Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimefuatilia mijadala juu ya matokeo ya Udiwani katika kata 20 na Ubunge wa Dimani. Nilichojifunza katika mijadala hiyo ni kwamba, CHADEMA na UKAWA wanakufa na Tai Shingoni. Wanajifariji huku wanateketea. Wanaumia ila wanajifanya wana tabasamu. Wanapigwa ila wanajifanya wakakamavu.
Mtakumbuka kuwa kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, Kata ya Tanga iliyopo Manispaa ya Songea ilichukuliwa na Mussa Ndomba wa CHADEMA. Hata hivyo, baada ya kuona kuwa CHADEMA hakipo kwa maslahi ya Watanzania, Ndomba aliamua kujiunga na CCM na hivyo kupoteza Udiwani. Mtakumbuka kuwa Mussa Ndomba amekabidhiwa kadi ya CCM tarehe 7 Januari 2017 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipofanya ziara mkoani Ruvuma.
Kutokana na uwezo wa Mussa Ndomba, CCM walimpa nafasi ya kugombea Udiwani kwenye uchaguzi wa Marudio wa Januari 22 akiwa na muda wa siku 15 tu ndani ya CCM. Hata hivyo, Wana Tanga walimwamini na wakampa kura za kishindo kuliko zile alizopata akiwa CHADEMA Oktoba 2015.
Nawashangaa sana UKAWA. Pamoja na CCM kutwaa kata hiyo ya Tanga, tumewapora pia kata nyingine kule Mkoa wa Tanga ambayo ilikuwa inashikiliwa na chama mwanachama wa UKAWA, CUF. Kwa hali hiyo, CCM tumeweza kutetea viti vyetu 17 na kuwapora UKAWA kata 2 na hivyo kutufanya kuibuka kidedea kwa kata 19.
Hivi CHADEMA wanajua kweli hesabu? Au wanafanya makusudi ili kuficha aibu? Kwa nini hawataki kukiri kuwa CCM ni baba lao? Kwa nini huyu UKAWA anakosa adabu kwa mzazi wake?
Endeleeni kujifariji. Tukutane 2020.