Kwanini viongozi wa CCM hawakuvaa kijani yao katika mkutano na Magufuli jana?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
9,335
13,293
upload_2016-4-22_9-47-26.png


Nilishangaa kutokuona nguo za kijani katika mkutano wa jana uliojumuisha wenyeviti wa mikoa na wilaya wa CCM ambao Rais Magufuli aliutumia kuwashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.

Tumezoeya kuona wana CCM wakiwa katika mavazi ya kijani hata katika shughuli za kawaida za kiserikali, je huu ni mwelekeo mpya wa CCM ijayo?!
 
Wengi wa mamluki bado hawajajua hatma yao ndani ya CCM baada ya JPM kukabidhiwa mikoba ya uongozi wa chama hapo mapema mwakani. Na kwa ujumla JPM hatabiriki kwa wanaomfatilia hivyo hawakuwa na uhakika na agenda rasmi ya mkutano ule na hivyo waliogopa,
e032b2d625bc01b8515ef2969e1c83fd.jpg
labda kutumbuliwa wakati wamevaa rangi ya chama chao hadharani..... Anyway ni mtazamo wangu tu.
 
Wengi wa mamluki bado hawajajua hatma yao ndani ya CCM baada ya JPM kukabidhiwa mikoba ya uongozi wa chama hapo mapema mwakani. Na kwa ujumla JPM hatabiriki kwa wanaomfatilia hivyo hawakuwa na uhakika na agenda rasmi ya mkutano ule na hivyo waliogopa,
e032b2d625bc01b8515ef2969e1c83fd.jpg
labda kutumbuliwa wakati wamevaa rangi ya chama chao hadharani..... Anyway ni mtazamo wangu tu.
Hapa wamempaka mafuta kwa mgongo wa chupa!!
 
Hata mimi nimeshangaa sana. Yaani wameamua kuwa kama Nyerere!? Maana inasemekana Nyerere hakuwahi vaa haya makijani na njano za ccm. Lakini nadhani ilikuwa ni sharti lililowekwa na Pombe mwenyewe maana hata mwenyewe hakuvaa minguo ya ccm
 
Hwakupewa pesa za kushonesha mashati nasikia kutano zote zilizopita walikuwa wakipewa pesa kwa ajili ya mavazi kabla ya mkutano...Sasa kwa Magu wataisoma namba wenyewe...
 
Mimi jana walinifurahisha sana, kiukweli kabisa toka moyoni huwa nachafukwa na roho nikiona yale manguo ya ccm kwenye majengo ya umma, mikutano ya kiserikali wakati uchaguzi ulishapita sa hivi wote tunajenga nchi bila kujali vyama vyetu. Ulaya huwezi kuta watu wamevaa manguo ya vyama.
 
aliwaita kama rais na sio kama kiongozi wa chama na isitoshe ulipofanyikia mkutano ni nyumbani kwa watanzania wote hapana dini kabila wala chama
 
Ikulu ni ya serikali ya watu wote wa vyama vyote.
Ndio maana mh Rais yupo pale kwa ajiri ya Taifa haikuwa busara wale wenyeviti kuvaa nguo zenye mlengo wa kisiasa.,Ikulu.
 
Kwani ni lazima kuvaa muda wote?
Wewe unajifanya mgeni nchi hii!! Lini uliwahi kuona wana - CCM wakiwa katika mkusanyiko wo wote bila kujali eneo au aina ya sherehe iwe ya kiserikali au kiraia hawajavaa sare zao?
 
mwenye nchi alishasema hataki mambo ya ....machama chama.....ole wanu mje na manguo yenu ya rangi rangi mtamkoma.. Je wajua watanzana walikuwa wanapenda upinzani wa vyama kuliko mgombea wa chama? ....je wajua kwa sasa watanzania wanampenda raisi kuliko wanavyopenda vyama vyao? chukua hiyo......
 
Back
Top Bottom