Kwanini Vijana Na Wazee Wanapopata Fedha Baada Ya Kutaabika Wanaamua Kunywea Pombe?

XINGLUX

Member
Mar 31, 2008
17
1
Watu wengi sana hasa wachimba madini wananisikitisha sana kuona walikuwa wana taabika lakini baada ya muda baadhi yao huwa wanafanikiwa na inapofikia malengo yao huishia kunywa pombe, wengine kufanya uhuni hasa ngono ambayo ni zembe na kuishia kupata magonjwa ya ukimwi na wengine kuishiwa kabisa fedha walizozipata na kuanza kutaabika tena
Bado sijafahamu ni kwanini? inakuwa hivyo ila nilikuwa nawaomba wajaribu kukumbuka walikotoka kwani maisha sio mchezo na bahati huwa haiji mara mbili na wengine huwa wanachanganyikiwa baada ya kuona maisha yao yanazidi kuwa mabovu
Nategemea vijana wenzangu kuona mnawashauri watu kubadili tabia zao ili kuweza kufikia malengo yao walio yapanga na kusaidia jamii zao
 
vijana naomba mbadili tabia kumbukeni maisha huwa sio rahisi kama mnavyofikiria wengine mnashindwa hata kusaida ndugu zenu na wsazazi wenu whhhyyyyy?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom