Kwanini viongozi na wafuasi wa CHADEMA wanashindwa kukiri kuwa wamepoteza Kata ya Tanga Songea?

Mtoa mada ni muongo na anataka kutuaminisha kuwa huyu alipitishwa kugombea akiwa sio Mwana CCM?

Pili mtajwa hakugombea Udiwani hivyo sio diwani wa kata hyo.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimefuatilia mijadala juu ya matokeo ya Udiwani katika kata 20 na Ubunge wa Dimani. Nilichojifunza katika mijadala hiyo ni kwamba, CHADEMA na UKAWA wanakufa na Tai Shingoni. Wanajifariji huku wanateketea. Wanaumia ila wanajifanya wana tabasamu. Wanapigwa ila wanajifanya wakakamavu.

Mtakumbuka kuwa kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, Kata ya Tanga iliyopo Manispaa ya Songea ilichukuliwa na Mussa Ndomba wa CHADEMA. Hata hivyo, baada ya kuona kuwa CHADEMA hakipo kwa maslahi ya Watanzania, Ndomba aliamua kujiunga na CCM na hivyo kupoteza Udiwani. Mtakumbuka kuwa Mussa Ndomba amekabidhiwa kadi ya CCM tarehe 7 Januari 2017 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipofanya ziara mkoani Ruvuma.

Kutokana na uwezo wa Mussa Ndomba, CCM walimpa nafasi ya kugombea Udiwani kwenye uchaguzi wa Marudio wa Januari 22 akiwa na muda wa siku 15 tu ndani ya CCM. Hata hivyo, Wana Tanga walimwamini na wakampa kura za kishindo kuliko zile alizopata akiwa CHADEMA Oktoba 2015.

Nawashangaa sana UKAWA. Pamoja na CCM kutwaa kata hiyo ya Tanga, tumewapora pia kata nyingine kule Mkoa wa Tanga ambayo ilikuwa inashikiliwa na chama mwanachama wa UKAWA, CUF. Kwa hali hiyo, CCM tumeweza kutetea viti vyetu 17 na kuwapora UKAWA kata 2 na hivyo kutufanya kuibuka kidedea kwa kata 19.

Hivi CHADEMA wanajua kweli hesabu? Au wanafanya makusudi ili kuficha aibu? Kwa nini hawataki kukiri kuwa CCM ni baba lao? Kwa nini huyu UKAWA anakosa adabu kwa mzazi wake?

Endeleeni kujifariji. Tukutane 2020.
View attachment 463601




Yani umefafanua vizuri mnooooo .
 
Mkuu, kwa nini sasa mnaficha kusema bayana kuwa CHADEMA mmepoteza Kata hiyo? Mbona hili lipo bayana!
MUSA NDOMBA alikwishas hutumiwa na kubainika ni mamluki ndani ya CDM toka kinyangiro cha Ubunge wa ndani ya CDM ndio maana kapigwa chini nafasi yake akashinda Joseph Fuime. Musa Ndomba alikihujumu Chama kwa kupiga kampeni cha chini kwa chini kwa watu wa Tanga kwamba mbunge wamchague Leonidas Gama na si Fuime ili yeye aje agombee 2020. Musa Ndomba alitaka kujitoa kugombea Udiwani 2015 ili Mgombea wa CCM apite bila kupingwa, wazee wa CDM wakambembekleza akakubali kuendelea na kampeni kwa kukubaliana yeye agombee 2020. Musa Ndomba alihama CDM mara baada ya kamati ya CDM kanda kumrudishia Uanachama kamanda Fuime pamoja na wenzake na Fuime kutangaza kugombea Ubunge tena 2020. Mbaya zaidi kwa Musa ni rufaa yake kugonga mwamba kwenye mkutano wa viongozi kitaifa Salum Mwalimu na Lowasa walipokuja Songea, na wao kuridhia akina Fuime na wenzake kurejeshewa uanachama. Kumbuka mara baada ya kuondoka akina Salum Mwalim ndipo Musa Ndomba alipoamua kujivua uanachama.
 
Lizaboni si mnapendwa na kuaminiwa na wananchi !!?? Tume huru basi ?! Utapambanaaje na mtu dhaifu huku na tume mmeikalia ?! Hebu iruhusiwe na vyombo vya dola kuwa fair
Tume huru haina faida! Mfumo uliopo unatosha. Kwani Uchaguzi huru ni lazima Wapinzani washinde! Baghdad we!!
 
Back
Top Bottom