Kwanini viongozi wa CHADEMA hawajaenda kuona wahanga?

Slaa na baadhi ya wenzake walikuwa waje Dar kwa ndege kuweza kushiriki kikamilifu na wananchi, walikuja kuchemsha baada ya uwanja wa ndege kufungwa kwa muda, ikawalazimu kuja kwa magari
"Ikawalazimu kuja kwa magari"?

Kiongozi wa chama cha upinzani kinachosema Serikali ya CCM inafuja hela "ikawalazimu kuja kwa gari" kutoka Dodoma? Alikuwa anasubiri ndege?

Hujui hayo ni matusi kwa Mtanzania ambae hajawahi hata kupanda basi, achilia ndege?

So outta touch.
 
Jesuit,

Sifa moja ya kuwa Jesuit ni usomi wa hali ya juu na hivyo utafiti wa hali ya juu na bila jazba. Post yako inatia mashaka hadi kwenye matumizi ya jina hilo, kama unafahamu historia yake. Tuache hayo:

i) Kauli yako inatisha"...... Makelele juu ya watu watatu waliojiua. Binadamu anashitaji kuheshimiwa na heshima kwa utu na ubinadamu haina gharama. Mtu yeyote makini stegemei atatoa kauli ya aina hiyo, Sembuse ungelitoa taarifa ya utafiti ningelielewa. Ushabiki wa aina haina unaendelea kuporomosha maadili na "core values za Taifa letu. Sikutaka kuingia jamvini lakini kauli ya namna hii imenilazimisha.

ii) Iwapo tumeenda Gongo la Mboto na kwingine kote kulikohusika, basi ni ishara ya dhahiri ya Taifa linakoelekea. Kugeuza misiba kwa manufaa ya kisiasa. Siamini si tu Mwana Chadema, bali mwana CCM wa kweli au wa chama kingine chochote anayejua na kujali thamani ya binadamu kama ataweka hilo kama lengo, japo katika hali halisi si rahisi kutenganisha vitu hivi. Kofia ya mtu huwezi kuivua artificially.Lakini kama kuna anayeweka kama lengo la msingi, basi huyo hana ubinadamu kabisa.

iii) "..Hamna FAIDA ya Kisiasa....huu ni upofo, licha ya upotoshaji wa hali ya juu.Chadema haiangalii Faida ya kisiasa kwa kupitia uhai wa binadamu. Faida ya kisiasa tunaipata na tutaipata kwa kuwa karibu na wananchi wetu, kwa kusimamia masuala yanayowahusu, na kamwe si kupigwa picha kwenye maeneo ya msiba. Kama hiyo inatokea ni kwa vile tu, kiongozi hafanyi kazi kwa maficho au chini ya meza. Lakini kamwe si lengo la msingi (primary objective).

iv) Kama ni uchungu ebu tutafakari:
a) Matukio yametokea, ndugu zetu wamepoteza maisha.Serikali imeonyesha vipi uchungu wake, aunhata hiyo Gaida ya kisiasa basi.Rais na alichoita Baraza la Usalama (ambalo kimsingi sina hakika kama ni Baraza la Usalama kweli) wote walilalia na kuendelea kulalia vitanda vyao hata baada ya kuwa wa mwanzo kujulishwa
b)Rais na vyombo vyake vya dola waliendelea na maisha kama kawaida.TBC ambayo ni chombo kinachoendeshwa kwa kodi ya Watanzania imeendelea na program zake kama desturi ukiachia vijimistari na Taarifa ya Habari. Kesho yake Taifa limepoteza nguvu kazi yake, TBC iliendelea na program zake ikiwa ni pamoja na michezo,tamthilia. Sijui kama Taifa tunaonyesha na tulionyeshaje uchungu wetu? Vyombo vya habari na hasa Electronic media ni viunganishi muhimu sana katika mazingira ya maafa. Lakini wapi. Mambo yalikuwa business as usual.
c) Msiba mkubwa kama huu, nimeshuhudia familia iliyopoteza mama na watoto wake wawili, malaika wa Mungu (wadogo sana) yaani historia yao imefutwa yote kwa ghafla-Mungu awatimie moyo wa uvumilivu mkubwa Baba na ndugu waliobaki. Kama Taifa linglitambua angalau basi hata bendera tu zingepepea nusu mlingoti. Wapi Bwana Business as usual, vikao viliendelea na sitashangaa kama vilikuwa vikao vya posho kwa hela hiyo hiyo ya Rambi Rambi. Ndugu yangu ushabiki hausaidii tunauchungu, na ka ni kusemana tunayo machungu mengi sana.
d) Hatimaye nimestuka sana kusikia Rais ambaye ni Baba wa Familia anaruka ndege kwenda nje "kusuluhisha" kwa wenzake wakati kwake kuna msiba mkubwa, tena uliosababishwa siyo na "Force Majour", kama kimbunga, tetemeko la ardhi ambayo ni matendo ya Mwenyezi Mungu na Kazi ya Mwenyezi Mungu haikosolewi. Lakini kwa uzembe wa Serikali!!!!Inatisha sana.Ushabiki pembeni fikiria umefiwa, na wewe Baba yako mzazi unayeishi naye nyumba moja anaondoka anakuacha kabla hata miili haijaingia kaburini. Ubinadamu tu, hatuhitaji kisomo, wala siasa kuona priorities ziko wapi. Kwako kunaungua moto wewe unasuluhisha kwa watu, na kama unasema Arusha walijiua basi subiri moto, wanaoleta vurugu nchini ni mashabiki kama wewe wasiojua kuchagua maneno katika mazingira waliyomo.

Sasa,Chadema wafanye nini:-

a) Mhe.Tundu Lissu (Chief Whip wa Chadema), Kambi Rasmi inayotambuliwa na Kanuni za Bunge taarifa ilipotoka tu, aliitisha Kamati yake ya Kambi ya Upinzani, na badala ya kulala walipeleka Taarifa kwa wahusika wote kuwa asubuhi, kwa vile Bunge linakutana basi waombe kwa mujibu waanuni ya 47 inyoruhusu Bunge kujadili Jambo la dharura halisi ma lililotokea punde. Kwa vile Asubuhi Waziri Mkuu alitoa taarifa ya awali ilikuwa halali na wajibu wawakilishi wa wananchi walijadili jambo hilo kwa kina. Nafasi haikutotolewa. Badala yake Spika alilidanganya Taifa kwa kusema anaahirisha Bunge ili wabunge wajadili jambo hilo katika kamati za Bunge na akataja kumbi mbalimbali ambapo kamati zitakutana. Ukweli ni kuwa ukiacha Kamati ya ulinzi na Usalama Kamati zingine zote ziliendelea na kupanga shughuli za kawaida za Kamati. Huu ndio uongozi wa Taifa letu. Asubuhi siku iliyofuata, Chief Whip wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu kwa kutekelrza wajibu wake wa kikanuni akaomba Bunge lijadili tukio hilo kwa mujibu wa Kanuni ya 47. Watanzania takriban wote waliokuwa na TV na Radio na pale ambako kulikuwa na umemr walishuhudia jeuri, kebehi na kutokujali ubinadamu wa Spika. Spika alikataa si jambo la dharura na halisi. Naamini Watanzania hawahitaji kuelezwa tafsiri ya kauli hiyo ya Mhe.Spika.
b) Baada ya kuzuiliwa kujadili tukio hilo katika chombo kinachoendeshwa kwa fedha nyingi kodi za Watanzania, Mhe. Lissu alitoa Kauli kwa niasba ya Kambi ya Upinzani ambayo yote inaundwa na Chadema kwa mujibu wa Kanuni za Bunge,na pia Mhe Selasini, Waziri Kivuli wa Ulinzi na usalama naye akatoa Tamko kama Waziri mwenye dhamana na wizara hiyo, akilaani tukio hilo,na hasa uzembe wa Serikali na kuwataka wahusika wajiuzulu. Hili ni jukumu la Kambi Rasmi, na ni Kauli ya Chadema
c) Leo Kaitibu Mkuu ameshiriki katika matikio kadhaa amenukuliwa na vyombo vya habari au la haitusumbui sana, kwa kuwa siyo lengo letu.

Kutokana na hayo yote, Jusuit, naamini nimeeleweka.

Wananchi, nimeeleza kwa kirefu ili tuwaweke kwenye picha halisi wale wote waliopotoshwa au hawakuwa na picha ya mlolongo mzima wafanye uamuzi wao wanapenda ushabiki kwa sababu ya ushabiki hatuwazuii, wanaopenda kutafuta ukweli wanaweza kuupata na wenginw wanaweza kuongeza pale ambapo sikufikisha ukweli katika hali yake halisi.

Nawashukluru sana wana Jamvi, ninarudia kutoa pole za dhati kwa wale wote waliathirika kwa namna moja au nyingine, waliopoteza ndyugu, amba sasa hivi wako safarini kwenda kwenye maziko katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, na pia ambao wamepoteza nyumba, na mali zao mbalimbali. Mwenyezi Mungu awatie nguvu na faraja. Ushabiki hata kabla miili ya ndugu zetu haijahifadhiwa imenistua sana na bado najiuliza ni Taifa la aina gani tumefikia!

Mungu anisamehe.

Ni ajabu viongozi wa CDM wanapiga makelele juu ya watu watatu waliojiua kwa makusudi kule Arusha, na hawaonyeshi concern yeyote juu ya watu zaidi ya 20 walikufa kwa ajali Gongolamboto! Ukweli ni kuwa wanaona hamna FAIDA ya kisiasa ndio maama wameamua KUPOTEZEA!
 
Dr slaa,mimi nimeshindwa hata kushangaa jk kwenda kusuluhisha nje wakati ndani hali ni tete,ni dhahiri hili ni anguko lake,huyu amekosa uhalali wa kuongoza maana ameshindwa hata kuonyesha utu na ubinadamu kwa watu wake
 
Kutokana na hayo yote, Jusuit, naamini nimeeleweka.

Wananchi, nimeeleza kwa kirefu ili tuwaweke kwenye picha halisi wale wote waliopotoshwa au hawakuwa na picha ya mlolongo mzima wafanye uamuzi wao wanapenda ushabiki kwa sababu ya ushabiki hatuwazuii, wanaopenda kutafuta ukweli wanaweza kuupata na wenginw wanaweza kuongeza pale ambapo sikufikisha ukweli katika hali yake halisi.

Nawashukluru sana wana Jamvi, ninarudia kutoa pole za dhati kwa wale wote waliathirika kwa namna moja au nyingine, waliopoteza ndyugu, amba sasa hivi wako safarini kwenda kwenye maziko katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, na pia ambao wamepoteza nyumba, na mali zao mbalimbali. Mwenyezi Mungu awatie nguvu na faraja. Ushabiki hata kabla miili ya ndugu zetu haijahifadhiwa imenistua sana na bado najiuliza ni Taifa la aina gani tumefikia!

Mungu anisamehe.

Asante kwa taarifa ya kina Mkuu. Asante kwa mwongozo. Poleni watanzania.
 
d) Hatimaye nimestuka sana kusikia Rais ambaye ni Baba wa Familia anaruka ndege kwenda nje "kusuluhisha" kwa wenzake wakati kwake kuna msiba mkubwa, tena uliosababishwa siyo na "Force Majour", kama kimbunga, tetemeko la ardhi ambayo ni matendo ya Mwenyezi Mungu na Kazi ya Mwenyezi Mungu haikosolewi. Lakini kwa uzembe wa Serikali!!!!Inatisha sana.Ushabiki pembeni fikiria umefiwa, na wewe Baba yako mzazi unayeishi naye nyumba moja anaondoka anakuacha kabla hata miili haijaingia kaburini. Ubinadamu tu, hatuhitaji kisomo, wala siasa kuona priorities ziko wapi. Kwako kunaungua moto wewe unasuluhisha kwa watu, na kama unasema Arusha walijiua basi subiri moto, wanaoleta vurugu nchini ni mashabiki kama wewe wasiojua kuchagua maneno katika mazingira waliyomo.
Sasa Mheshimiwa, hicho kitu ukija kukilalamikia hapa ni Watanzania wangapi watakusoma humu?

Ndo haya mambo ya kuwa out of touch. Toa public condemnation ya safari ya Kikwete kwenda Mauritania wakati wa msiba wa Taifa. Sio kuja kuhojiana na kusomwa na watu kumi na tatu kwenye mtandao.

Kuhusu CHADEMA wamefanya nini, unaeleza habari za Lissu, Chief Whip, na Selasini, Mbunge wa kamati, hatutaki kusikia habari za Chief Whip, whatever the heck that means, tunataka kusikia statement ya the head honcho in opposition, ambae ni wewe!

Ni mara ngapi CHADEMA mnakataa jumbe za Rais zinazoletwa na wasaidizi, mnataka matamko yake mwenyewe? Basi onyesha mfano.
 
Dr slaa,mimi nimeshindwa hata kushangaa jk kwenda kusuluhisha nje wakati ndani hali ni tete,ni dhahiri hili ni anguko lake,huyu amekosa uhalali wa kuongoza maana ameshindwa hata kuonyesha utu na ubinadamu kwa watu wake

Problem of priorities. Such a leader normally: "majors on minor issues and minors on major issues".
 
Sasa Mheshimiwa, hicho kitu ukija kukilalamikia hapa ni Watanzania wangapi watakusoma humu?

Ndo haya mambo ya kuwa out of touch. Toa public condemnation ya safari ya Kikwete kwenda Mauritania wakati wa msiba wa Taifa. Sio kuja kuhojiana na kusomwa na watu kumi na tatu kwenye mtandao.

Kuhusu CHADEMA wamefanya nini, unaeleza habari za Lissu, Chief Whip, na Selasini, Mbunge wa kamati, hatutaki kusikia habari za Chief Whip, whatever the heck that means, tunataka kusikia statement ya the head honcho in opposition, ambae ni wewe!

Ni mara ngapi CHADEMA mnakataa jumbe za Rais zinazoletwa na wasaidizi, mnataka matamko yake mwenyewe? Basi onyesha mfano.

Safari ya Mauritania imefanyika leo ... Dr. Slaa amesema amestuka kusikia hivyo na wewe unataka tamko lake haraka haraka. Mimi kwanza nafikiri CDM wanafanya busara kutafakari yote kabla ya kutoa matamko. Maisha si matamko tu. Watanzania wanauelewa wa kutosha, wanaweza kuchuja pumba na mchele.

Pili, Dr Slaa si mwenyekiti wa chama. Tuache ushabiki wa uchaguzi. Chama kina uongozi wake na taratibu zake. Najua ana nafasi yake kubwa tu kama Katibu Mkuu; lakini ni vyema tukaona umuhimu wa uamuzi wa pamoja la sivyo tutaanza kusikia matamko kama ya kina Makamba hapa ambayo ni ya kukurupuka tu.
 
Sembuse ungelitoa taarifa ya utafiti ningelielewa. .

sijui kama huwa unafanya makusudi ila huwa unalitumia neno hili kuwa intimidate watu wasieleze mawazo yao hasa yanayopingana na wewe, ingelikuwa wewe unafanya utafiti kabla haujasema au kuandika kitu ningekuelewa sana unapodai utafiti lakini ni kinyume kabisa.
 
Sasa Mheshimiwa, hicho kitu ukija kukilalamikia hapa ni Watanzania wangapi watakusoma humu?

Hivi nyie watu huwa manashirikisha ubongo katika hayo mnayoyasema. Umeelewa Dr Slaa alikuwa akimjibu nani? Umeambiwa alikuwa akijibu kwa ajili ya watz au alikuwa akimuelewesha huyo anayejiita jesuit wakati hashirikishi ubongo? tatizo lenu makada wa mafisadi mlishakuwa brainwashed kiasi kwamba hamko tayari kufungua macho. Iko siku kitaeleweka tu!
 
sijui kama huwa unafanya makusudi ila huwa unalitumia neno hili kuwa intimidate watu wasieleze mawazo yao hasa yanayopingana na wewe, ingelikuwa wewe unafanya utafiti kabla haujasema au kuandika kitu ningekuelewa sana unapodai utafiti lakini ni kinyume kabisa.

Bado narudi kule kule, nikusaidie mkuu, one premise does not make a valid conclusion. Yaani umechukuwa mstari mmoja ndo umepandia hapohapo na kuacha maana nzima ya mada. Najua kweli cc wabongo ni wavivu sana wa kujisomea, nadhani umeona hiyo post ta dr Slaa ni ndefu ukawa mvivu wa kuisoma na kuamua kuchukuwa mstari tu?

Kazi tunayo wabongo!
 
sijui kama huwa unafanya makusudi ila huwa unalitumia neno hili kuwa intimidate watu wasieleze mawazo yao hasa yanayopingana na wewe, ingelikuwa wewe unafanya utafiti kabla haujasema au kuandika kitu ningekuelewa sana unapodai utafiti lakini ni kinyume kabisa.

The Following User Say Thank You to Mjepu For This Useless Post:

LAT (Today),
 
Chadema na vyama vingine wameshiriki kama kawaida,wala suala hili halikuwa la kampeni wala kutafuta umaarufu.
kumbuka serikali iliyopo madarakani ndio ilitakiwa kuwa mbele kwa hali na mali sio kisiasa.kwani unajua waliokufa ni wanachama wa vyama gani?
try to find another weak point to supress but not on this issue
narudia tena kusema jambo hili halikuwa siasa..ni janga la kitaifa lililopaswa kuangaliwa na macho yote!
 
Siasa iko wapi hapa ina maana Lipumba,Mtatiro,Mbatia na wapinzani wengine kuonyesha ushikiano ni siasa. Acha ushabiki kwa hapa cdm wamedunda

Smartboy nadhani Maxence Melo amekujibu vizuri hapo juu dhamira nzuri ya viongozi wa CHADEMA kushiriki kwenye maafa haya yanayosababishwa kwa makusudi na serikali ya CCM. Au kuna la zaidi ulilohitaji? Zaidi ya hapo wewe ndio unataka kuleta ushabiki na siasa!!
 
Mkuu,

Kama mfuasi wa kweli basi ungekuwa na taarifa zaidi ya sisi wengine hata si wafuasi bali wafuatiliaji wa karibu wa wanasiasa wetu.

Slaa ametoka muda si mrefu Amana Hospital, wakati mabomu yanalipuka wengi wao (pamoja na Slaa) walikuwa Dodoma, walitoa tamko lao hata kabla serikali na JWTZ hawajatoa kauli.

Baada ya tukio (usiku) kesho yake Slaa na baadhi ya wenzake walikuwa waje Dar kwa ndege kuweza kushiriki kikamilifu na wananchi, walikuja kuchemsha baada ya uwanja wa ndege kufungwa kwa muda, ikawalazimu kuja kwa magari (kumbuka wengine wanalazimika kubaki bungeni maana ndio lilikuwa linaahirishwa).

Jana Slaa alitakiwa kufika Uwanja wa Uhuru kuwaona wahanga (sijui kama alifika au la), na ilikuwa iwe saa 5 asubuhi, kilichotokea (inadaiwa) ni kuwa wahanga waliondolewa eneo la uwanja huo saa 1 kabla!

Sasa, wewe kama 'mfuasi' wa kweli habari hizi huna???

Asante Maxence kwa maelezo mazuri na kuwa mstari wa mbele kusimamia ukweli.Namshukuru pia mtoa mada kwani amesaidia kupata hisia za watu mbalimbali za pande zote alkini pia amesaidia kufikisha ujumbe kwa wengine waliokuwa hawafahamu kama CHADEMA tumeshiriki katika janga hili kwa hali na mali.Wabunge wote wa CHADEMA tumechangia fedha,chama makao makuu kimetoa fedha na vile vile baadhi ya wabunge na viongozi wetu wameshiriki. Jamani hakuna ambaye hajaguswa na tukio la Gongo la Mboto na hakuna chama kischotaka kushiriki kwenye hili.

Thank You once again both of You,Maxence and Smartboy. Nawashukuru na wote pia mlioonyesha mnajali katika hili.

Tupo pamoja
Aluta Continua.

Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira.
 
maafa haya yanayosababishwa kwa makusudi na serikali ya CCM. !!

kwa kushindwa kumdhibiti kiongozi mmoja aliyewahi kujitangaza hadharani kuwa ana vijana wake jeshini na vyombo vingine vya usalama vinaripoti kwake tena akaapa kuwa nchi haitatawalika, nadhani sasa ameanza kuwatumia vijana wake na nchi kwa hali hii haitawaliki.
 
Mimi ni mfuasi wa CDM lakini nimejaribu kufutilia vyombo vya habari sijaona kiongozi wa CDM maeneo ambayo wahanga wa mabomu wamekusanyika iwe hospitalini au viwanjani. Au labda kuna ambaye amewaona?

Imezoeleka hapa JF watu wanajadili weakness za CCM tu, naomba kwa moyo mkujufu kabisa mtu mwenye sababu atueleza ushabiki ukae kando. Na kama kuna wabunge wa cdm humu watuambie vinginevyo cdm imeonyesha picha mbaya.

Nawasilisha

dogo we si mfuasi wa cdm unaonekana kama ni kada vile, kwasababu umeng`ang`ania ushabiki wakati umeshaelezwa, una kichwa kigumu kuelewa sijui mwalimu wako alikuwa anafanyaje, kwani MAXENCE MELO amekuelaza vizuri sana lakini huelewi. jaribu kuwa karibu na "media" za maana na si vyombo vya habari vya ccm kwani haviwezi kuweka habari za chadema.
 
kwa kushindwa kumdhibiti kiongozi mmoja aliyewahi kujitangaza hadharani kuwa ana vijana wake jeshini na vyombo vingine vya usalama vinaripoti kwake tena akaapa kuwa nchi haitatawalika, nadhani sasa ameanza kuwatumia vijana wake na nchi kwa hali hii haitawaliki.

NADHANI MJEPU huna HOJA hapa.
 
Mimi ni mfuasi wa CDM lakini nimejaribu kufutilia vyombo vya habari sijaona kiongozi wa CDM maeneo ambayo wahanga wa mabomu wamekusanyika iwe hospitalini au viwanjani. Au labda kuna ambaye amewaona?

Imezoeleka hapa JF watu wanajadili weakness za CCM tu, naomba kwa moyo mkujufu kabisa mtu mwenye sababu atueleza ushabiki ukae kando. Na kama kuna wabunge wa cdm humu watuambie vinginevyo cdm imeonyesha picha mbaya.

Nawasilisha

ulitegemea uwaone TBC, mbona hata huko Arusha CCM hawakuonekana kuwapa pole wahanga
 
Kama kila chama kikimbilia kuonekana kwenye TV nani atakayebaki akiwahudumia Wahanga?Siasa kwenye majanga kama haya ni ashirio la ukosefu wa utu na kujali thamani ya Utu,Ni dalili ya umimi,ubinafsi na kutokujal lwa hali ya juu kabisa ni sawa na kusema yatokee majanga ili umaarufu wetu upande.CDM,CCM,CUF kwepeni mtego huu.
 
Back
Top Bottom