DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,212
- 4,515
Bila shaka hata huko mtaani kwako wapo vijana waliotumikia pale mbele Altare ya Bwana maisha yao Leo hii hawana habari na Mungu wala kanisa.
Maana kanisa liliwalea ili siku wajiunge na Seminary na hatimae kuja kuwa mababa wa baadae.
Lakini tofauti unakuta ni mmoja kwa kumi aliyeenda Seminari wengine wote walitokomea na kuachana kabisa na habari za Kanisa.
Mimi maisha yangu yooote ya utotoni hadi ujana nimeishi madhabahuni. Mzee wangu alikuwa askifu, kaka yangu mmoja naye kwa sasa ni askofu, mwingine ni mchungaji.
Mimi nilifikia hatua nikawa katibu Mkuu wa umoja wa vijana taifa, ila nilivyojitafakari na kusafiri sana, nilivyoona kanisha linavyoendeshwa, kuna ufuska, utapeli na uwongo mkubwa ndani ya kanisa.
Lakini kubwa zaidi kilichonitoa kanisani zaidi ni kitendo cha kutambua siri iliyopo nyuma ya dini hususani kwa muafrika. Niliamua kujiweka pembeni kabisa.