma ni Kazini na Dar ni Nyumban

Kambarage alikuwa sikukuu anaila akiwa kwao Butiama

Mzee Mwinyi alikuwa anailia 'kwao' Msasani

Mkapa akiwa Kwao Lupaso

Jakaya alikuwa anailia kwao Msoga

Samia anailia kwao Znz japo sina hakika kama ni Makunduchi maana Makunduchi kule ni Platform iliyomleta kwny Bunge la Jamhuri ni asili ya Baba yake

Labda kwake ni Kijitoupele au Jia la Uzi (njia kuu ya kupitishia Nyaya za Umeme) au Kiembe samaki ( Seaview ya Znz)

Baada ya Mwendazake kumaliza Mwendo sasa hivi ofisi za Wizara za Dar es salaam zimeanza kufufuliwa mdogo mdogo wenyewe wamesibatiza jina 'Ofisi ndogo ya Wizara' wameanza ku beep kuja kufanyia visemina Uchwara Dar vya wiki mbili mbili ili angalau wawe karibu na Familia zao

Mzee alikuwa anapenda sana kushadadia yale mambo ya kukomoa komoa tu
 
Nauliza tu maana Dodoma wamebakia akina mzee Mgaya na mzee Ndugai wengine wote wametimkia Dar es salaam kula sikukuu ya Eid El Fitr.

Ni kwamba Dodoma ni padogo au bado ni mashambani hakufai kusherehekea sikukuu zenye amsha amsha?!!

Eid Mubarak!
Ngoja wale wenye uzi 'DAR ITAPAUKA BAADA YA SERIKALI KUHAMIA DODOMA" waje watie neno hapa
 
Back
Top Bottom