Kwanini vijana/watoto wengi waliotumikia Altareni Leo hii asilimia kubwa sio watu wa dini wala kusali

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
1,301
2,000
Bila shaka hata huko mtaani kwako wapo vijana waliotumikia pale mbele Altare ya Bwana maisha yao Leo hii hawana habari na Mungu wala kanisa.

Maana kanisa liliwalea ili siku wajiunge na Seminary na hatimae kuja kuwa mababa wa baadae.

Lakini tofauti unakuta ni mmoja kwa kumi aliyeenda Seminari wengine wote walitokomea na kuachana kabisa na habari za Kanisa.

Mimi maisha yangu yooote ya utotoni hadi ujana nimeishi madhabahuni. Mzee wangu alikuwa askifu, kaka yangu mmoja naye kwa sasa ni askofu, mwingine ni mchungaji.

Mimi nilifikia hatua nikawa katibu Mkuu wa umoja wa vijana taifa, ila nilivyojitafakari na kusafiri sana, nilivyoona kanisha linavyoendeshwa, kuna ufuska, utapeli na uwongo mkubwa ndani ya kanisa.

Lakini kubwa zaidi kilichonitoa kanisani zaidi ni kitendo cha kutambua siri iliyopo nyuma ya dini hususani kwa muafrika. Niliamua kujiweka pembeni kabisa.
 

Manton

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,161
2,000
Ni kwa sababu hawafundishwi kuhusu Jesus na imani.There is really nothing special.Most of them they dont even believe that Jesus is God.Do your research and you will see.
Yule aitwaye, Maria mzazi, mama wa Mungu unamjua (Salamu Maria)! Maana hakuna mwana bila mama, na hakuna mama bila baba. Yaani uko mbali sana, soma vitabu sana upate ufunuo wa imani na makanisa zaidi ya ule wa Yohana.
 

Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
4,694
2,000
Ungedadavua kidogo kuhusu hao masista na mapadre, mpaka kupelekea kukufanya mtu kukosa appetite ya kuingia church, pindi tu unapojua mambo yao kama ulivyotudokeza mkuu
Ndani zitaenda sana ili kulinda heshima na faragha.

Wale ni binadamu kama tulivyo sisi na wanahisia kama sisi, hisia za kingono.
Unapokua karibu nao ndio unajua namna wanvyojihusisha nayo.

Lakini katika mambo ya uchumi wale ni watufutaji kama wengine tulivyo na katika kutafuta kwao wana dhulumu wanatapeli wana lalia watu nk.

Kama hauna hela, yaani muumini kama wewe hauna hela moja kwa moja hauna nafasi kwao.

Ukitaka huduma kwao wanaangalia kwanza wewe ni nani , kama ni wakaida huenda wasikuhudumie au wakupe huduma hafifu.

Lakini ukiwa na hela huduma inaukufuata mpaka nyumbani kwako.

Kwa ufupi ni binadamu kama sisi, wana roho mbaya, ni wachawi wengine, ni wazinzi wengine, ulevi tusihesabu sana maana pombe sio dhambi kwao.

Haya yote na kuzidi utayapata kuyajua ukiwa karibu nao, na mengi zaidi, na sio wao tu hata maaskofu wao, na wengine ukaribu inavyozidi wanajifungulia n Siri za maandiko.

Kuna mmoja alishawahi kuniambia sirius hakuna jehanamu wala kiyama wala hakuna mbingu au pepo.
 

Muscovy

Senior Member
May 19, 2019
144
250
Mimi ni mmoja wao mkuu wakati nipo primary nilikuwa mwana shirika wa St. Aloysius Gozanga (Patron saint of Roman Catholic Youth) nimetumikia sana.

Secondary nikaenda seminary Salesian Seminary (Don Bosco) mpaka form six. Itoshe tu kusema exposure ya kanisa niliyonayo ni yakutosha kuzidi walei wengi.

Lakini nadhani hiyo exposure ilinifanya nifike mahali nisite kuendelea na wito wangu wa kuwa parde na mpaka sasa sio muumini wakueleweka.
Hatuna tofauti mkuuu nilianza utumikizi nikiwa darasa la tatu Hadi form 4 .....ukinikosa nyumbani njoo parokiani utanikuta ilifika mahali kengele Misa ya asbh ikipgwa nikiwa mbali na Anza kukimbia niweze kuwah rozali na Misa baaada ya kuacha kutumikia nilikuwa mvivu Sana wa kusali Mungu mwema now nimerud kwenye line Kama muumin wa kawaida

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 

COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
2,136
2,000
Mimi maisha yangu yooote ya utotoni hadi ujana nimeishi madhabahuni. Mzee wangu alikuwa askifu, kaka yangu mmoja naye kwa sasa ni askofu, mwingine ni mchungaji.

Mimi nilifikia hatua nikawa katibu Mkuu wa umoja wa vijana taifa, ila nilivyojitafakari na kusafiri sana, nilivyoona kanisha linavyoendeshwa, kuna ufuska, utapeli na uwongo mkubwa ndani ya kanisa.

Lakini kubwa zaidi kilichonitoa kanisani zaidi ni kitendo cha kutambua siri iliyopo nyuma ya dini hususani kwa muafrika. Niliamua kujiweka pembeni kabisa.
Ndo mtuambie hiyo Siri NASISI tuijue tuachane na huo uzwazwa
 

Babuyao

JF-Expert Member
Jun 6, 2009
1,741
1,500
Inatokeaga , ndio mana Yesu alizungumza kuhusu mbegu za mwibani
mimi mwenyewe niliasi kanisani Almost miaka 15 katika hio 15 nimeenda kanisani hata mara 10 haifiki na kulikua na sababu maalum niliasi mpaka nikawa na Phobia ya kwenda kanisani, na hii phobia wanayo wengi sana... kuna watu unakuta wanawish waende ila akijiangalia anasema ntaanzia wapi kuingia.

Yani watu tuliasi tangu enzi ya "bwana awe pia nawe", tunekuja kurudi " Awe rohoni mwako"
miezi mi2 ya mwanzo nilipata shida sana kutoka kwa wanaonijua unaingia church watu wanakuangalia utasema uliwaambia ntakuja na shetani
Ila mwisho wa siku tumerudi na maisha yanasonga. Kwahiyo tuwaombee ipo siku tu.

Sent from
Wewe dada umenichekesha sana bado asubuhi. Ila hongera kwa kurudi tena kanisani.
 

Babuyao

JF-Expert Member
Jun 6, 2009
1,741
1,500
Bila shaka hata huko mtaani kwako wapo vijana waliotumikia pale mbele Altare ya Bwana maisha yao Leo hii hawana habari na Mungu wala kanisa.

Maana kanisa liliwalea ili siku wajiunge na Seminary na hatimae kuja kuwa mababa wa baadae.

Lakini tofauti unakuta ni mmoja kwa kumi aliyeenda Seminari wengine wote walitokomea na kuachana kabisa na habari za Kanisa.
Familiarity breeds contempt. Kukaaa sana altareni na kuyazoea mno mambo matakatifu wakati mwingine kunaweza kuondoa ile hofu ya Mungu na matakatifu yake na kumfanya mtu ayaone mambo ya kawaida tu na hivyo kupoteza hamasa ya maisha ya kiroho
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,795
2,000
Hatuchekani kabisa, juzi nililazimika kuingia misa ya mazishi maana aliefariki alikua mzito parokiani, basi daah bado kidogo niumbuke niliacha tunaanza na maji pale mlangoni lakini sasahivi hamna, ile ‘tutakiane amani’ sasahivi mambo ni tofauti.
Matokeo ya korona hayo!
 
  • Thanks
Reactions: R.K

neyro

JF-Expert Member
Apr 27, 2011
232
225
Kusoma kwako vitabu hakujakusaidia.Waliosoma sana vitabu wamekutana na maswali mengi ambayo sayansi imeshindwa kujibu na imani imejibu zamani sana. I am talking scientist kama akina Stephen Hawkings na wengine.
I second you!
Na hata hao anao Refer wote ni pro Christianity
Napata shaka na ground yake aliyoisimamia
 

princess ariana

JF-Expert Member
Aug 19, 2016
6,238
2,000
Tatizo watu wengi wanajaribu kufuata dini na viongozi wake lakini sio imani juu ya Yesu.

In my part the more i started to understand about faith the more i wanted to know.And i am happy i got to understand more about Christian faith.
Naunga mkono hoja!
watu wengi wanawazingatia hawa mababa na mama wa kiroho kuliko neno lenyewe.
Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Luka 8:21

Lakini Yesu akawaambia watu wote, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika.”

Yani kikubwa kuliko vyote ni neno la Mungu na kulishika! Ukiweza hapa mengine yote yatakua ziada Watumishi wa Mungu wako pale kukukumbusha na kufundisha neno.

Sent from
 

Kwisimla

Senior Member
Apr 15, 2011
154
225
Ndani zitaenda sana ili kulinda heshima na faragha.

Wale ni binadamu kama tulivyo sisi na wanahisia kama sisi, hisia za kingono.
Unapokua karibu nao ndio unajua namna wanvyojihusisha nayo.
Viongozi wa dini ni watu kama wengine kabisaa. Kwa hiyo kati yao wapo ambao wana imani na ambao hawana! Mwenyezi Mungu ameruhusu. Kama mwingine alivyoeleza huko juu, kuwa na imani kwa Mungu na dini ni suala la kuongozwa na Roho Mtakatifu, si suala kulala na kuamka umeamua! Na ndio maana husemwa "wanaoitwa ni wengi lakini wateule ni wachache".
 

Mbwa dume

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
4,090
2,000
Bila shaka hata huko mtaani kwako wapo vijana waliotumikia pale mbele Altare ya Bwana maisha yao Leo hii hawana habari na Mungu wala kanisa.

Maana kanisa liliwalea ili siku wajiunge na Seminary na hatimae kuja kuwa mababa wa baadae.

Lakini tofauti unakuta ni mmoja kwa kumi aliyeenda Seminari wengine wote walitokomea na kuachana kabisa na habari za Kanisa.
Ni wapiga pombe wazuri pia hupenda Sana chini halafu Kuna mmoja mdingi tunapigaga naye nyeto anasema aliwahi kufanya hizo mishe za kikanisa enzi ya ujana wake
 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
2,441
2,000
Wengi ya tuliokua karibu Sana na hizi dini hapo mwanzo ndio sisi Kwa idadi kubwa ni
Non believer, Atheists,Theism nk
Mwanzo nilijikita kusoma vitabu vya mwanzo na kuchambua kitabu Cha ufunuo in deep
Katika kuchimba Sana historia nikaja gundua hata Abraham aliabudu miungu ANNUNAKI maana alikua ni jamaa kutoka kabila za waashuru wa kale na hata hivyo chanzo Cha kuanza kumwabudu mungu El ni baada ya kukutana na mfalme wa Salem Merchizedec ambaye inasadikika alikua ni kiumbe mtu kutoka Garaxy za Andromeda's

So nikaja kujua dini ni propaganda Kali Sana za kuwafunga fahamu watu,wakazi halisi wa Dunia tujione hapa sio kwetu na hii Dunia inamilikiwa na kiumbe anayeitwa Mungu Ili tuendelee kua watumwa wa fikra na ndio maana Kwa maelfu ya miaka binadamu tulikua duni Sana tukiishi kwenye Dunia local sababu ya hizo mambo mpaka pale karne kadhaa nyuma baadhi yetu walipoanza kufunguka akili na kujijua wao ni wakazi halisi wa Dunia na wakaanza pata fahamu za kupiga hatua kimaendeleo na vumbuzi mpaka tulipofikia angalau
Natumaini ipi siku Dunia itaenda na watu wataenda kupiga hatua kubwa kimaendeleo tufanane na jamii nyingine za viumbe kutoka galaxies za mbali!
 

mbaritsamenya

JF-Expert Member
Apr 28, 2019
409
500
Kwasababu inafika wakati mtu akiweza kutambua mbivu na mbichi za kanisa, upuuzi na ukweli kwamba tunapumbazwa na dini kama kilainisha kurahisisha utawala wa akili zetu basi mtu anaamua kujiweka pembeni.

Dini ni utapeli hususani kwa muafrika haina faida
Nikweli mkuu sematu kanisani tunaenda tuu kwakuwa tulipandikizwa imani hizi tukiwa wadogo lakini ukifikiri kwa umakini dini ni mzigo sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom