Kwanini uwekezaji mkubwa wa kimkakati unaofanywa na Serikali ya awamu ya tano utaongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya watu.

Nov 27, 2019
35
145
Serikali ya awamu ya Tano katika dhamira yake kuu ya kujenga uchumi wa kati wa viwanda, imekuwa ikijenga miundombinu wezeshi ya kufika azima hiyo. Kutokana na miundombinu hiyo ukuaji wa maendeo ya watu unafanyika.Mathalani

Umeboreshaji wa sekta ya elimu kwa kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, sera ya bure lengo likiwani kupata rasilimali watu wenye weledi kwenye kusimamia uchumi huo. Kupitia uboreshaji huo Serikali imefanya maendeleo ya watu wake kwenye eneo la elimu (maarifa na ujuzi).

Uboreshaji wa sekta ya afya kwa Ujenzi wa Hospitali, zahanati, vituo vya afya, kuajili watumishi na kuongeza bajeti ya dawa ili kuhakikisha afya za watanzania zinakuwa dhabiti muda wote. kwa kufanya hivyo Serikali inafanya maendeleo ya watu kwenye eneo la afya.

Usambazaji wa Nishati ya umeme nchi zima kupitia miradi ya REA ambapo maeneo mengi mjini na vijijni yamewekewa umeme na machache yaliyobakia shughuli inaendelea. Upatikanaji wa umeme kwa binadamu unachangia maendeleo yake binafsi kutokana na kutumia nishati hiyo kwa matumizi ya nyumbani na shughuli za kibiashara pia.

Uboreshaji wa huduma za maji ambapo hadi sasa takwimu zinaonesha asilimia 85 ya watu waishio mijini nchini wanapata maji safi na salama huku vijijini ni zaidi ya asilimia 47. Upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi unachagiza maendeleo yao ya kiafya na hata kiuchumi.

Ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano ikiwemo barabara za rami, madaraja, uboreshaji wa viwanja vya ndege n.k maendeleo ya watu hujumuisha kipato chao, kupitia uboreshaji na uimarishaji wa miundombinu unawasaidia wananchi kufanya biashara hasa za mazao ambayo hulimwa kwa wingi vijijini pamoja kupunguza Muda wa kufuata huduma zinazopatikana maeneo mengine.

Nimeona baadhi ya wanaharakati wanatumia ripoti ya Shirika la umoja wa mataifa la maendeleo ya watu ya mwaka 2019 kubeza jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo ya watu, ukweli ni kwamba maendeleo ya vitu 'STRUCTURES' na maendeleo ya watu 'WELL BEING' huenda sambamba na mara nyingi maendeleo ya vitu huleta maendeleo ya watu.

Kwa mchambuzi makini ni vugumu sana kufikia hitimisho la kwamba Serikali ya awamu ya Tano imeshindwa kuongeza kasi ya maendeleo ya watu kwa kuwa miradi yake ni ya kimkakati na ya muda mrefu na hivyo matokeo yake pia yanatarajiwa kuonekana kwa ukubwa baada ya muda.
 
Undp:tafiti zaonyesha maendeleo ya watanzania yamerudi nyuma ukilingwnisha na miaka 2 iliyopita
 
Nimeishia kusoma paragraph ya pili na kuhitimisha kuwa hujui elimu bora ni kitu gani na nini ni muhimu kufanyika ili kuboresha elimu.

Soma hapa chini..

 
Nimeishia kusoma paragraph ya pili na kuhitimisha kuwa hujui elimu bora ni kitu gani na nini ni muhimu kufanyika ili kuboresha elimu.

Soma hapa chini..

Upatikaji wa elimu kwa wote 'access to education' ni jambo la kwanza baadae linakuja swala la ubora
 
Matunda ya uwekezaji mkubwa na wa kimkakati yatachukua muda kidogo kuonekana, kwa watu wanaotazama leo tu yhawawezi kuliona hilo
Ukishauwa demokrasia na sector binafsi huo uchumi wa Viwanda Wa wapi labda Wa majukwaani.Huwezifika uchumi Wa viwanda wakati kilimo kiko ICU
 
Kuna indicator ipi ionyeshayo nafuu mbeleni?
Ongezeko la mapato ya serikali. na matumizi bora ya mapato katika kuwekeza zaidi na kuimarisha miundombinu itakayoongeza mapato zaidi kama miradi ya umeme, kurahisisha miundombinu ya usafiri -ndege, reli na barabara, kutimua wenye vyeti feki, na mengine mengi tu!
 
Ongezeko la mapato ya serikali. na matumizi bora ya mapato katika kuwekeza zaidi na kuimarisha miundombinu itakayoongeza mapato zaidi kama miradi ya umeme, kurahisisha miundombinu ya usafiri -ndege, reli na barabara, kutimua wenye vyeti feki, na mengine mengi tu!

Amekuuliza indicators. Anyway, unapimaje returns za hata ulivyovitaja hapa?
 
Back
Top Bottom