Kwanini viongozi wa dini husoma sala kwenye karatasi wanapokaribishwa kufungua shughuli?

Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
1,111
2,377
Nimekuwa naona mara nyingi kunapokuwa na ziara ya rais wale viongozi wa dini wanaokaribishwa kufungua shughuli kwa sala/swala wanakuwa na vikaratasi wanakuwa wanavisoma, najua ntaambiwa eti ili wasikosee wakatamka visivyo, mara protokali n.k,

Hivi kwenye sala/swala kiongozi anaweza kuteleza nini hasa? Mbona kanisani/msikitini hawasomi na hawakosei? Au kuna sababu gani hasa logically?

Binafsi huwa naona yale ni maigizo tu hakuna sala/swala pale.

Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu, kuongea mbele ya wananchi wenzio ni rahisi kuliko kuongea mbele ya Rais, sikumbuki vizuri ila kuna siku ilitokea kiongozi wa dini kujiumauma kama kasahau cha kuongea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Askofu, shehe wa mkoa anakosa exposure ya kusali/kuswali kweli?
Tatizo wanachanganya maombi na siasa, kuna haja gani ya kutaja majina ya viongozi na misifa kibao kwenye sala/swala?
Maombi kwa Mungu tunasoma kama risala kwa mgeni rasmi kweli???
 
Back
Top Bottom