SoC01 Kwanini vijana wengi wana uoga wa kuongea mbele ya watu (public speaking)?

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 29, 2021
81
158
“According to most studies, people’s number one fear is Public speaking. Number two is death. Death is number two. Does that sound right? This means to the average person, if you go to a funeral, you’re better off in the casket than delivering the eulogy.”- Jerry Seinfeld, Comedian.

“ Kutokana na tafiti nyingi zilizofanywa, hofu ya kuzungumza mbele za watu ndio hofu kubwa kuliko hofu zote duniani. Hofu namba mbili ni hofu ya kifo. Au siyo? Hi ina maana kwa mtu wa kawaida, aliyeko msibani, anaona ni bora awe mtu aliye kwenye jeneza kuliko yule mtu anayetakiwa kusoma wasifu wa marehemu!”- Jerry Seinfeld, Mchekeshaji.

Unaweza ukashangazwa na hayo yaliyosemwa na muda mwingine ukakataa kabisa kuyaamini, lakini haya ni mambo ya ukweli ambayo yanatokea na tunayaona kila siku. Nikiwa shule nakumbuka wenzangu walikuwa wako radhi watoroke katika kusanyiko (assembly) ili mradi tu wasije wakaitwa mbele kutoa hotuba (Morning speech) mbele ya watu. Walikuwa wanatoroka ihali wakijua watapata adhabu baadae. Kwahiyo walikuwa wako radhi kupata adhabu kuliko kusimama mbele na kutoa mawazo yao mbele ya wanafunzi wenzao.

Kuna baadhi hushindwa kabisa kuongea wakifika mbele za watu, mfano mzuri ni rafiki yangu mmoja niliyesoma nae kidato cha Tano , yeye alilazimishwa kusimama mbele ya darasa na kuzungumza nasi kuhusu jinsi alivyoelewa somo ambalo mwalimu alilifundisha, yeye hakuweza hata kutuangalia , kwa jinsi alivyokuwa na hofu alianza kulia pale mbele.
Lakini kilichonisikitisha zaidi ni kile mwalimu alichokifanya, nakumbuka mwalimu alimpiga sana huyo rafiki yangu pamoja na kusema maneno mabaya na yenye kejeli na kumdhihaki, kwasababu anashangazwa kwa mtu mzima kama yeye ni aibu kushindwa kuongea mbele za watu.

Kwanza napenda kusema kuwa kushindwa kuongea mbele za watu hakumaanishi kuwa wewe ni mjinga au huna akili au haufai. Na sio kitu cha kumfanya umcheke au kumdharau mtu kama jinsi mwalimu wangu alivyo mfanyia rafiki yangu. Kuwa na hofu hiyo ni kitu cha kawaida, na hata wale waliobobea kwenye sanaa hii ya uneni huwa wanakuwa na hofu kabla ya kusimama na kuhutubia umati wa watu, tofauti kati yao na wengine ni kwamba wao wanajua jinsi ya kutumia hofu hiyo kwa manufaa yao.

Hivyo Kama mwalimu alitakiwa kumsaidia huyo mwanafunzi ambaye Ni rafiki yangu kwa njia nyingine na sio kwa kumpiga na kumdhalilisha kule. Hivyo funzo kwa walimu wetu tunaomba waweze kuwafundisha watoto na kuwapa fursa mbalimbali za kutoa mawazo yao ili kuweza kuwasaidia kujenga tabia ya kujiamini ambayo itasaidia kuweza kusimama na kuongea mbele za watu. Na pia wazazi wanatakiwa kuwalea watoto wao katika mfumo ambao mtoto ataruhusiwa kutoa mchango wake wa mawazo na kusikilizwa,na michango yao kufanyiwa kazi. Hii itasaidia kujenga kujiamini ndani ya mtoto na hivyo kutasaidia awe na uwezo wa kusimama na kuongea mbele za watu bila kuwa na uwoga wala aibu.

Pia wazazi na walimu wanatakiwa kusaidiana kuhakikisha wanaandaa fursa nyingi ambazo zitamjenga mtoto wao katika kujiamini kuongea mbele za watu na kwenye sanaa hii ya uneni, kwasababu kama msemo wa kiingereza unavyosema “ Practice makes Perfect”, ikimaanisha , “Mazoezi hukamilisha” hivyo tujitahidi kuwafanya watoto wetu waweze wakafanya mazoezi mengi ilikuweza kuwapa uzoefu katika hili.

Kama nilivyoeleza hapo awali kwamba kila mtu huwa na hofu kabla ya kusimama na kutoa mawazo au hotuba yake mbele za watu hivyo kuwa na hofu Ni kitu ambacho hakikwepeki na wala usihangahike kutafuta njia za kuhakikisha unaondoa hofu moyoni mwako maana utajisumbua bure, kwakuwa hata wabobezi huwa na hofu kidogo.

Hivyo sitajajaribu kutoa mbinu za kuondoa hii hofu ila nitakupa njia za kufanya ambazo zitasaidia kuongeza kujiamini kwako na kupunguza hofu wakati unatakiwa kuwasilisha mawazo yako mbele ya umati wa watu.

MBINU YA KWANZA: MSHIRIKISHE MUNGU KATIKA MAADALIZI YAKO NA JINENEE MANENO MAZURI;
Haijalishi wewe ni Mkrisro , Muislamu au dini nyingine yoyote, kitu cha muhimu ni sala kabla ya kitu chochote. Na ndivyo ilivyo hata kwenye sanaa hii.

Unapo Sali unamkaribisha Mungu aweze kuwa pamoja nawe na kukuongoza wakati wa kuongea na kutoa kwako mawazo mbele za watu. Mfano mzuri ni Mimi mwenyewe, nakumbuka sana wasilisho letu la GM 200 ya mwaka wa kwanza, tulianza na kumuomba Mungu tukiwa nje ya darasa kabla ya kuingia darasani. Na baada ya hapo nakumbuka tulikuwa tukiambiana kuwa siku ya leo tutatoa wasilisho letu vizuri na tatafanya vizuri sana. Nakumbuka baada ya uwasilishaji mwalimu alitupongeza sana na kusema kuwa sisi ndio tulio ongea vizuri kuliko vikundi vingine vyote.

Hivyo kabla ya kila kitu Sali kwasababu hii husaidia kupunguza hofu, kwa maana unajua hauko peke yako, na pia ukimaliza kusali jinenee kitu , jinenee mambo mazuri unayoyataka yatokee pale ambapo utaenda kutoa mawazo yako mbele za watu.

MBINU YA PILI:
FANYA MAZOEZI BARABARA ;
Fanya mazoezi barabara: Nadhani Sababu kuu ya mtu kushindwa kuongea mbele za watu ni kukosa maandalizi ya kutosha . Sasa utawambia nini watu Kama haujajiandaa? Hivyo pale tu unapopewa taarifa kuwa utatakiwa kwenda kutoa hotuba mbele za watu itabidi uchukue muda wa kuisoma hiyo mada na kuielewa , kuifanyia utafiti kwenye mitandao na hata kwa watu wengine ili uweze kupata uelewa zaidi na upande wa pili wa hiyo mada.

Mfano mzuri nilikuwa nataka nifanye tafiti kuhusu utamaduni wetu wa kutoa mahali pale mwanaume anapotaka kuoa, nilisoma kuhusu hili sana mitandaoni na nikajiona nimeelewa Sana, lakini nilipokuja kushirikisha wenzangu ndipo nilipogundua kuwa sikuwa nimefanya utafiti wa kutosha kwakuwa walikuwa wanna mtazamo mwingine tofati kinyume na mimi na waliongea vitu ambavyo vilinifanya nifikirie sana kabla ya kujibu.

Na pia nilipata kujua upande mwingine, maana kwa upande wangu nilipna hii ni tatizo kwanini mpaka leo tunatoa mahali wakati tulishasoma kuwa mahali inashusha hazi ya mwanamke? Lakini wenzangu kwa upande wao hawakuliona kama Ni tatizo kabisa hivyo hii ilinipa changamoto kwasababu utatatuaje tatizo ambalo jamii yako halilioni kama Ni tatizo? Hivyo ilinipa changamoto ya juanza kuwaelewesha na kuwaonyesha jinsi gani hii mada ni tatizo katika jamii yetu.

MBINU YA TATU: VAA VIZURI;
Mbinu hii ni ya muhimu kwasababu itasaidia kuongeza kujiamini kwako wakati unapokuwa ukiongea na watu na pia inaepusha kuto kuondoa wasikilizaji wako kutoka kwenye kuisikiliza mada yako kwenda kukutathmini mavazi uliyo yavaa pale ambapo umevaa vibaya.

Na uvaaji utategemea na mahali unapotakiwa kuyoa hotuba yako, Kama unaenda kutoa mawazo yako kwa watu Kama wanasheria suti itakuwa Ni nguo iliyobora kwao , itawafanya wakuchukulie Kama mmoja wao, na kama utaenda kuongea na watu labda mafundi itabidi uvae nguo ambazo itawafanya wakuchukulie Kama mwezao tofauti na ukivaa suti, wanaweza wakakuona kuwa wewe sio sawa nao. Lakini mwandishi mkubwa James Mwang'amba ameshauri kuwa katika kitabu chake cha EFFECTIVE PUBLIC SPEAKING AND PRESENTATION SKILLS kuwa, “ni bora uvae suti kama ukifika sehemu ukagundua kuwa hadhira yako hawajavaa aina hiyo ya nguo, unaweza kuvua koti, na kukunja shati ili kuonekana Kama wao, kuliko uende umevaa kawaida au vibaya na ukute hadhira yako wamevaa suti , utalitoa wapi koti?”

Mbinu ya nne na ya mwisho, fanya majaribio ya kutoa hotuba yako mbele za watu, mbele ya watu wachache , inaweza ikawa wanafunzi wenzako, wazazi wako, mke au mume wako. Kufanya hivi kutakufanya uzoefu wa kuongea mbele za watu na kupunguza hofu, pia kutakuwezesha kutamka maneno ambayo ni magumu kutamka. Mimi katika maandalizi yangu ya kutoa mawazo yangu kuhusu somo husika chuoni huwa ninasimama mbele ya rafiki zangu na kuwaomba wanisikilize na baada ya kutoa hotuba yangu , huwa nawauliza wanaonaje hotuba hiyo niliyoitoa na kuchukua michango yao na kuifanyia kazi ili kuifanya hotuba yangu kuwa nzuri zaidi.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anae zaliwa akiwa anajua kuongea mbele za watu, hii sanaa ya uneni ,Ni Sanaa Kama Sanaa nyingine zozote ambazo hufundishwa , hivyo usijione umeshindwa kunachohitajika ni utayari katika kujifunza, soma vitabu kuhusu Sanaa hii ya uneni na ukikosea usivunjike moyo, jaribu tena na tena mwishowe utakuwa muongeaji mzuri na kuweza kugusa maisha ya watu wengi kwa hotuba zako.
 
1. Tunalelewa bila ya kuwa nq uhuru wa kutoa mawazo kwenye familia zetu, siku zote mtoto ni wa kutekeleza tu na haruhusiwi kuuliza maswali au kutoa hoja yoyote ambayo itafunua makosa ya wakubwa zake. Hii inatujengea hofu ya kutokuwa huru na vile tunavyowaza (insecurities)

2. Elimu inaanza na kuishia kwenye chumba cha mtihani, unasoma ili ufauli mtihani lakini sio kutengenezwa kujiamini au kuwa huru au kupata critical thinking

mwisho wa siku yanayoanzia katika familia, yanakaziwa zaidi na jamii + mfumo mbovu wa elimu. Mwisho wa siku ndio unatupata zile products unazoziona
 
Nadhani hapo kuna suala la low self-esteem, poor social skills nat

1. Tunalelewa bila ya kuwa nq uhuru wa kutoa mawazo kwenye familia zetu, siku zote mtoto ni wa kutekeleza tu na haruhusiwi kuuliza maswali au kutoa hoja yoyote ambayo itafunua makosa ya wakubwa zake. Hii inatujengea hofu ya kutokuwa huru na vile tunavyowaza (insecurities)

2. Elimu inaanza na kuishia kwenye chumba cha mtihani, unasoma ili ufauli mtihani lakini sio kutengenezwa kujiamini au kuwa huru au kupata critical thinking

mwisho wa siku yanayoanzia katika familia, yanakaziwa zaidi na jamii + mfumo mbovu wa elimu. Mwisho wa siku ndio unatupata zile products unazoziona
Well said. Kwakuwa ngazi ya familia ndo sehemu kuu ya kumkuza mtoto nakama anakosa Uhuru wa kujieleza haitawezekana kwake kupata hali ya kujiamini akikua. So malezi Ni changamoto ya kwanza.
 
“According to most studies, people’s number one fear is Public speaking. Number two is death. Death is number two. Does that sound right? This means to the average person, if you go to a funeral, you’re better off in the casket than delivering the eulogy.”- Jerry Seinfeld, Comedian.
“ Kutokana na tafiti nyingi zilizofanywa, hofu ya kuzungumza mbele za watu ndio hofu kubwa kuliko hofu zote duniani. Hofu namba mbili ni hofu ya kifo. Au siyo? Hi ina maana kwa mtu wa kawaida, aliyeko msibani, anaona ni bora awe mtu aliye kwenye jeneza kuliko yule mtu anayetakiwa kusoma wasifu wa marehemu!”- Jerry Seinfeld, Mchekeshaji.
Unaweza ukashangazwa na hayo yaliyosemwa na muda mwingine ukakataa kabisa kuyaamini, lakini haya ni mambo ya ukweli ambayo yanatokea na tunayaona kila siku. Nikiwa shule nakumbuka wenzangu walikuwa wako radhi watoroke katika kusanyiko (assembly) ili mradi tu wasije wakaitwa mbele kutoa hotuba (Morning speech) mbele ya watu. Walikuwa wanatoroka ihali wakijua watapata adhabu baadae. Kwahiyo walikuwa wako radhi kupata adhabu kuliko kusimama mbele na kutoa mawazo yao mbele ya wanafunzi wenzao.

Kuna baadhi hushindwa kabisa kuongea wakifika mbele za watu, mfano mzuri ni rafiki yangu mmoja niliyesoma nae kidato cha Tano , yeye alilazimishwa kusimama mbele ya darasa na kuzungumza nasi kuhusu jinsi alivyoelewa somo ambalo mwalimu alilifundisha, yeye hakuweza hata kutuangalia , kwa jinsi alivyokuwa na hofu alianza kulia pale mbele.
Lakini kilichonisikitisha zaidi ni kile mwalimu alichokifanya, nakumbuka mwalimu alimpiga sana huyo rafiki yangu pamoja na kusema maneno mabaya na yenye kejeli na kumdhihaki, kwasababu anashangazwa kwa mtu mzima kama yeye ni aibu kushindwa kuongea mbele za watu.

Kwanza napenda kusema kuwa kushindwa kuongea mbele za watu hakumaanishi kuwa wewe ni mjinga au huna akili au haufai. Na sio kitu cha kumfanya umcheke au kumdharau mtu kama jinsi mwalimu wangu alivyo mfanyia rafiki yangu. Kuwa na hofu hiyo ni kitu cha kawaida, na hata wale waliobobea kwenye sanaa hii ya uneni huwa wanakuwa na hofu kabla ya kusimama na kuhutubia umati wa watu, tofauti kati yao na wengine ni kwamba wao wanajua jinsi ya kutumia hofu hiyo kwa manufaa yao.

Hivyo Kama mwalimu alitakiwa kumsaidia huyo mwanafunzi ambaye Ni rafiki yangu kwa njia nyingine na sio kwa kumpiga na kumdhalilisha kule. Hivyo funzo kwa walimu wetu tunaomba waweze kuwafundisha watoto na kuwapa fursa mbalimbali za kutoa mawazo yao ili kuweza kuwasaidia kujenga tabia ya kujiamini ambayo itasaidia kuweza kusimama na kuongea mbele za watu. Na pia wazazi wanatakiwa kuwalea watoto wao katika mfumo ambao mtoto ataruhusiwa kutoa mchango wake wa mawazo na kusikilizwa,na michango yao kufanyiwa kazi. Hii itasaidia kujenga kujiamini ndani ya mtoto na hivyo kutasaidia awe na uwezo wa kusimama na kuongea mbele za watu bila kuwa na uwoga wala aibu.

Pia wazazi na walimu wanatakiwa kusaidiana kuhakikisha wanaandaa fursa nyingi ambazo zitamjenga mtoto wao katika kujiamini kuongea mbele za watu na kwenye sanaa hii ya uneni, kwasababu kama msemo wa kiingereza unavyosema “ Practice makes Perfect”, ikimaanisha , “Mazoezi hukamilisha” hivyo tujitahidi kuwafanya watoto wetu waweze wakafanya mazoezi mengi ilikuweza kuwapa uzoefu katika hili.

Kama nilivyoeleza hapo awali kwamba kila mtu huwa na hofu kabla ya kusimama na kutoa mawazo au hotuba yake mbele za watu hivyo kuwa na hofu Ni kitu ambacho hakikwepeki na wala usihangahike kutafuta njia za kuhakikisha unaondoa hofu moyoni mwako maana utajisumbua bure, kwakuwa hata wabobezi huwa na hofu kidogo.

Hivyo sitajajaribu kutoa mbinu za kuondoa hii hofu ila nitakupa njia za kufanya ambazo zitasaidia kuongeza kujiamini kwako na kupunguza hofu wakati unatakiwa kuwasilisha mawazo yako mbele ya umati wa watu.

MBINU YA KWANZA: MSHIRIKISHE MUNGU KATIKA MAADALIZI YAKO NA JINENEE MANENO MAZURI;
Haijalishi wewe ni Mkrisro , Muislamu au dini nyingine yoyote, kitu cha muhimu ni sala kabla ya kitu chochote. Na ndivyo ilivyo hata kwenye sanaa hii.
Unapo Sali unamkaribisha Mungu aweze kuwa pamoja nawe na kukuongoza wakati wa kuongea na kutoa kwako mawazo mbele za watu. Mfano mzuri ni Mimi mwenyewe, nakumbuka sana wasilisho letu la GM 200 ya mwaka wa kwanza, tulianza na kumuomba Mungu tukiwa nje ya darasa kabla ya kuingia darasani. Na baada ya hapo nakumbuka tulikuwa tukiambiana kuwa siku ya leo tutatoa wasilisho letu vizuri na tatafanya vizuri sana. Nakumbuka baada ya uwasilishaji mwalimu alitupongeza sana na kusema kuwa sisi ndio tulio ongea vizuri kuliko vikundi vingine vyote.
Hivyo kabla ya kila kitu Sali kwasababu hii husaidia kupunguza hofu, kwa maana unajua hauko peke yako, na pia ukimaliza kusali jinenee kitu , jinenee mambo mazuri unayoyataka yatokee pale ambapo utaenda kutoa mawazo yako mbele za watu.

MBINU YA PILI:
FANYA MAZOEZI BARABARA ;
Fanya mazoezi barabara: Nadhani Sababu kuu ya mtu kushindwa kuongea mbele za watu ni kukosa maandalizi ya kutosha . Sasa utawambia nini watu Kama haujajiandaa? Hivyo pale tu unapopewa taarifa kuwa utatakiwa kwenda kutoa hotuba mbele za watu itabidi uchukue muda wa kuisoma hiyo mada na kuielewa , kuifanyia utafiti kwenye mitandao na hata kwa watu wengine ili uweze kupata uelewa zaidi na upande wa pili wa hiyo mada. Mfano mzuri nilikuwa nataka nifanye tafiti kuhusu utamaduni wetu wa kutoa mahali pale mwanaume anapotaka kuoa, nilisoma kuhusu hili sana mitandaoni na nikajiona nimeelewa Sana, lakini nilipokuja kushirikisha wenzangu ndipo nilipogundua kuwa sikuwa nimefanya utafiti wa kutosha kwakuwa walikuwa wanna mtazamo mwingine tofati kinyume na mimi na waliongea vitu ambavyo vilinifanya nifikirie sana kabla ya kujibu. Na pia nilipata kujua upande mwingine, maana kwa upande wangu nilipna hii ni tatizo kwanini mpaka leo tunatoa mahali wakati tulishasoma kuwa mahali inashusha hazi ya mwanamke? Lakini wenzangu kwa upande wao hawakuliona kama Ni tatizo kabisa hivyo hii ilinipa changamoto kwasababu utatatuaje tatizo ambalo jamii yako halilioni kama Ni tatizo? Hivyo ilinipa changamoto ya juanza kuwaelewesha na kuwaonyesha jinsi gani hii mada ni tatizo katika jamii yetu.

MBINU YA TATU: VAA VIZURI;
Mbinu hii ni ya muhimu kwasababu itasaidia kuongeza kujiamini kwako wakati unapokuwa ukiongea na watu na pia inaepusha kuto kuondoa wasikilizaji wako kutoka kwenye kuisikiliza mada yako kwenda kukutathmini mavazi uliyo yavaa pale ambapo umevaa vibaya.
Na uvaaji utategemea na mahali unapotakiwa kuyoa hotuba yako, Kama unaenda kutoa mawazo yako kwa watu Kama wanasheria suti itakuwa Ni nguo iliyobora kwao , itawafanya wakuchukulie Kama mmoja wao, na kama utaenda kuongea na watu labda mafundi itabidi uvae nguo ambazo itawafanya wakuchukulie Kama mwezao tofauti na ukivaa suti, wanaweza wakakuona kuwa wewe sio sawa nao. Lakini mwandishi mkubwa James Mwang'amba ameshauri kuwa katika kitabu chake cha EFFECTIVE PUBLIC SPEAKING AND PRESENTATION SKILLS kuwa, “ni bora uvae suti kama ukifika sehemu ukagundua kuwa hadhira yako hawajavaa aina hiyo ya nguo, unaweza kuvua koti, na kukunja shati ili kuonekana Kama wao, kuliko uende umevaa kawaida au vibaya na ukute hadhira yako wamevaa suti , utalitoa wapi koti?”
Mbinu ya nne na ya mwisho, fanya majaribio ya kutoa hotuba yako mbele za watu, mbele ya watu wachache , inaweza ikawa wanafunzi wenzako, wazazi wako, mke au mume wako. Kufanya hivi kutakufanya uzoefu wa kuongea mbele za watu na kupunguza hofu, pia kutakuwezesha kutamka maneno ambayo ni magumu kutamka. Mimi katika maandalizi yangu ya kutoa mawazo yangu kuhusu somo husika chuoni huwa ninasimama mbele ya rafiki zangu na kuwaomba wanisikilize na baada ya kutoa hotuba yangu , huwa nawauliza wanaonaje hotuba hiyo niliyoitoa na kuchukua michango yao na kuifanyia kazi ili kuifanya hotuba yangu kuwa nzuri zaidi.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anae zaliwa akiwa anajua kuongea mbele za watu, hii sanaa ya uneni ,Ni Sanaa Kama Sanaa nyingine zozote ambazo hufundishwa , hivyo usijione umeshindwa kunachohitajika ni utayari katika kujifunza, soma vitabu kuhusu Sanaa hii ya uneni na ukikosea usivunjike moyo, jaribu tena na tena mwishowe utakuwa muongeaji mzuri na kuweza kugusa maisha ya watu wengi kwa hotuba zako.
Vijana wengi kiasi gani na wa wapi?
 
Lwel
1. Tunalelewa bila ya kuwa nq uhuru wa kutoa mawazo kwenye familia zetu, siku zote mtoto ni wa kutekeleza tu na haruhusiwi kuuliza maswali au kutoa hoja yoyote ambayo itafunua makosa ya wakubwa zake. Hii inatujengea hofu ya kutokuwa huru na vile tunavyowaza (insecurities)

2. Elimu inaanza na kuishia kwenye chumba cha mtihani, unasoma ili ufauli mtihani lakini sio kutengenezwa kujiamini au kuwa huru au kupata critical thinking

mwisho wa siku yanayoanzia katika familia, yanakaziwa zaidi na jamii + mfumo mbovu wa elimu. Mwisho wa siku ndio unatupata zile products

1. Tunalelewa bila ya kuwa nq uhuru wa kutoa mawazo kwenye familia zetu, siku zote mtoto ni wa kutekeleza tu na haruhusiwi kuuliza maswali au kutoa hoja yoyote ambayo itafunua makosa ya wakubwa zake. Hii inatujengea hofu ya kutokuwa huru na vile tunavyowaza (insecurities)

2. Elimu inaanza na kuishia kwenye chumba cha mtihani, unasoma ili ufauli mtihani lakini sio kutengenezwa kujiamini au kuwa huru au kupata critical thinking

mwisho wa siku yanayoanzia katika familia, yanakaziwa zaidi na jamii + mfumo mbovu wa elimu. Mwisho wa siku ndio unatupata zile products unazoziona
Nmekuelewa vyema sana chief, mm ni mhanga wa hili Mzazi wangu(Baba) alinitenegenezea mazingira ya kuwa na hofu sana hata nilipohisiwa kufanya kosa hata kama sio halali nikitaka kujietetea basi anakuambia nani kakufundishia kuongea mbele ya wakubwa so iliniathiri sana makuzi yangu nikawa mtu wa kupenda kukaa pekee yangu mpaka baada ya kwenda kidato cha 5 na 6..
 
Back
Top Bottom